Uthubutu: Kijana atakayeelezea jinsi atakavyoizalisha elfu 50 ndani ya mwezi mmoja nitamkopesha bila riba

Kwa kijana yoyote ambae ramani hazijakaa sawa namshauri afwate huu ushauri kwa moyo wote na akili zote na kama ataona aibu ahame mkoa akaifanye mkoa mwingine kwa uhuru.kwani ni biashara ya mtaji mdogo na yenye faida kubwa.

Mimi ni shuhuda wa hii biashara na sijaiacha hadi leo.nilipomaliza college na kielimu cha diploma ya pharmacy nimedispense dawa kwenye maduka makubwa ya wahindi kwa miezi 3 tu nikiwa nalipwa laki 5 na nusu.
Nkaacha kazi nkasepa chuga kuuza mishkaki! Wazaz,ndugu na jamaa wacha wanilaumu mno hakuna hata mmoja alienisupport ila sasa hivi wananipongeza!

Yani watanzania wengi sijui tukoje,mtu yupo radhi afanye kazi ya heshima ila haina maslahi makubwa kuliko kazi isiyo na hadhi yenye faida lukuki.ndani ya mwezi wa kwanza tu niliingiza faida ya m1.2!sasa ndugu zangu wana jf kipi kilikua bora kati ya kugawa dawa huku ukiwa na clinical coat ndani ya kiyoyozi mhindi anakupelekesha siku nzima kafunga na camera kabisa kila kona ukichat au ukisinzia ni msala,kazi unaingia saa 1.30 hadi saa 2-3 usiku kila siku huku upande wa mishkaki nilikua nadaamka saa10 kwenda machinjioni kununua nyama kwa bei chee narudi naandaa saa12 niko shule ya msingi naanza kuwachomea madogo saa 6 mchana nshamaliza naingia mtaani kuangalia mishe nyingine,jioni tena huyo maeneo ya stendi kuchoma mishkaki.

Najua ni ngumu sana kwa msomi ila toka mkoa uliopo wanakujua nenda sehemu ambayo hakuna hata anaejua kama ulifika hata la 7!

Nilianza hivyo taratibu hatimae nkaweka vijana waaminifu niliowatoa vijijini huko na hivi nnavyoandika,naingiza si chini ya laki mbili faida kila siku ya Mungu bila pua za TRA wala cha Halmashauri
Ushauri huu mzuri Sana kaka
 
Back
Top Bottom