Utu na utoaji!

Juzi kuna kapindi kilinisikitisha kweli!Kuna baba ambae ana tatizo la figo..zimefail kabisa kwahiyo anategemea mashine kuishi!Huyo mzee ana dada na kaka zaidi ya watatu na hamna hata mmoja aliyetaka hata kupima kuona kama wanamatch na ndugu yao achilia mbali kujitolea figo imsaidie!
Ikabidi nijiulize wangapi kati ya ndugu na rafiki zangu wakikutwa na tatizo kama hilo ntakua tayari kujitolea figo yangu moja kusaidia.Wachache ningewapa kwa moyo mkunjufu na wengine ningewapa tu ilimradi!Wewe je?
Kuna jamaa yangu figo zake ziliacha kufanya kazi mtoto wake wa kipekee alijitolea kumpa moja lakini bibi mzaa baba akakataa mjukuu wake atoe kwa kudai mwanae ameshaishi vya kutosha afe tu sio kumuumizia mjukuu wake wa pekee,na kweli baada ya muda akafariki dunia.Sasa huzuni ilikuja baada ya mjukuu nae kuuawa na majambazi baada ya miaka 2 kwa hiyo bibi akakosa wote.
 
lIZZY, KUTOA FIGO NI RAHISI KAMA UKO NCHI ILIYOENDELEA, LAKINI KUTOA FIGO TANZANIA YAWEZA IKAWA NDIO MWISHO WA MAISHA YAKO
Hahahaha MTM mbona unatuogopesha sasa?Nimeanza kupata mawazo ya pili!!

MBU pole sana kuhusu mzee!Binafsi nashindwa kuelewa hili la damu watu wanaogopa nini haswa??Hata kitu ambacho hakituishii tunanyima?Kweli hii ni hatari..yani uchoyo mpaka umepitiliza!
 
Kuna jamaa yangu figo zake ziliacha kufanya kazi mtoto wake wa kipekee alijitolea kumpa moja lakini bibi mzaa baba akakataa mjukuu wake atoe kwa kudai mwanae ameshaishi vya kutosha afe tu sio kumuumizia mjukuu wake wa pekee,na kweli baada ya muda akafariki dunia.Sasa huzuni ilikuja baada ya mjukuu nae kuuawa na majambazi baada ya miaka 2 kwa hiyo bibi akakosa wote.
Loh!Bibi aliamua mmoja aishi akakosa wote wakati kuna uwezekano baba angeishi mwana nae angesalia
 
Back
Top Bottom