Utunzaji wa vyakula kwenye friji

Utunzaji wa vyakula kwenye friji

unapo chemsha unaichemsha yenye pekee au kuna vitu vingne unatia? Ebu tupe somo kidogo hapo tujaribu
Mie huwa nachemsha ya muda mrefu siweki kitu.

Ila unaweza weka na kitunguu na kitunguu saumu (sina uhakika ukiweka kitunguu kama itaendelea kukaa kwa muda mrefu sana kama vile mwezi+)

Ila waweza weka na viungo upendavyo
 
Thermostat ipo pale kwa kazi hio badala ya wewe kuzima na kuwasha baridi uliyoweka ikifika yenyewe inajizima..., ila kuhusu untunzaji kama vitu vinavyohitaji baridi zaidi viweke kwa juu au mwanzoni kwenye baridi kubwa na vingine chini au mwishoni....

Unachoongelea wewe kilikuwa fridge za zamani au kwa sasa coolers unaweka barafu na kitu chako unachohitaji kitunzwe (zamani fridge ilikuwa kabati na watu walikuwa wanapita nyumba kwa nyumba kuzambaza barafu) Barafu zilikuwa zinavunwa huko Antarctica n.k. na kusambazwa sehemu nyingine duniani (kwa meli na trains) hio ni kabla ya kupata teknolojia ya ku-manufacture ice...

Huku Africa kwa maji fridge ilikuwa ni Mtungi au kwa mboga kuzizika ardhini au kukausha....

Sorry kama nipo out of topic..... lakini hii ni Historia nzuri sana (The Quest for Absolute Zero)
 
Habari!!!! Naomba kujua mnatunza vipi vyakula kwenye friji? Mfano; samaki,nyama,nyanya,karoti,matunda,na mboga mboga? Je? Mnawasha friji kila siku bila kulipumzisha,au mnawasha kwa mda hadi nyama zigande na lile baridi ndipo mnazima au mnafanyaje?
Kimsingi kama una friji hizi za kisasa hupaswi kuizima, yenyewe inajizima na kujiwasha kulingana na ubaridi uliouset..
 
Evelyn Salt asante sana kwa somo lako la kublend nyanya.... Ningekuwa na namba yako ningekuunga kifurushi cha mwezi😘

Kama una mbinu zingine za kurahisisha maisha ya "jikoni" tusaidie ili sisi bachelors tupate njia za kurahisha maisha ..
Namba nakupa, 🤣🤣🤣🤣 nasubiria msg pendwa.

Nikupe mbinu ya chapati?
 
KUTUNZA NYAMA Ya NG'OMBE
Osha na katakata nyama yako vipande upendavyo

Chukua kitunguu maji kimoja kisage weka kwenye hiyo nyama
Chukua tangawiz kias kidogo na kitunguu swaumu saga pamoja weka kwenye nyama yako changanya
Chukua bakuli ndogo zenye mfuniko,mfuko unaofunga vizuri tenganisha nyama zako kias unachopenda kutumia Kwa siku
Weka kwnye friji hazipotezi ladha
 
KWANZA USAFI
hifadhi vitu vyako vikiwa safi na jokofu liwe safi pia,kwenye mbogamboga hifadhi zikiwa safi na kavu yani umezifuta maji baada ya kuosha

PILI
kwenye nyama osha nyama kuondoa damu na katakata kwe kiwango cha matumizi ya siku kisha tenga kwenye mifuko au kontena na hifadhi kwenye jokofu epuka kuchanganya nyama nyekundu na nyeupe pamoja

washa jokofu 24hrs au masaa 14 kwa siku
Ongeza asichanganye cooked foods na raw foods pia kuepuka cross contamination
 
KUTUNZA HOHO ZIKAE HATA WIKI MBILI
Chukua hoho zioshe
Kisha zifute hakikisha hazina maji maji weka kwenye mfuko funga vizuri weka kwenye friji

Njia ya pili
Osha hoho zifute maji maji
Kata katikati toa zile mbegu Kisha weka kwenye mfuko zihifadhi
 
KWANZA USAFI
hifadhi vitu vyako vikiwa safi na jokofu liwe safi pia,kwenye mbogamboga hifadhi zikiwa safi na kavu yani umezifuta maji baada ya kuosha

PILI
kwenye nyama osha nyama kuondoa damu na katakata kwe kiwango cha matumizi ya siku kisha tenga kwenye mifuko au kontena na hifadhi kwenye jokofu epuka kuchanganya nyama nyekundu na nyeupe pamoja

washa jokofu 24hrs au masaa 14 kwa siku
Nyama iliyotoka kwa mnyama aliyechinjwa kisawasawa na katika mazingira safi, haitakiwi kuoshwa.
 
Back
Top Bottom