Uthubutu: Kijana atakayeelezea jinsi atakavyoizalisha elfu 50 ndani ya mwezi mmoja nitamkopesha bila riba

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,580
7,938
Mimi si tajiri ila nataka kuwafundisha utu na ubinadamu matajiri walioko JF.

Nataka kijana mwaminifu mmoja kutoka Jf nimwazime 50 na airejeshe baada ya mwezi mmoja au miwili ili nimwazime mwingine.

Changanua wazo lako na weka namba ya simu kama utapenda kuiweka hapa Kisha members wengine watanisaidia kumchagua mtu sahihi.

Please huu sio mkopo kwa wanaojiweza kwa sababu hauna riba na utakuwa umedhulumu haki ya mwingine.

Masharti na vigezo vitazingatiwa. Mshindi atatakiwa kusubmit some of his/ her details PM.

Pesa nitamtumia au kumkabidhi Ijumaa 21/ Febuari/2020.

Shindano litadumu kwa siku 3 tu.

UPDATES
23:15 Jumatano, nimefunga shindano
Nashukuru kwa mliojitokeza kuwania hichi kiasi kidogo cha 50.
Niko busy kidogo na majukumu na washiriki ni wengi.
Ninaomba Jumamosi weekend ndio nipitie post to post ili kuleta haki.
Mshindi atatangazwa na nitampa pesa mkononi kama yuko Dar na kama yuko mkoani nitamtumia na ya kutolea.
Kila mwezi nitafanya kitu hichi na atakayetengeneza faida kubwa zaidi nitampa Pesa nyingi zaidi.

UPDATES
JUMAMOSI SAA 2:50 ASUBUHI
Nimeanza kufanya sorting, niko page number 3. Leo hii hii mshindi atatangawa.

UPDATES
09:15 AM
Nimemaliza uchambuzi wa awali na kupata post 22 zenye nguvu zaidi.
Nakunywa chai kisha nimalizie kusort na kupata vijana 3 nitakaowaleta mbele yenu, asanteni.

Updates
09:48 am
Saturday
Nimepata watu hawa, na uchambuzi unaendelea miongoni mwao.
Kama kuna mtu hajatendewa haki anaruhusiwa kuleta malalamiko within one hour.
Walioingia kwenye kinyang'anyiro ni;
1.Zero IQ post no.29
2.Zwenge Ndaba post no.
3.Noelia, post no.170
4.CONTROLA post no.175
5.Davie post no.236
6.Naipenda Familia yangu, post.#57
7.Peramiho Yetu post #30
8.FK21 post #147.

Updates
1930 hrs
Ninaomba radhi kwa kuchelewesha matokeo ya mwisho.
Sikuwa hewani kwasababu zilizo nje ya uwezo.
But nikitulia nitamaliza kazi leo hii hii na mhusika atapewa chake kwa kadri tutakavyokubaliana njia ya kumfikishia Pesa yake.

Updates
23: 50
Nawashukuru washiriki wote wa shindano hili dogo.
Ninatamani kila mshiriki nimpe pesa nyingi kwaajili ya wazo lake ila kamba yangu ni fupi.
Nawashukuru pia wasomaji na wachangiaji wa Uzi huu.
Washindi ni hawa wafuatao;
3: Zwenge Ndaba, katika post yake #208 inayoelezea biashara ya maziwa kutoka Chalinze kwenda Kibaha au Dar es salaam.
2.Peramiho Yetu, katika post yake #30 anaelezea biashara ya Mahindi mabichi ya kuchoma kutoka Stereo Temeke .
1:Napenda Familia Yangu, katika post yake #57 ameelezea biashara ya maandazi na half cake .
Mimi kwasasa nitaanza na kutoa zawadi kwa mshindi nambari 1.
Kwa atakayekuniunga mkono anaweza kuungana nami kuwapa mtaji washindi nambari 2 & 3 au kumwongezea mtaji mshindi nambari moja.

Note:
Nitaendeleza hili jambo kila baada ya mwezi mmoja na ninawashauri watakaokosa wajaribu tena.
Mshindi anione pm
 
Nina jamaa yangu anafanya biashara ya samaki, anawanunua sehemu anakuja anakaanga na kuwauza nafikiri iyo 50 anaipata kwa wiki ama siku 2 kama atapata mzigo mfululizo.

Kama naruhusiwa kumkopea mimi nibebe dhamana niko tayari.
 
Mkuu, Mimi hapa ukinipatia Mtaji wa TZS 50,000 nitairejesha baada ya Miezi mitatu na nitaiwekeza katika huduma/biashara ya hii hapa chini:
  1. Nitaanzisha taasisi ambayo italenga kutoa huduma kwa wenye nyumba na wapangaji ambayo sio real estate agent bali ni zaidi kwa ajili ya kuwasaidia wapangaji kufahamu ubora wa nyumba kwa kuzifanyia nyumba grading,mitaa grading kwa kutumia vigezo vya kitaalam.Na nitaanza kwa kutoa huduma hio kwa jiji la Dar es Salaa kwanza.Gharama ya huduma hio itakuwa ni nafuu ambapo mwenye nyumba atalipia kisha Mpangaji akitaka kufahamu iwapo nyumba au eneo husika limefanyiwa utafiti atapatiwa ripoti ya eneo husika.
  2. Ripoti hizo zitakuwa za kiswahili na zitaonesha,wastani wa gharama za maisha,ikiwamo kodi chakula,maji umeme.Uwepo wa huduma za elimu afya na burudani,vituo vya polisi,mawasiliano ya viongozi wa eneo husika,usalama na uhalifu.Fursa za ajira zilizopa maeneo ya karibu.Fursa za biashara zilizopo maeneo hayo.
  3. Vilevile mpangaji anaweza kuomba kufanyiwa utafiti huo kabla ya kuhamia eneo fulani.
  4. Kwa kupitia taarifa hio tunaweza kupima na kutoa taarifa juu ya maeneo mazuri kabisa kuishi na maeneo mabaya kabisa kuishi na pia taarifa yetu itakusaidia kufahamu fursa na changamoto za kila eneo bila kujali umbali wa eneo.
Kwa shilingi elfu 50 utakayonipatia nitawekeza TZS 25000 kwenye kusajili jina la biashara brela na TZS 25000 kwenye kusajili domain name ambamo taarifa hzio zitawekwa.Mimi binafsi nitachangia gharama za kufanya hosting pamoja na gharama za kupata leseni ya biashara,gharama za nauli na uendeshaji kwa kipindi cha mwanzo.Iwapo utapenda kuwekeza zaidi katika biashara hii ili tuweze kuwa wabia tunaweza kujadili zaidi kwani wazo hili linahitaji mtaji wa TZS milioni 75 na lina potential ya kuleta mapato ya hadi milioni 150 kupitia huduma,matangazo commision n.k.

NB.Unaweza kutekeleza wazo hili ila hakikisha unawasiliana na mimi kwanza
 
Hiyo elfu 50 mchanganuo, wake kwa biashara ya mishikaki.

Naenda kwa Fundi kuchomelea aniandalie Jiko elfu 25,

Natafuta kijiwe kizuri sehemu wanayopita watu wengi,

--Sokoni nyama kg 2 steki tupu =16000,
--mkaa wa 1500
-Viungo vyake 5000(hiyo siyo vya siku moja ukinunua ni vingi mpaka viishe vitakaa kaa kidogo. )
-vijiti vile vistiki vyake 2000.

Naandaa mishikaki yangu ya wastani tu ya kuuza mia 2 mia 2 tu,

Kwenye kg 2 nina uhakika wa kupata faida ya 10K kila siku hapo baada ya kutoa matumizi ya mkaa, vijiti na Nyama.

Ndani ya wiki tayari nimekurudishia 50k yako.


NB:
Nilishawahi kufanya hii kazi hivyo nina uhakika nayo. Ndio kazi iliyonipa mtaji wa kibanda cha kuchakata viazi kuwa Chips.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna sehemu wale wakaanga ndizi kwenye mabanda ya chips huwa wanapata tabu kuzipata zile ndizi ndefu kubwa(mzuzu),,, sasa Kuna mahala zile zinapatikana kwa wingi, na huko zinanunuliwa sh 50 kila moja mara usafiri na vingine zinafika sokoni kwa sh 80 mpaka 90 kwa kila moja, na huwa zinachukuliwa kwa bei ya jumla 200 mpaka 250 kila moja.... Kwahiyo mtu hapo anaweza kutengeneza hiyo elfu 50 sio mwezi Bali tuchukulie wiki mbili tu maximum.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom