Utiaji saini wa Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Sengerema - Nyehunge km 53.4 na Kivuko cha Buyagu-Mbalika. Aprili 23, 2023

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,309
5,464
Utiaji saini wa Mradi wa Ujenzi wa Barabara ya Sengerema - Nyehunge km 53.4 kwa kiwango cha lami, Aprili 23, 2023.


47fcba5a-18e9-4952-b4bb-2caf51e42c68.jpg


Godfrey Kasekenya, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi
Anasema: “Utashi na maoni ya Rais Dkt. Samia ni kuwa ili Tanzania iendelee moja ya kitu muhimu ni kujenga na kuboresha miundombinu.

"Wananchi waliokuwa wakipata adha kwa miaka nenda rudi leo wanapata kivuko na vile vibobu vinakarabatiwa ili viweze kufanya kazi kwa uhakika na salama.

"Daraja la Kigongo Busisi ni kati ya madaraja marefu Afrika, lina urefu wa Kilometa 3, tunatarajiwa likamilike Februari 2024.

"Kwa sasa limefikia hatua ya 72% na Wakandarasi hakuna wanachodai, wao ndio wanadaiwa na Serikali ya Rais Dkt. Samia.

"Likikamilika linatarajiwa kugharimu Tsh. Bilioni 716 na sehemu ambayo tulikuwa tunatumia saa tatu kuvuka lakini tutatumia dakika 5 hadi 10 kuweza kuvuka.


Mtendaji Mkuu wa TANROADS, Mhandisi Rogatus Mativila
Akizungumza katika tukio hilo kabla ya zoezi la kusaini mikataba, Mhandisi Mativila amesema "Kutakuwepo na madaraja manne utafanyika katika barabara ya Sengerema hadi Nyehunge (KM 54.4), makalavati makubwa 10,makalavati madogo 23, kutakuwa na ujenzi wa mifereji ya maji ya mvua na uwekaji wa alama za barabarani.

"Ujenzi wa barabara ya Sengerema-Nyehunge itaongeza ufanisi katika usafiri na usafirishaji katika Mkoa wa Mwanza.
a9ca708b-7f61-424b-bd87-57a1c74ac9dd.jpg
Barabara hii (Sengerema-Nyehunge KM 54.4) ni moja ya barabara muhimu katika mtandao wa barabara muhimu za Mkoa wa Mwanza na inaiunganisha Mkoa wa Mwanza na mikoa ya Kigoma, Kagera na Geita Kupitia Nyamadoke. Hivyo ni kiungo muhimu katika nchi yetu.

"Barabara ya Sengerema hadi Nyehunge utakapokamilika itachochea shughuli za ukuaji wa uchumi kama vile usafirishaji wa mazao ya misitu, chakula, uvuvi na mazao ya biashara.

"Upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Sengerema-Nyehunge ulifanywa na kampuni ya Inter Consult Ltd ya Tanzania kuanzia mwaka 2018 na kukamilika mwaka 2020 kwa gharama ya shilingi 779,274,725.80.

"Zabuni za ujenzi wa barabara hii (kutoka Sengerema hadi Mwanza) zilitangazwa tarehe 13 Juni, 2022 na kufunguliwa tarehe 30 Agosti, 2022. Jumla ya zabuni 12 zilipokelewa na kufanyiwa tathmini. Zabuni zilipokelewa kutoka kampuni 12.

"Mkandarasi aliyeshinda tuzo (katika ujenzi wa barabara ya Sengerema-Nyehunge KM 54.4 kwa kiwango cha lami) ni kampuni ya AVM-Dilingham Construction International Inc. ya nchini Uturuki.

“Mradi huu utajengwa kwa gharama ya shilingi 73,047,903,363.67, bila kujumuisha kodi ya ongezeko la thamani (18% VAT) ya Shilingi TZS 13,148,622,605.46. Muda wa utekelezaji wa mradi ni miezi 28.

"Napenda kutoa shukrani za dhati kwa serikali yetu kwa kutoa fedha za ujenzi wa mradi huu (wa barabara ya Sengerema-Nyehunge KM 54.4 kwa kiwango cha lami). Wakala ya Barabara (TANROADS) itasimamia utekelezaji wa mradi huu na kuhakikisha kuwa Mkandarasi anazingatia viwango vya kiufundi (Technical Standards) na mradi unakamilika kwa wakati.

"Natoa wito kwa mkandarasi anayetekeleza mradi wa ujenzi wa barabara ya Sengerema-Nyehunge KM 54.4 kwa kiwango cha lami, kampuni ya AVM-Dilingham Construction International Inc. kufanya kazi yake kwa weledi wa hali ya juu ili kazi zote zikamilike ndani ya muda uliopangwa na kwa viwango na gharama zilizokubalika.”
9311d8c5-20db-45c2-a92c-f4054ec4476f.jpg

77c94a77-b415-4418-bafb-12fb9ef9cb87.jpg

Mtendaji Mkuu wa TEMESA, Lazaro Kilahala
Akizungumza katika tukio hilo, Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) Lazaro N. Kilahala amesema “Serikali kupitia Wakala inafanya ukarabati wa vivuko 18 na Ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya vivuko katika maeneo 11 ya huduma kwa gharama ya Tshs 27.5 bilioni.

“Ujenzi wa kivuko kipya kitatoa huduma maeneo ya Buyagu-Mbalika Mkoani MwanzA, gharama ya ujenzi wa Kivuko ni Tsh. 3,817,064,000.00 (pamoja na VAT) na Ujenzi huu unatarajiwa kuchukua miezi kumi (10) baada ya Mkandarasi kupokea malipo ya awali.

“Kivuko kipya kinatarajiwa kuwa na uwezo wa kubeba Tani 50 zikijumuisha; abiria 100 (waliokaa 50 na waliosimama 50) pamoja na magari madogo (saloon cars) 6 na ujenzi utazingatia viwango vya kimataifa na utasimamiwa Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) ili kuhakikisha ubora na usalama wa kivuko kwa matumizi yaliyokusudiwa.

“Hitaji la kivuko kinachojengwa imekuwa ni kilio cha muda mrefu kwa wananchi wa maeneo hayo, hivyo Ujenzi wa kivuko hiki utakapokamilika utaondoa kero nyingi za kiuchumi na kijamii ambazo zimekuwa zikichelewesha maendeleo ya wananchi.

"Tunaishukuru sana Serikali ya Awamu ya 6 chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kwa kukubali kuanza utekelezaji wa mradi huu na mingine.“
ShiGONGO.jpg

Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo
Shigongo amesema “Kinachofanyika hapa ni ndoto kuanza kutimia kwa Wanabuchosa kuona walichokiota kwa muda mrefu kimeanza kutimia.

“Kwa vijana wa sasa wanaweza wasione kama Tanzania tunapiga hatua, wakati tunapata uhuru Mwaka 1961 tulikuwa tuna lami Kilometa 1,300 leo hii tuna Kilometa 14,000 tunaelekea Kilometa 15,000 tulikuwa tunasafiri kwa saa nane kutoka Buchosa kwenda Mwanza na basi lilikuwa moja.

“Kwa sasa unaweza kwenda na kurudi Mwanza mara kadhaa ukitokea Buchosa, maendeleo haya ya barabara inamaanisha umasikini unaenda kufika mwisho kwa wakazi wa uchosa, biashara zitafanyika, usafiri utakuwa rahisi, ujasiriamali na uchumi wa Buchosa utakua pia.
66d8751b-7a28-4e05-aa4e-fdaa77a53af5.jpg

39d50418-a077-4551-9247-280b0ec66132.jpg
 
Utawasikia hakuna barabara zinazojengwa tena . Watu wanafanya tena makubwa tu ila kwa staili tofauti siyo mikelele na kubweka kama vichaa
 
Ee si umeona wanavyopiga.
Wamepiga nn ambacho hakijawahi kupigwa . Tulishapigwa sana sasa kama magazeti, radio, TV nk vilikuwa kifungoni tungejuaje kama tunapigwa?
Acheni kukuza mambo upigaji haujawqhi kuisha Tanzania. Mtu anamuita mtengeneza ndege wanakaa wawili tu unajua 10% ya ndege moja ni shilingi ngapi?
 
sasa 54Km ambayo ni almost bil100 tunafanya sherehe na uzinduzi?.

Hapo Bosi wa tanroad mkoa angemalizana nao tu na ikikamilika tanroad mkoa wanaikabidhi kwa wadau kupitia RC kwa kufanya site visit mkutano na wananchi then done.

Tiss kupitia engineering dpt yao kila stage wanafanya balance and check feed back to state house, kama below standard wahusika wanakula vitanzi maisha yanaendelea...

Tujaribu kiwa smart kidogo, dunia inakwenda kasi sana, tukiendelea kutegemea akili hizi tutaachwa nyuma sana na kila siku tutakuwa ombaomba duniani.
 
sasa 54Km ambayo ni almost bil100 tunafanya sherehe na uzinduzi?.

Hapo Bosi wa tanroad mkoa angemalizana nao tu na ikikamilika tanroad mkoa wanaikabidhi kwa wadau kupitia RC kwa kufanya site visit mkutano na wananchi then done.

Tiss kupitia engineering dpt yao kila stage wanafanya balance and check feed back to state house, kama below standard wahusika wanakula vitanzi maisha yanaendelea...

Tujaribu kiwa smart kidogo, dunia inakwenda kasi sana, tukiendelea kutegemea akili hizi tutaachwa nyuma sana na kila siku tutakuwa ombaomba duniani.
Unaijua Bilioni hata 1 lakini?
 
Back
Top Bottom