SoC02 Uvutaji wa sigara janga la Taifa

Stories of Change - 2022 Competition

Linus jeremiah

Senior Member
May 13, 2018
142
137
Ilikua sku ya asubuhi sauti ya Babu mwenye umri wa kukadilia Kama miaka 68 aliyekuwa amelala kwenye kitanda wodini na kuwaambia ndugu zake "Mpira nliowekewa pembeni ya kifua changu na unapitisha damu kutoka kwenye mapafu yangu na madaktari wamenieleza mapafu yangu yamejaa damu na nina kansa ya damu " .Baada ya kuchukua mda kidogo kuongea na yule Babu alieza ujana wake wote alikuwa na uwezo wa kuvuta pakiti moja ya sigara.


UVUTAJI WA SIGARA
Kwa kipindi cha karibuni dar es salaam na mikoa karibia yote ya Tanzania swala la uvutaji sigara lmekua too much .Alaf mbaya wavutaji hata aibu hawana unaweza kuta yupo kwenye mikusanyiko ya watu anavuta sigara tu bila hata kujari.Na wakati mwingine wanao mzunguka nao wana enjoy tu mtu anavyo vuta hio sigara bila kumwambia avutie pembeni.

Na kwa kiwango kikubwa vijana wadogo chini ya miaka 18 nao wamekua wahanga maana ndo kundi ambapo wanaongoza kuvuta sigara.Ndani ya sigara Kuna kemikali inayoitwa nikotini ambayo ndo hufanya mtu asisimuke baada ya kuvuta sigara.

Kitaalam wanasema unavovuta sigara mara kwa mara ndo chanzo kikubwa cha wewe kuhathirika zaidi.Na mara nyingi shida ztokanazo na uvutaji wa sigara uwezi kuziona ukiwa na umri mdogo mara nyingi zinatokea katika umri mkubwa.

Jambo lingine ambalo watu halijui ni kua hata yule ambae havuti lkn yupo jirani na mtu anaevuta sigara mfano mke na mme nae yupo katika hatari ya kupata shida Kama yule anaevuta.

MADHARA YA KIAFYA YATOKANAYO NA UVUTAJI WA SIGARA.

Uvutaji wa sigara unaharibu kila kiungo ndani ya mwili wa mwanadamu Kama vile mfumo wa upumuaji ,moyo na sehemu nyingine.Yafuatayo ni madhara ya sigara kutoka kiungo kimoja moja ndani ya mwili

1.Kansa ya mapafu
Ndani ya sigara Kuna kemikali inayoitwa nikotini.Kemikali hii ndo chanzo kikubwa cha kansa ya mapafu.Kutokana na utafiti katika vifo 9 Kati ya 10 vya kansa ya mapafu kisababishi kikuu ni uvutaji wa sigara.

Naona ni wakat sahihi wa serikali kuanzia vituo maalum pembezoni mwa ma barabara,kwenye mikusanyiko ya watu mfano sokoni ili wavutaji wanapovuta sigara moshi usiwaathir ambao hawavuti sigara.

2.Magonjwa ya moyo
Uvutaji wa sigara hupelekea uharibifu ndani ya mirija ya damu ,moyo na seli za damu .Kemikali iliyo ndani ya sigara hupelekea mishipa ya damu kusinyaa na wakati mwingine kupasuka kwa mirija ya damu ambayo huzuia damu kufika kwenye moyo au sehemu nyingine ya mwili hivyo kupungua kwa kiasi cha oksijen sehemu mbalimbali za mwili .Hii inaweza pelekea vitu Kama maumivu ya kifua ,Ikitokea damu kiasi kidogo imefka au haijafika kbsa kwenye ubongo hii uweza pelekea kiharusi (stroke) hivyo inaweza pelekea kifo.

3.Uharibifu ndani ya mfumo wa uzazi
Kemikali iliyo ndani ya sigara ndo chanzo kikubwa cha mabadiliko ya hormone kwa wanawake hivyo hupelekea mwanamke kutokuwa na uwezo wa kushika mimba.Na Kama mwanamke akishika mimba huweza kupelekea mimba kutungwa sehemu ambayo si sahihi,kujigungua kabla ya mda,kuzaa mtoto mwenye mzito mdogo na inaweza kuwa chanzo Cha vitu Kama mdomo sungura .

Kwa wanaume hupelekea uume kushindwa kusimama na hupunguza ubora wa mbegu za kiume hivyo mwanaume kushindwa kutungisha mimba.

4.Kisukari aina ya pili.
Tafiti znasema anaevuta sigara anauwezekano mkubwa wa kupata kisukari ukilinganisha na yule ambae havuti.Pia mtu mwenye kisukari akiwa anavuta sigara inakuwa ni ngumu sama kwa uyo mtu ku control sukari yake na pia ni chanzo kikuu cha magonjwa ya Figo na moyo kwa mtu ambaye tayari ana kisukari

5.Kinywa kichafu
Mtu anaevuta sigara Kwanza mara nyingi wanakua wanatoa harufu mbaya mdomo ,watu hawa pia huvimba fizi na wakati mwingine kutoa damu wakati wanapiga mswaki ,pia hili swala ni chanzo Cha meno kulegea na wakati mwingine kutoka menyewe na wakati mwingine watu wanaovuta sigara huwa wanakuwa na uchafu kwenye meno yao ambao hautoki kwa kupiga na mswaki.Na wakati mwingine watu hawa wanakua na midomo mikavu maana kiasi cha mate kinapungua kuzalishwa.

6.Kansa ya kinywa ,Koo na wakati mwingine tumbo.

FAIDA ZA KUACHA UVUTAJI WA SIGARA

Unapoacha uvutaji wa sigara maana yake viungo vyote vya mwili vinarudi katika hali ya kawaida .Mfano mapigo ya moyo,mfumo wa uzazi kujifungua mtoto mwenye uzito kamili na katika sku kamili ,uwezo wa kusimamisha na kuongezeka kwa ubora wa mbegu za kiume na mtu kuwa na afya nzuri ya kinywa na mwili.

NINI KIFANYWE NA SERIKALI

Japokuwa sigara ina madhara yote hayo lkn ndo zao linalopewa kipaumbele zaidi ndani ya Tanzania.Ni ngumu Sana kwa serikali kupiga marufuku ulimwaji wa hili zao la kibiashara .Lkn inaweza punguza uzalishaji wake kwa kufanya uwekezaji zaidi kwenye mazao ya chakula ambayo yana uhitaji ukubwa ukilinganisha na mazao ya biashara.

Lakini serikali inabid iweke sheria ambazo zitafanya vijana wa chini ya miaka 18 kuacha kbsa kutumia sigara .

Pia ndani ya jamii matumizi horera ya sigara kila mahali nayo yapunguzwe .Serikali ifanye mpango wa kuweka vituo maalum hasa pembeni ya barabara ambavyo vitakua kwa ajili ya wavuta sigara.Na yoyote atakefuta sigara Tofauti na hayo maeneo apigwe faini .Hii itasaidia watu ambao hawavuti sigara kuepukana na uvutaji wa hewa yenye sigara.
 
Namaanisha kansa ya mapafu sio damu na alikuwa na uwezo wa kutumia pakiti moja la sigara kwa siku moja
 
Kwa nini sigara zinazalishwa na tena zinauzwa kwa wingi bei poa?

Ni bora viwanda vikafungwa ili kuzuia madhara hayo.

Kinyume chake ni kelele za chura tu, wavutaji wataongezeka sana tu.
Inakuwa ngumu hasa kwa Serikali yetu kuzuia hili maana ni moja Kati ya bidhaa zinazoliiingizia kwa wingi pesa Serikali.

Hapa Cha msingi ni mtu mwenyewe kupambana na hili swala lkn tusitegemee nguvu toka juu

Kama hujawai vuta usijaribu kuvuta na Kama unavuta jaribu kutengeneza mazingira ya kupunguza au kuacha kbsa kutumia.
 
Huu uraibu sio mchezo, mtu anaamka asubuhi ana jero tu mfukon ila ni heri kwake akakate kiu ya sigara kwanza kuliko kununua mihogo afungue kinywa. Mwengine hawez kwenda haja kubwa bila sigara dah! Nashkuru niliacha
kwamba adi kwenda haja, Kaka ww uliwezaje kuacha ? Nazan ww unaweza kuwa mwalimu wa vijana na wazee wanaotumia kuacha kbsa hiki kitu
 
Huu uraibu sio mchezo, mtu anaamka asubuhi ana jero tu mfukon ila ni heri kwake akakate kiu ya sigara kwanza kuliko kununua mihogo afungue kinywa. Mwengine hawez kwenda haja kubwa bila sigara dah! Nashkuru niliacha
hahaha kwamba sigara inalainisha choo au mimi sijaelewa. naonaga wengine hiyo kiu ikiwashika wanasema wanajisikia kama tumbo la kuhara hebu tuelezee mkuu
 
hahaha kwamba sigara inalainisha choo au mimi sijaelewa. naonaga wengine hiyo kiu ikiwashika wanasema wanajisikia kama tumbo la kuhara hebu tuelezee mkuu
Kwahiyo nimekua case study sio?? 😁 ni hatari kuna mzee kitaa alipata cancer ya koo alikua ana hali mbaya pamoja na vitisho vyote vya ma doctor hakuacha kuvuta mpaka anakufa.
 
Kwahiyo nimekua case study sio?? 😁 ni hatari kuna mzee kitaa alipata cancer ya koo alikua ana hali mbaya pamoja na vitisho vyote vya ma doctor hakuacha kuvuta mpaka anakufa.
babu yangu alivuta hadi 2014 akiwa na miaka 108 tena alikuwa akipiga nyota zile na tumbaku ya kutosha. Madhara yake nafikiri yanatofautiana kabisa maana kuna wazee kabisa wana 90+ na wanapiga fresh tu wala hawaumwi chochote
 
hahaha kwamba sigara inalainisha choo au mimi sijaelewa. naonaga wengine hiyo kiu ikiwashika wanasema wanajisikia kama tumbo la kuhara hebu tuelezee mkuu
Hahaha Kuna jamaa mmoja yy alikuwa anasema bila sigara yy si chochote na bila hii kitu hawezi fanya Jambo lolote mwili unawasha Koo nalo ndo usiseme
 
Kwahiyo nimekua case study sio?? ni hatari kuna mzee kitaa alipata cancer ya koo alikua ana hali mbaya pamoja na vitisho vyote vya ma doctor hakuacha kuvuta mpaka anakufa.
Hahaha mzee alikuwa ameshakua mraibu kweli kweli na huenda alikuwa ndani ya game la kuvuta sigara kwa zaidi ya miaka 20
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom