Ile wikiendi ya sikukuu ya Nane Nane niliendesha gari kutoka Dar hadi Morogoro na kugeuza baada ya siku kadhaa, na Jumamosi ya juzi pia niliendesha kutoka Dar hadi Chalinze, nilichokiona barabarani nyakati zote, wakati wa kwenda na hata wakati wa kurudi, kilinishtua na kunishangaza sana, idadi kubwa ya malori ambayo sijawahi kuiona kabla.
Ni utitiri wa malori usio wa kawaida, sikuweza kuamini macho yangu kwamba unaweza kupishana na malori hadi 100 yakiwa kwenye msafara.
Ikitokea tatizo dogo katikati ya barabara basi wenye magari mengine ya kawaida watataabika kwa kukaa kwenye foleni isiyo na maelezo. Sina hakika nini kimesababisha hali hii, mwenye kujua atujuze, lakini ni wazi kwamba:
a) Wingi wa malori hayo utaathiri ubora wa barabara
b) Kuna mazingira hatarishi ya ajali na uhalifu kujitokeza barabarani
c) Usafiri kwenye barabara hiyo utasababisha ucheleweshaji na kero kubwa kwa wananchi
Tusingoje hadi balaa litokee ndipo tuchukue hatua, ni muhimu hatua za tahadhari zinahitaji kuchukuliwa SASA.