Wasanii kuchukua hatua ya kujiondoa kwenye mitandao ya kijamii sio suluhisho la unyanyasaji mitandaoni

Wild Flower

Member
Jul 20, 2023
80
96
Katika miaka ya hivi karibuni, unyanyasaji wa mtandaoni umekuwa tatizo kubwa katika majukwaa ya mitandao ya kijamii kama vile TikTok, Instagram, Twitter na Facebook. Unyanyasaji huu hujitokeza kupitia mashambulio ya kauli za chuki, utani uliopitiliza, comments za kudhalilisha na matusi. Vitendo kama hivi vinaweza kusababisha matatizo ya afya ya akili na hata baadhi ya watu kujiua au kujidhuru mwili.

Tatizo hili linajitokeza sana kwa watu maarufu kama wasanii na baadhi yao wameamua kuchukua hatua kwa kujitoa kwenye mitandao hiyo kwa muda au kufuta kabisa akaunti zao. Mfano mzuri ni hivi karibuni tareh 9 Machi ambapo rapa maarufu kutoka Marekani Amala Ratna Zandile Dlamini, maarufu kama “Doja Cat” alifuta akaunti yake ya Instagram yenye wafuasi zaidi ya million 24 kwa ajili ya kuboresha afya yake ya akili.

Kupitia akaunti yake ya Instagram aliandika ujumbe huu "Habari zenu, nafuta akaunti yangu ya Instagram kwa sababu sioni umuhimu wa kuitumia tena. Huwa napenda kutembelea mtandao huu kwa ajili ya kutafuta hamasa lakini nimechoka na nashindwa kuvumilia jinsi ninavyozungumziwa na kuchukuliwa katika mtandao huu kwani najiskia vibaya na kupata Mawazo mabaya. Tafadhali kuweni makini na jinsi mnavyowazungumzia watu mitandaoni.”

Uamuzi huu alichochewa na mashabiki zake kuanza kusema vibaya mitandaoni kuhusu tetesi za mahusiano yake kuvunjika na mchekeshaji wa mtandaoni J. Cyrus.

Wanamuziki kujiondoa kwenye mitandao ya kijamii imekuwa jambo la kawaida miaka ya karibuni. Jambo hili tumeshudia kwa watu maarufu nchi nyingine kama vile Selena Gomez, Justin Bieber, Tom Holland, Megan Thee Stallion and wengine wengi.

Uamuzi wa watu maarufu kujiondoa kwenye Instagram unapaswa kuwa wito wa hatua kali dhidi ya unyanyasaji wa mtandaoni. Inatukumbusha umuhimu wa kujenga utamaduni wa mtandaoni unaounga mkono na kuhimiza upendo, heshima, na uelewa. Ni wakati kila mmoja wetu kuchukua jukumu katika kujenga jamii mtandaoni inayojali na kuondoa kabisa vitendo vya unyanyasaji.
 
Wajiondoe tu,umaarufu wao unatokana na kufatiliwa pia
Wasipofatiliwa hawana lolote

Ova
 
Back
Top Bottom