Uwajibikaji kwenye eneo la kazi

CCM Music

JF-Expert Member
Dec 5, 2018
1,036
1,782
Kwa mtazamo wangu binafsi naona jamaa amefikiria vizuri sana.

Serikali yetu ya CCM hii tusilaze damu tuchukue fasta.

Na wapinzani nawaonya, Serikali ya CCM ikichukua huu ushauri hahahahahaha mtapoteana miaka 50 mbele huko. Nimemwelewa sana.

Document hii nimepata kwenye group moja la WhatsApp la ma jobless wa kitaa

Jisomee mwenyewe.

======

'ONE VOTE COUNTS TANZANIA' (IDARA KUU HUDUMA KWA WANANCHI TANZANIA):

A: MSINGI WA UANZISHWAJI WAKE:


Mama, ikumbukwe kuwa mtumishi yeyote awe wa sekta ya umma ama sekta binafsi asipomhudumia mwananchi vizuri lawama na adhabu siku ya kupiga kura hubebwa na Serikali iliyopo madarakani na sio huyo mtumishi aliyeshindwa kutoa huduma vizuri kwa wananchi. Wananchi wengi wa hali ya chini wanakwazika zaidi na namna wanavyohudumiwa na watumishi wasio waadilifu katika utumishi wao kiasi cha kushusha lawama zote kwa Serikali iliyopo madarakani na hatimaye chama tawala. Ikumbukwe pia ‘customer care’ kwa Watanzania walio wengi ni mtihani mkubwa mno.

Kutokana na ukiritimba kwenye ofisi nyingi hasa za umma mwananchi wa kawaida hawezi kirahisi sana kupeleka malalamiko yake kwenye ngazi za juu pale anapoona hajahudumiwa vizuri na watumishi. Hata akipeleka bado ni business as usual.

Hata hivyo, uhakika ni kwamba ubunifu huu wa kisasa wa kuanzishwa Idara hii utakuwa suluhisho kubwa la matatizo ya wananchi wanayokumbana nayo wakati wa kutafuta huduma kwenye taasisi za umma ama binafsi.

Kitendo cha kuanzisha Idara kama hii kitawafanya wananchi waamini kwamba sasa kuna uwajibikaji mkubwa sehemu za kazi hasa sehemu za umma na hata binafsi. Idara hii itakuwa kama Kituo Kikuu cha kupokea malalamiko ya wananchi pale ambapo wananchi wanaona hawahudumiwi vizuri na watumishi kama inavyopasa, iwe kwenye ofisi za umma ama ofisi binafsi. Ni muhimu kwa kila mwananchi akawa na namba za Idara pamoja na kufahamu akaunti zake za mitandaoni kwa ajili ya kuwasiliana na Idara popote pale anavyoona inapasa kuhusu kuhudumiwa kwake.

Maneno haya ‘One Vote Counts Tanzania’ ambayo ndio jina la Idara yanamaanisha kwa kila kura yaani kila mwananchi Tanzania hupaswa kuhudumiwa vizuri sana.

B: JINSI INAVYOFANYA KAZI:

Idara ikishapokea malalamiko ya mwananchi pale anapohudumiwa, bila kukawia Idara huwasiliana na Uongozi wa juu wa ofisi husika na kuwajulisha kuhusu malalamiko ya huduma kwa wananchi kwenye ofisi yake anayosimamia kama Kiongozi (Hii maana yake ni kuwa Idara hii inakuwa na mawasiliano ya moja kwa moja na kila kiongozi wa umma ama binafsi kwa maslahi mapana ya wananchi wote).

Idara ikishamaliza kuwasiliana na Uongozi wa juu wa ofisi husika pia hulazimika kuwasiliana tena na mwananchi aliyeleta malalamiko yake na kumpa mrejesho (feedback) kuhusu malalamiko yake. Idara pia humsihi mwananchi arejeshe mrejesho wake mara baada ya kuhudumiwa kwake, ili Idara ijiridhishe kuwa kweli mwananchi ameridhika na huduma aliyohudumiwa, na pia kuweka kumbukumbu kwa ajili ya ofisi.

Pale ufumbuzi wa malalamiko hayo utakapokosekana basi suala hilo Idara litalipeleka moja kwa moja bila kukawia kwenye meza ya viongozi wakuu wa Serikali kwa utaratibu utakaowekwa. Hii ni moja ya kazi nzito na kubwa sana yenye tija kubwa mno kwa serikali iliyopo madarakani pamoja na chama tawala kwa vizazi vijavyo.

Kwa ajili ya kumbukumbu za kiserikali kila malalamiko na hatua zilizochukuliwa huwekwa katika kumbukumbu nzuri kwa ajili ya marejeo pale panapohitajika.

C: ITAKAVYOKUWA KWA MCHORO BAADA YA KUANZISHWA IDARA HII:

Baada ya kuanzishwa Idara hii ya Huduma kwa Wananchi, mtiririko wa huduma kwa wananchi unapata sura mpya kidogo kutokana na ukweli kuwa sasa mwananchi wa kawaida kabisa anaweza kuhudumiwa vema na watumishi ama viongozi wakuu kwenye vitengo vya kazi kwa kuhofia nguvu aliyopewa mwananchi na Serikali ya kuwasiliana na mamlaka ya juu zaidi kwenye Taifa kama inavyoonekana kwenye mchoro hapo chini.

FUNGUO:

K – SERIKALI KUU (IKULU).

V – VIONGOZI WATEULE WANAOTEULIWA NA SERIKALI KUU.

T – WATUMISHI WANAOHUDUMIA WANANCHI MOJA KWA MOJA.

W – WANANCHI KWA UJUMLA.

D – IDARA YA HUDUMA KWA WANANCHI (ONE VOTE COUNTS TANZANIA).

----- - MAWASILIANO HAFIFU SANA

- MAWASILIANO YA KARIBU MNO

TAFSIRI YAKE:
Mwananchi wa kawaida atakuwa na nafasi ya kuwasilisha malalamiko yake yoyote yale kwa kiongozi wa ngazi yeyote hata kwa Rais kupitia kwa Idara ya Huduma kwa Wananchi (One Vote Counts Tanzania). Hii ni kwa sababu Idara hii ipo karibu zaidi na wananchi katika kuhudumiwa kwao na pia Idara hii ina link ya moja kwa moja na viongozi wakuu wa Serikali pamoja na viongozi wateule (Mawaziri, Makatibu na wakuu wa vitengo mbali mbali serikalini, wabunge, wenyeviti serikali za mitaa na wajumbe wa mitaa).


D: TASWIRA YAKE:
Hii ni sawa na kusema sasa serikali imeleta IKULU karibu zaidi na wananchi wake. Na wananchi sasa wana uwezo wa kuwasiliana na Ikulu muda wowote watakao kupitia Idara ya Huduma kwa Wananchi pale wanapoona hawahudumiwi vile inavyopasa na watumishi wa sekta ya umma ama sekta binafsi. Idara hii inakuwa kama wananchi wanaisaidia serikali yao kuwahudumia maana huripoti pale wasipohudumiwa vema.

Kwa maneno mengine: Idara ya Huduma kwa wananchi ndio Call Centre ya Taifa ya malalamiko ya wananchi, ndio kitengo cha Customer Care ya Taifa ya malalamiko ya 3/7 wananchi. Makampuni ya biashara yana vitengo vyao vya huduma kwa wateja wao. Ni vema nayo Serikali yetu kwa ulimwengu wa sasa ikawa na kitengo cha huduma kwa wananchi.

Kwa ulimwengu wa sasa Serikali ni kama kampuni kubwa inayofanya biashara ya siasa na wateja wake ni wapiga kura (wananchi) ambao ndio wanaolipa kodi (wanaowapa pesa) na ndio wanaowapa madaraka kwa njia ya kupiga kura. Hivyo, ni muhimu kuwepo na kitengo cha huduma kwa wananchi wake (wapiga kura). Kwa kufanya hivi ni dhahiri kuwa Serikali itakuwa inaenda sambamba kabisa na mabadiliko ya nyakati za sayansi na teknolojia ya siasa, maana siasa pia ni sayansi.

E: MANUFAA YA IDARA:
Rais (Msimamizi Mkuu wa Serikali) na Waziri Mkuu (Mtendaji Mkuu wa Serikali) kuwa karibu zaidi na wananchi wake kuliko nyakati zozote zile kupitia Idara hii.

Rais (Msimamizi Mkuu wa Serikali) na Waziri Mkuu (Mtendaji Mkuu wa Serikali) kuwa na uhakika zaidi kuhusu jinsi wananchi wanavyohudumiwa sehemu mbali mbali nchini kupitia Idara hii kwa sababu wananchi wenyewe wana uwezo wa kuwasilisha malalamiko yao moja kwa moja kwa Rais na Waziri Mkuu kupitia Idara hii.

Viongozi wateule (kimsingi wapo kwa ajili ya kusaidia Serikali kuwatumikia wananchi) nao watapata uhakika wa wananchi kuhudumiwa vizuri kwenye ofisi zao kwa kuwa wananchi wana uwezo wa kuwasilisha malalamiko yao moja kwa moja kwa viongozi hao kupitia Idara hii. Kiongozi anayelalamikiwa sana anakwenda na maji.

Watumishi kuwajibika zaidi katika kuwatumikia wananchi kwa kuwa wanafahamu wananchi wana uwezo wa kuwasiliana moja kwa moja na viongozi wao wakuu kwenye maeneo yao ya kazi pamoja na viongozi wakuu wa Serikali (Rais na Waziri Mkuu) kupitia Idara hii. Idara hii ni kama 'government watchdog' kwa huduma wanazopewa watanzania iwe kwenye sekta za umma ama sekta binafsi.

Kuongezeka kwa imani ya kuendelea kuhudumiwa na Serikali iliyopo madarakani kwa kuwa, sasa wananchi wenyewe wanaona wapo karibu zaidi na viongozi wao wakuu wa Serikali pamoja na viongozi wateule kupitia Idara ya Huduma kwa Wananchi. Hii ina 4/7 manufaa makubwa zaidi kwa Chama cha Mapinduzi (Rais, Wabunge wake, Madiwani wake na Wenyeviti wake wa serikali za mitaa).

Kupungua kwa vitendo vya rushwa kama sio kutoweka kabisa kwa wale watumishi wasio waadilifu katika kuwahudumia wananchi wa hali ya chini zaidi kwenye Taifa letu. Ni wazi kuwa wananchi wa hali ya chini watakombolewa sana kutoka kwenye mikono ya rushwa na ujio wa Idara hii.

Kupunguza ama kuondoa kabisa mtindo wa baadhi ya watumishi kuhudumia wananchi kwa kufahamiana, hivyo wananchi wa hali ya chini kunufaika zaidi kwa kuwa ndio wahanga zaidi wa mtindo huu wa kuhudumiwa kwa kufahamiana.

Idara hii itakuwa na msaada mkubwa sana kwa Idara ya Usalama wa Taifa katika masuala mbali mbali yanayohusu huduma kwa wananchi kwenye maeneo mbali mbali nchini.

Idara hii pia itakuwa na msaada mkubwa sana kwa taasisi ya kupambana na kuzuia rushwa nchini (TAKUKURU) katika masuala mbali mbali yahusuyo rushwa.

Idara hii husaidia kujenga uzalendo wa wananchi kwa Taifa lao, mfano kupenda kulipa kodi na kufuata sheria za nchi bila shuruti.

Idara hii iwe sehemu kuu ya kupokelea mapendekezo ama ushauri mbali mbali toka kwa wananchi kuhusu Taifa letu (Ingawa hakatazwi mtu kupeleka anakotaka)

F: MAOMBI NA MAPENDEKEZO KUHUSU IDARA:
Hili ni jambo jema katika kuisaidia Serikali kuendelea kuaminiwa na wananchi wake, hivyo, ninaomba Idara hii ikikupendeza Mheshimiwa Rais iundwe rasmi na iwe chini ya Ikulu. Kuwa chini ya Ikulu ni kuwaonyesha wananchi kuwa sasa wana uwezo wa kuwasiliana moja kwa moja na kiongozi wao mkuu waliyemchagua. Rais huwa ndio mhangaikaji wa kutafuta kura kwa wananchi.

Ikulu ni Ofisi ya juu katika Taifa, hivyo ni kuwaonyesha wananchi kuwa sasa wana uwezo wa kuwasiliana moja kwa moja na Ofisi ya juu zaidi katika nchi yao jambo ambalo ni kubwa sana katika siasa za Tanzania.

5/7

Lakini pia kuwa chini ya Ikulu inakuwa kama Serikali imetuma ujumbe wa moja kwa moja kwa watumishi wote wa umma na binafsi kuwa sasa jicho la Ikulu lipo mbele yao muda wote wa kuwahudumia wananchi. Jambo hili litajenga imani kubwa sana kisiasa kwa wananchi hasa nyakati hizi za uchaguzi wa siasa za ushindani.

G: HITIMISHO:
Nina imani kubwa sana kuwa wazo hili litapata kibali kutoka kwako na bila shaka Idara hii itakuwa ni moja ya ‘legacy’ yako kubwa sana katika utumishi wako kwa Taifa letu la Tanzania kwa kuwa utakuwa umewaheshimisha sana watanzania wa hali ya chini zaidi kwa kuwaweka karibu na Uongozi wa juu kwenye Taifa lao kupitia Idara hii, jambo ambalo halijawahi kutokea tangu uhuru wa Taifa letu.

Uanzishwaji wake hauna gharama sana. Panahitajika ofisi, fanicha kidogo, komputa chache, simu za mikononi na wafanyakazi wachache kwa kuanzia.

Kiasi kidogo cha ‘fedha za Jimbo’ zielekezwe kwenye uendeshaji wa Idara hii. Hii ni kwa sababu Idara hii inawabeba kwa kiasi kikubwa sana viongozi wa kisiasa kwa ngazi zote kuanzia mitaa hadi ngazi ya Urais.


Kama ambavyo mara kwa mara vyombo vya ulinzi na usalama vya Taifa vinaku brief kuhusu ulinzi na usalama kwenye maeneo mbali mbali nchini, hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa Idara hii kwamba itakuwa kwa kila siku ama mara kwa mara inaku brief kuhusu malalamiko ya wananchi sehemu mbali mbali nchini.

Mwisho kabisa, watanzania wengi wana imani na Mama na Mama ni mlezi. Mama yetu anapenda wanaye hasa wale wa hali ya chini. Na ndio maana imani yao ni hii kuhusu Mama yetu. Mama Samia ataleta suluhu ya matatizo yetu mbali mbali nchini.

Hii mtaani kwetu tunasema ‘Ikulu ipo popote ulipo mwananchi vimba’

# Suluhu is the legacy of Samia.

# New Tanzania – Tanzania Mpya ya Samia.

Wasalaam,

ONE VOTE COUNTS TANZANIA (IDARA KUU HUDUMA KWA WANANCHI–TANZANIA).
 

Attachments

  • UWAJIBIKAJI SEHEMU ZA KAZI - UMMA NA BINAFSI.pdf
    329.1 KB · Views: 6
Soon, naweka nyingine kuhusu Migogoro ya ardhi pamoja na Usafi jiji la DSM.

Huyu jamaa ajengewe hata sanamu pale Ikulu
 
Kama document imeletwa na mwana CCM basi hiyo ni takataka tupu, CCM ipo tangu uhuru lakini bado tunaishi kwenye nyumba za tembe. Shame on you
Mm ndo mwana CCM na huniambii kitu aliyeandika sijui ni nani.

Kwani wapinzani mna hoja gani hasa tuwape nchi? Au mnataka tuwape nchi kwenye ki sahani. Wekeni hoja nzito mezani acheni kudemka
 
Maxence Melo huu uzi moderator hakuweka namba za jamaa mwishoni wala zile handle zake za mitandaoni.
Waambie mode wamtendea haki wanakikuka miiko na maadili na Imani ya JF.
Wamuwekee namba zake, amejitahidi kuwa very constructive, na hili huwapa JF mileage.

Hata heading haijakidhi standards za JF tunazozijua Sisi. Yule mode wa uzi wa Usafi DSM Yule so professional na anaijua JF.

Halafu kaweka kwenye jukwaa la matangazo madogo madogo dah hii kweli inapaswa kuwa hapa uzi unaomhusu Mh Rais? Aiseee huyu mode kachoka dadadeki Maxence Melo do the needful pls!

Naomba kuwasilisha Kwa Mkurugenzi Mtendaji Mh. Maxence Melo
 
Back
Top Bottom