Rare Sapphire

JF-Expert Member
Jul 24, 2021
576
1,626
Habari Wakuu,

Naamini wengi sio wageni na akaunti za watoto kwenye mitandao ya kijamii kama vile Instagram, Facebook, TikTok na kadhalika.

intaneti.jpg

Akaunti hizi zinazofunguliwa na wazazi/walezi zimekuwa zikisimamiwa na wazazi wenyewe mara nyingi, na mara chache mtoto anaachiwa kuendesha account hiyo mwenyewe.

Wazazi/Walezi wengine huenda mbali zaidi na kufanya kama vile mtoto huyo anafanya mazungumzo kwenye akaunti hizo, yaani anaweka kitu pamoja na jibu kanakwamba mtoto wake wa miaka 2 au mitatu kajibu.

Akaunti hizi huwa na taarifa nyingi kumuhusu mtoto huyo kama vitu anavupenda kufanya, anavyopenda kula, picha mtoto akiwa ameweka pause tofauti tofauti, video ya matukio mbalimbali kama siku ya kuzaliwa ama mtoto akiwa anacheza, sehemu anayoishi ikiwemo na mazingira ya chumbani nk, shule anayosoma (kama ameanza shule) na mambo mengine kadha wa kadha.

Naleta kwenu mjadala huu tupate cha kujifunza kadri tutakavyoendelea, ni sababu gani zinazowafanya wazazi/walezi wafungue akaunti za kijamii kwa ajili ya watoto wao?

intaneti1.jpg
 
Sioni haja ya kujadili ishu inayofanywa na chini ya 1% ya watu wote...Mara nyingi ni wasanii na Kama unavyojua wasanii target yao ni kufuatiliwa Mara kwa mara...mchakarikaji wa maisha daily hawezi hata kufikiria kumfungulia mtoto account ya social network
 
Sioni haja ya kujadili ishu inayofanywa na chini ya 1% ya watu wote...Mara nyingi ni wasanii na Kama unavyojua wasanii target yao ni kufuatiliwa Mara kwa mara...mchakarikaji wa maisha daily hawezi hata kufikiria kumfungulia mtoto account ya social network
Wasanii wanaweza kuwa wanaongoza lakini watu wa kawaida hawapo nyuma. Ni trend inayokuwa kwa kasi
 
Mimi nimemfungulia Instagram kutunza picha zake nazoona zina umuhimu, akaunti naona mimi na mamake tu.
 
Ushamba tu wa wazazi.

Mtoto naye ana haki, moja wapo ni ya faragha.

Ipo siku watu wataanza buruzwa mahakamani kwa kutumia picha za watu
 
Back
Top Bottom