Just Distinctions
JF-Expert Member
- May 5, 2016
- 3,322
- 6,990
Friji huwa haizimwi, na binafsi yangu toka nilipoliwasha mara ya kwanza sijawahi kulizimaHabari!!!! Naomba kujua mnatunza vipi vyakula kwenye friji ili visiharibike? Mfano; samaki,nyama,nyanya,karoti,matunda,na mboga mboga? Je? Mnawasha friji kila siku bila kulipumzisha,au mnawasha kwa mda tu na kuzima?
Huwa linazimika lenyewe pale umeme ukikatika na umeme ukirudi ngoma isambe na nimeweka fridge guard kwa hiyo hofu ya kuungua sina
Kuhusu vyakula, nyama naweka kwenye mifuko ya nylon kisha nagandisha pia sausages n.k
Vingine kama maziwa fresh na mtindi naweka kwenye friji hivi kwa ubaridi tu zinadumu
Kuna baadhi ya misosi au matunda hayapaswi kuwekwa kwenye friji hivyo siyanunui kwa wingi kama tikiti, mkate n.k