Uvivu wa serikali kukusanya kodi ndo unaleta tozo.

BestOfMyKind

JF-Expert Member
Apr 26, 2012
1,335
1,386
Serikali imewaonea huruma wafanyakazi wanaolipwa kima cha chini lakini bado wanakatwa PAYE.
Ikaona si sawa mtu alipwe laki 3 yenye kodi wakati kuna bodaboda wana ingiza mpaka laki 6 kwa mwezi na hawalipi kodi ya kipato.
Sasa namna ya kuchukua kodi kwa watu ambao wana kipato na hawalipi kodi ndo ikawavuruga kina mwigulu. Wakaona njia sahihi ni kuchukua hata sehemu ya hela za rambirambi, michango ya maafa, sehemu ya hela za urithi wa watu n.k
Wakati hapo kwa msururu wa viongozi tulionao ( wa kuteuliwa na kuchaguliwa) tungeweza kujua kabisa nani ana taxable income na tukampa makadirio kwa mwaka alipe kiasi gani.
Sasa uvivu wa hawa jamaa imefanya hata bibi yangu wa Namabengo kule Songea nikimpa zawadi ya pesa ya sukari nayo ikatwe tozo wakati si kipato chake kile.
Hawa mabalozi, wenyeviti wa mitaa, watendaji, wakuu wa wilaya, wakuu wa mikoa kazi zao hasa ni nini?
Hawa ni rahisi kujua wananchi na shughuli zao ili anapokuja afisa wa kodi ajue kufanya makadirio ya kodi kwa kila mwenye kipato.
Inauma sana kumtumia mtu hela ya zawadi au shukrani ya kukulea na hela ile ikageuzwa kuwa sehemu ya kipato chake. Hata hakufanya vile ili nije nimlipe, namimi sijampa ile kama kipato bali zawadi.
Sijui kwanini sisi tuna asili ya uvivu? Yani tuna mnyororo mzuri wa uongozi ambao ungeweza kusaidia kupata mapato ya kutosha lakini tumechagua njia rahisi yenye maumivu makubwa mno.
Aliyepaa sio wa ardhini, mwigulu haijalishi ulipata shida kiasi gani wakati unakua wewe huwez kusemea watu wa hali duni wa mwaka 2022.
Nimegoogle aina ya mapato ambayo hayakatwi kodi marekani
Nontaxable income won't be taxed, whether or not you enter it on your tax return. The following items are deemed nontaxable by the : Inheritances, gifts and bequests. Cash rebates on items you purchase from a retailer, manufacturer or dealer.
 
Back
Top Bottom