Uwezekano wa kuenea kwa salafi jihadi nchini Tanzania

KAKA NADHAN UNAJUA NIKITUMIA NENO JIHADI NINI NAMAANISHA, ILE ILIYOKUA INAPIGANIWA SOMALIA ILIKUA SI JIHADI BALI ILIKUA NI VITA YA KISIASA BAINA YA AL SHABAAB NA AHLUL SUNNA WAL JAMAA , SOON NTAWEKA UZI KATIKA SUALA ZIMA LA NINI KILICHOPO NDANI YA KIVULI CHA JIHADI. AHSANTE SAANA
Unazidi kudhihirisha ujinga wako. Umelishwa propaganda za kimagharibi,kisha unajitia ujuaji
 
NAJARIBU KUELEZEA KUTOKANA NA MATUKIO YANAYOTOKEA KATIKA NCHI MAJIRANI, NA PIA VILEVILE NIMESEMA ÚWEZEKANO" . NA PIA KAANGALIE MIAKA ILIYOPITA . SIKUSEMA TANZANIA KUNA KAMBI ZA KIGAIDI JIULIZE MBONA TANZANIA TULIKUA TUNAONGOZA KWA KUA NA WAPIGANAJ WA AL SHABAAB SOMALIA. NINGEPENDA ULIFUATILIE SUALA HILI KWA UMAKINI AUN WASILIANA NA MIMI NIKUPE USHAHIDI.
Hebu tupe idadi ya watanzania waliokuwapo alshabaab wakati huo hadi tukaongoza na kuwazidi wasomali
 
Hhhhhhh
Masha Allah
Chief,Mola akubaarik sana
Labda nikuambie jambo moja tu
Quraan pekee,ndio Kitabu Sahihi kisichokuwa na Shaka ndani yake,ama vilivyobaki,ni lazim vitazamwe na kuangaliwa Usahihi wake
Tujifunze kuchunguza kauli hizi tunazozinukuu juu ya usahihi wake,Je!kweli Imam fulani amesema hili....?!!!nk
Kisha
Huwezi kusoma kwa mtu fulani,kisha ukajua kasoro zake,ikiwa ww ni mchanga kielimu,ndio maana nikasema,Tafuta Elimu na Soma ukweli

Twariqa uliyokuwa nayo ya Qaadiriyyah,wengine wetu tulikuwepo huko,kisha tukatoka kwasababu ya kusoma na kuujua ukweli
Bro
Allah akulipe kheri ya Dunia na Akhera
Tusome Dini yetu,Tufuate njia za Wema waliotangulia
Maimam Wanne
Abuu Hanifah
Maalik
Shaafiy
Hanbaly
رحمهم الله
Hakuna hata mmoja aliekuqa Sufi au kusisitiza mtu kusoma au kuwa Sufi,
Lau utafuatilia juu ya usahihi wa maandishi na ukweli wake,utajua hili
Shukran sana
Allah akubaarik
Unaandika kauli ya kujiamini ambayo wewe hauna uhakika nayo zaidi ya kusikia ama kwa kuambiwa na Sheikh wako na ukaitakidi hivyo na makaambiwa Usufi ni bidaa, ni shirki ni kufr! Nini maana ya Usufi? Nijibu, ni nini maana yake?

Tafuta njia ya wema waliyotangulia?! Hii ni kauli ya Salafi! Miongoni mwa nilipochota elimu nimepitia kwa kwa Sheikh wa kisalafi mwaka 2012-2013 na 2014 hivi. Hawafuati haki wanachokifuata ni itikadi tu! Kwamba sisi tupo hivi basi, hata ujeushahidi wa wazi wa namna gani hawafungamani nao kisa upo tofauti na jamuu ya wanawazuoni wanaofuata mwenendo wao. Sikupendezwa! Mimi si mfuasi wa itikadi, mimi ni mfuasi wa haki. Itakapo simama nami nitasimama.

Siwachukii ila wananishangaza kwa wanachokisema ni tofauti na wanachomaanisha. Watu wema waliyotangulia na wanachokifanya wao ni mashariki na magharibi. Watu wema waliyotangulia walishikamana na Usufi, wao hawashikmani nao. Maimam wa 4 walishikamana na Usufi waohawashikamani nao! Ni nini maana ya Usufi? Nijibu.

Nimepitia tafsiri ya Qur'an ya swahaba ya Mtume s.a.w ya Ibn Abas r.a nimeona amezungumzia Usufi upo ndani ya Uislam. Nimepitia tafsiri ya Imam ambaye wanawazuoni wanakubaliana ndiye beberu wa tafsiri ya Qur'an naye ni Imam Qurtubi nimeona kazungumzia Usufi kwa maana upo ndani ya Uislam. Asili ya Usufi imetoka kwa Nabii Ibrahim a.s. Kwenye hadith Mtume s.a.w kaizungumzia na kafanya mpaka dhikri ya Saadiyah. Ni nini maana ya Usufi? Jina linaweza likawa linakuchanganya. Ni nini maana ya Usufi?

Nimekupa marejeleo ya vitabu wewe umenipa maneno matupu na umekanusha. Hujanikanushia kwa marejeleo, umenikanushia kwa taarifa ambayo yeyote anaweza akaiandika, na elimu haikwendi hivyo! Nipe marejeleo ya kukanusha nikavipitie hivyo vitabu. Kwa taarifa yako hili suala nilianza kulichunguza tangu 2017. Sikulichunguza tu hivi hivi. Kwa kila swala niliyoswali imma iwe ya faradhi ama ya sunnah na visimamo vya usiku na mpaka muda huu ninaoandika huwa sichoki na sitochoka kumuomba Mungu aniongoze kwenye njia ya haki.

Mimi si miongoni mwa yule ninayesoma na kuitakidi moja kwa moja kwa ninayofundishwa na ustadhi basi nikayakubali moja kwa moja. Huwa nauliza unachonifundisha ewe Ustadhi nitajuaje kuwa ndiyo dini ya Mtume Muhammad s.a.w? Wakanijibu muombe Mungu akuonyeshe njia ya haki! Namuomba Mungu na huwa sichoki na siriziki nitaendelea kumuomba Mungu anionyeshe njia ya haki, na aufanye moyo wangu uwe mlaini na ufungamane na haki.

Nami nakusihi! Tafuta elimu, soma! Na usome kwa lengo la kuijua haki.
 
Suala la ugaidi lipo, refer Kibiti, Tanga(Amboni) na sasa kwa majirani zetu Mozambique baada ya kushindikana hapa. Vijana wenge wa mikoa ya pwani wamejiingiza kwenye masuala ya kigaidi kwa kivuli cha kupigania uislam.

Vijana wengi wa ukanda wa kusini sasa wanajikuta wanashawishika kuvuka na kujiunga na hili kundi ambalo linasumbua Mozambique,,, kundi hili limekuwa kubwa sasa kwasababu wamefikia hatua ya kuteka mkoa(Refer Mocimboa Da praia 2017) na hivi juzi March 2020 waliteka kambi ya jeshi na kuchukua silaha zote yakiwepo magari ya kijeshi.

The majority of these men are swahili speakers, tena kiswahili cha bongo kabisa wakichanganya na kimwani cha mozambique kaskazini. Wanachinja watu kikatili sana wakitumia mapanga na silaha za kivita(mostly A.K 47).Wanateka mabenki na kuchukua fedha halafu wanatokomea msituni.

Wilaya walizoteka mpaka sasa ni nyingi tu mfano Muidumbe, Macomia na Carbo dela Gardo mpaka hapa Nangade wilaya iliyopo less tha 50km kutoka border yetu.

Nimekuwa huku border since February mwaka huu kwahiyo ninaongea nikiwa kwenye maeneo ambayo hizi taarifa anazijua hata mtoto wa darasa la kwanza. Kikubwa tu nikuelimishana kuwa hizi dini hazipo kwa ajili ya kudhuru bali baadhi ya watu ndiyo wanazitumia vibaya.

Nimeandika kwa uchache sana.

Pundugu.
 
Acha porojo, futeni vifungu vinavyohamasisha na kuhalalisha mauaji kwa waliotofauti na uislamu....
Yale ni maneno ya Mungu, hatuthubutu kuyafuta. Na ukisoma context utaelewa nini kinazungumzwa, sio kuchukua aya moja, na tena hio unapewa na mtu bila wewe kuthibitisha. Hatuna ujinga huo katika uislam.

Hii inaonesha kuwa nyie mmefuta maneno ya Mungu kwenye vitabu vyenu na kuweka ya kwenu ili kukidhi matamanio ya nafsi zenu. That is to say, Christianity is a man made religion yenye kuabudu Mungu zaidi ya mmoja
 
Sisi ktk Biblia Takatifu moja kati ya Amri za Mungu inasema USIABUDU MIUNGU China, India nk wanamiungu yao tofauti na unayoabudu wewe...kwa hiyo ujue kuna miungu mingi...
Allah ni mungu sio Mungu kwa hiyo mnaweza tu kufuta vifungu vinavyoruhusu kuua mkuu.
 
Mungu sio kiumbe kwa sababu hajaaumbwa. Sanamu sio mungu, Mtu hawezi kuitwa Mungu wala kiumbe chochote kile hakiwezi kuwa Mungu.

Na Allah hakuumbwa, hakuzaa wala hakuzaliwa, iweje niabudu kiumbe alichokiumba yeye? Quran ni maneno yake na wala Yesu hawezi kuwa Mungu kwani hana sifa ata moja ya moja. Ni ushirikina kumuabudu Yesu. Nyinyi endeleeni kubadilisha bibilia ili ikidhi matakwa yenu ya kidunia. Sie waislam tunatakiwa tuijenge Akhera yetu zaidi na duniani ni mapito tu.
 
Shida huelewi mkuu allah sio Mungu bali ni mungu. Sanamu ni mungu, mtu anaweza kuwa mungu na viumbe wengi tu wanaweza kufanywa mungu km nyie mnavoabudu majini km miungu yetu baada ya allah na muhamedi.........
Allah hafanani wala hafananishwi na chochote wkt Mungu wa kweli alituumba kwa mfano wake na sura yake. Yesu ni Mungu
 
Suala la ugaidi lipo, refer Kibiti, Tanga(Amboni) na sasa kwa majirani zetu Mozambique baada ya kushindikana hapa. Vijana wenge wa mikoa ya pwani wamejiingiza kwenye masuala ya kigaidi kwa kivuli cha kupigania uislam.

Vijana wengi wa ukanda wa kusini sasa wanajikuta wanashawishika kuvuka na kujiunga na hili kundi ambalo linasumbua Mozambique,,, kundi hili limekuwa kubwa sasa kwasababu wamefikia hatua ya kuteka mkoa(Refer Mocimboa Da praia 2017) na hivi juzi March 2020 waliteka kambi ya jeshi na kuchukua silaha zote yakiwepo magari ya kijeshi.

The majority of these men are swahili speakers, tena kiswahili cha bongo kabisa wakichanganya na kimwani cha mozambique kaskazini. Wanachinja watu kikatili sana wakitumia mapanga na silaha za kivita(mostly A.K 47).Wanateka mabenki na kuchukua fedha halafu wanatokomea msituni.

Wilaya walizoteka mpaka sasa ni nyingi tu mfano Muidumbe, Macomia na Carbo dela Gardo mpaka hapa Nangade wilaya iliyopo less tha 50km kutoka border yetu.

Nimekuwa huku border since February mwaka huu kwahiyo ninaongea nikiwa kwenye maeneo ambayo hizi taarifa anazijua hata mtoto wa darasa la kwanza. Kikubwa tu nikuelimishana kuwa hizi dini hazipo kwa ajili ya kudhuru bali baadhi ya watu ndiyo wanazitumia vibaya.

Nimeandika kwa uchache sana.

Pundugu.
Vipi kuhusu hatua ilizochukua Serikali ya huko kuwasambaratisha hawa magaidi, je zinafanikiwa?
 
Shida huelewi mkuu allah sio Mungu bali ni mungu. Sanamu ni mungu, mtu anaweza kuwa mungu na viumbe wengi tu wanaweza kufanywa mungu km nyie mnavoabudu majini km miungu yetu baada ya allah na muhamedi.........
Allah hafanani wala hafananishwi na chochote wkt Mungu wa kweli alituumba kwa mfano wake na sura yake. Yesu ni Mungu
Shida huelewi na hujui tofauti ya Mungu na mungu. Allah ni Mungu, na vyengine vyote mkivifanya mungu basi mnafanya ushirikina. Yaani kama ni mtu wa kutumia akili, utajua kuwa Mungu hawezi kufananishwa na chochote, kwa sababu Sifa za Mungu sio sifa za kiumbe. Mwenye akili zake timamu hawezi kuamini kuwa mungu anazaliwa tena baada ya kumpa mimba mama yake.

Yesu amesema kuwa yeye ni mtu, nakushangaeni mnampa sifa ambayo hajakwambieni mumpe. Lakini hii yote ni kwa sababu badala ya kusoma maneno ya Mungu, mnasoma vitabu ambavyo waandishi wake hawajulikani bali wanadhaniwa tu. Na tena bado vikiwa vimebadilishwa.

Huwezi kutufananisha sie tunasoma Maneno ya Mungu na nyinyi mnaosoma maneno MNAYODHANIA yameandikwa na akina mattayo, joni n.k
 
Ungetumia kiswahili tu😂😂😂😂

Ugaidi tena ukiingia hapa kwetu, watafanikiwa sana ku recruit sio waislamu tu hata wa dini nyingine,it all about money and we poor,others are eating good others are starving.Unadhani itakuwa ngumu kujilipua katika mechi ya wapinzani wa jadi kwa kijana aliechoka kabisa na kuichukia jamii?
 
Ungetumia kiswahili tu😂😂😂😂
Nimeona nilipokosea,nilikuwa naandika haraka haraka hiyo siku😃.Lakini ni vitu vidogo(minor) sema kwako lazima uone sababu umeshakuwa "CHIZI MAARIFA"....Its a great thing!Stay blessed
 
Unachonisihi nimelifuatilia kwa miaka ila nilichogundua ni kuwa kuna baadhi ya Waislam na Masheikh wenye kuitakidi hivyo pia wana wazungumzia Sufi pasipo kuwajua.

Hii inatokana na wao wenyewe kuwazungumzia kwenye baadhi ya vitabu vyao kisha wanajihitimishia kuwa Sufi wapo hivi: Kuwa Sufi ni grave worshippers (Waabudu Makaburi), Sufi ni washirikina n.k. Inafika pahala wana watuhumu na kuwatukana Sufi mpaka wanawatukana na Maimam ambao Sufi wanafuata mienenendo yao. Usimpe sikio pekee anayelalamikia kadhia fulani, mpe sikio na anayelalamikiwa kisha utajua uhakika wa mambo jinsi ulivyo.

Imam Ibn Hajar Al Asqalani kwenye Fat'h Al Baari 2nd volume na Sahihi chain kutoka kwa Imam Al Bayhaqi na Al Haakim na Ibn Khuzayma imepokewa kwamba: Bilal Ibn Al Haarith alikwenda kwenye kaburi la Mtume kipindi cha Aamu rramada Ukhalifa wa Umar na akisimama kwenye kaburi la Mtume akasema; " Yaa rasuulallah! Ardhi na mimea imenyauka, tafadhali tuombee kwa Mungu atunyeshelezee mvua kwa ummah wako"

Unaielewaje hii?

Imam Malik anasema: " Whoever studies tafaqaha and didn't study Sufism will be corrupted, and whoever studied Sufism and didn't study tafaqaha will became a heretic, and whoever combined both will be reach the truth. [The Scholar Ali Al Adawi volume.2 p 195]

Imam Ahmad Ibn Hambal: O My son, you have to sit with people of Sufism, because they are like a fountain of knowledge and they keep the remembrance of Allah in their hearts. They are the ascetics and have the most spiritual power [ Tanwir Al Quluub p. 405]

Imam Shafii kawazungumzia pia kwa wema mzuri watu wa Sufi na akasema amekaa kwao na amepata kujifunza dini kwao. ImamAbuu Hanifa kadhalika naye ni vivyo hivyo kuwa ni watu wema kwenye Ad Dur Al Mukhtar vol. 1 p. 43.

Unawazungumzia vipi hao Maimam kwa walichokisema ama kuwazungumzia Sufi?

Nimesoma Tawhiid ndugu, itikadi sahihi naijua. Kadri nilivyozidi kusoma ndivyo kadri nilivyozidi kujua na naandika kwa wema na siyo chuki. Wanaowapinga sufi wengi wao ni Salafi! Na salafi kielimu wamejifunga! Hawaamini wala hawamfuati Imam yoyote wa Sunnih wal Jamaa bali wanawafuata Maimam wenye Itikadi ya kwao. Ikiwa kama wakimfuata Imam wa Sunnih wal Jamaa basi wanachukua kipande kinachoendana na kile kinachokwenda sambamba na kile wanachokipigania wao. Ni watu waliyoivishwa itikadi ni watu wenye uchache wa elimu.

Kadri nilivyozid kutafuta ukweli nikakuta wana wa zuoni wakubwa wote wa Madhehebu ya Hambali walikuwa ni Sufi. Hambal Saudi Arabia wanajinasibu ni dhehebu lao lakini wanakataza Tasawwuf,Kutembelea makaburi n.k. Sikutanguliza itikadi. Nilitanguliza kuujua ukweli.

Ninasoma kwa Sheikh wa kisufi na nahudhuria hafla mbalimbali na hata siku moja sijawahi kushuhudia Sufi wakimuabudu mwengine zaidi ya Allah! Watu wanasema wanamuabudu Mtume sijawahi kuona hill! Watuwanasema wanawaabudu Mawalii sijawahi kuona hili! Watu wanasema wanaabudu makaburi sijawahi kuona hili! Na kuna mengine yanazungumzwa hata sijawahi kuyasikia zaidi ya kutoka kwa hao wanaowatuhumu.

Mimi ni Sunni, madhehebu ya Imam Shafii na nimeridhia kufuata twariqah ya Sheikh Abdul Qaadir Al Jaylaan.
Kaka nakuomba hapa https://www.jamiiforums.com/index.php?threads/1740065/
 
Shida huelewi na hujui tofauti ya Mungu na mungu. Allah ni Mungu, na vyengine vyote mkivifanya mungu basi mnafanya ushirikina. Yaani kama ni mtu wa kutumia akili, utajua kuwa Mungu hawezi kufananishwa na chochote, kwa sababu Sifa za Mungu sio sifa za kiumbe. Mwenye akili zake timamu hawezi kuamini kuwa mungu anazaliwa tena baada ya kumpa mimba mama yake.

Yesu amesema kuwa yeye ni mtu, nakushangaeni mnampa sifa ambayo hajakwambieni mumpe. Lakini hii yote ni kwa sababu badala ya kusoma maneno ya Mungu, mnasoma vitabu ambavyo waandishi wake hawajulikani bali wanadhaniwa tu. Na tena bado vikiwa vimebadilishwa.

Huwezi kutufananisha sie tunasoma Maneno ya Mungu na nyinyi mnaosoma maneno MNAYODHANIA yameandikwa na akina mattayo, joni n.k
Mnaabudu miungu huyo Allah sio Mungu ni mungu. Mungu hawezi kukuletea kitabu kinachohamasisha chuki na mauaji....
 
41 Reactions
Reply
Back
Top Bottom