Uthubutu wake, Kukabiliana Kwake na Umakini wake dhidi ya Janga la 'CORONA' lamfanya Rais Dkt. Magufuli akubalike kama 'Malaika' nchini Uganda

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,571
108,922
Watanzania najua baadhi yetu tunaweza ama tukawa hatujui 'Thamani' ya Rais Dkt. Magufuli au 'Umuhimu' wake Kwetu ila itoshe tu kusema kwamba pamoja na kwamba 'Kibinadamu' anaweza akawa na 'Mapungufu' yake kama niliyonayo Mimi GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE ila kwa Tanzania 'Kumpata' Kiongozi kama Yeye (JPM) ni kama vile Mwenyezi Mungu 'ametupendelea' sana tu.

Leo asubuhi kupitia Kipindi cha BBC News (Africa) kinachoruka Kuanzia Saa 1 na Nusu hadi Saa 2 Kamili (Redioni) nilibahatika kuwasikia Viongozi mbalimbali wa 'Kidini' na Wananchi kadhaa (waliowawakilisha) Wenzao (Waganda) katika 'Mjadala' mkubwa uliokuwa 'Mezani' wa Janga la CORONA na namna nzima ya 'Kukabiliana' nalo.

Mazunguzo ya 'Kimjadala' yalikuwa ni mengi na yenye 'Tija' na 'Mantiki' ila katika kila 'Mzungumzaji' aliyekuwa akichangia wote walikuwa 'wakimpongeza' sana Rais wa Tanzania Dkt. Magufuli kwa 'Kupambana' Kwake juu ya Janga la CORONA huku 'wakimshutumu' wazi wazi Rais wao Mzee Museveni kuwa 'ameshindwa' na kwamba kazidiwa mbali na Rais Magufuli.

Mwishoni kabisa Wote 'walisikika' wakisema kuwa laiti kungekuwa kuna uwezekano wa 'Kukopana' Marais hata kwa muda fulani tu basi kwa 'Taabu' ambazo wanazipitia sasa 'Waganda' na Maisha magumu 'waliyonayo' tokea Janga hili la CORONA lianze huku 'wakizuiwa' Kufanya Shughuli zao mbalimbali za 'Kiuchumi' basi wangetuomba Watanzania 'tuwakopeshe' Rais wetu huyu Dkt. Magufuli.

Kwa 'Kuhitimisha' Kwao tu Viongozi hao wa 'Dini' na Wananchi wa Uganda 'wamemtaka' Rais wao Mzee Museveni 'ayaige' mengi ya Rais Wetu JPM.

Nami GENTAMYCINE ANTIBIOUTIQUE ninamalizia pia kwa kusema hebu Watanzania 'tujivunie' mno Rais Magufuli na 'tumsaidie' pale anapokosea.
 
Mwishoni kabisa Wote 'walisikika' wakisema kuwa laiti kungekuwa kuna uwezekano wa 'Kukopana' Marais hata kwa muda fulani tu basi kwa 'Taabu' ambazo wanazipitia sasa 'Waganda' na Maisha magumu 'waliyonayo' tokea Janga hili la CORONA lianze huku 'wakizuiwa' Kufanya Shughuli zao mbalimbali za 'Kiuchumi' basi wangetuomba Watanzania 'tuwakopeshe' Rais wetu huyu Dkt. Magufuli.
I like this! Kama taarifa ni ya kweli, maana siku hizi, Mkuu, sikuelewi elewi haha haaa! (Take it ease, Mkuu!)
 
Jpm anampenda Mungu. Na hiki ndicho kinampa sifa kubwa Tanzania na duniani kwa ujumla

Mungu yupi? Hakuna mtu anayempenda Mungu wa mbinguni anayeweza kutamani wale wanaoishi kama malaika waishi kama mashetani. Halafu Mungu anaweza kumtumia mtu yeyote hata kama ni mbaya kama shatani. Mungu alimtumia mfalme Koreshi mpagani kuwaruhusu Israeli kwenda kujenga upya kuta za Yerusalemu na Hekalu.
 
Huko Uganda nakumbuka kuna jamaa alikuwa anaitwa Kibwetere, alichokifanya kwenye nyumba yake ya ibada kunaonyesha akili za Waganda. Hivyo sishangai baadhi ya Waganda wachache wakija na porojo hizi. Hata hivyo nilimpongeza Magufuli sio kwa kupambana na Corona maana hajawahi kupambana nayo, bali kutokutuweka lockdown maana nisingekubaliana naye, hatimaye ningeonekana napinga kila kitu. Maamuzi haya ni baadhi ya maamuzi machache sana niliyowahi kukubaliana na Magufuli toka awe rais.
 
Kwahiyo Wananchi wa Uganda na Viongozi wote wa 'Dini' wa Uganda hawayaoni 'Mema' au 'Mazuri' ya Rais JPM hadi Wewe 'Umchukie' namna hii?
 
Siku hizi nakupenda na naanza kukuelewa hasa katika 'Michango' yako hapa JF kwani hufanyi 'Criticism' kwa JPM bali unafanya 'Critique' tu. Heko!!
 
Kwahiyo Wananchi wa Uganda na Viongozi wote wa 'Dini' wa Uganda hawayaoni 'Mema' au 'Mazuri' ya Rais JPM hadi Wewe 'Umchukie' namna hii?

Sijasema nimemchukia ila nimekusaidia kujua kwamba kutumiwa na Mungu siyo sababu ya mtu kuwa mcha Mungu. Hata hivyo waganda siyo Watanzania. Biblia inasema asiyewajali wa nyumbani kwake ni mbaya kuliko asiyeamini. Inasaidia nini kusifiwa na Waganda wakati Watanzania wengi wamehudhunishwa?
 
waganda wako frustrated, Wamemchoka Museveni wanaona Magufuli ana nafuu kwao, lakini hiyo haimaanishi kuwa Magufuli ni raisi mzuri. Waliovunjiwa nyumba zao Mbezi Kimara wanakubaliana na mimi

Kwahiyo 'Chuki' yako Kwake Rais Magufuli ni kwa 'Kuvunjiwa' tu Nyumba huko Mbezi Kimara? Nilikuwa 'ninakuheshimu' sana ila sasa ninakudharau.
 
Sijasema nimemchukia ila nimekusaidia kujua kwamba kutumiwa na Mungu siyo sababu ya mtu kuwa mcha Mungu. Hata hivyo waganda siyo Watanzania. Biblia inasema asiyewajali wa nyumbani kwake ni mbaya kuliko asiyeamini. Inasaidia nini kusifiwa na Waganda wakati Watanzania wengi wamehudhunishwa?

Nipe hiyo Idadi ya hao Watanzania wako 'unaowasemea' hapa kuwa 'hawamkubali' Rais Dkt. Magufuli kati ya Watanzania Milioni 55+ waliopo sasa.
 
Back
Top Bottom