Uthubutu: Kijana atakayeelezea jinsi atakavyoizalisha elfu 50 ndani ya mwezi mmoja nitamkopesha bila riba

Unapikia kwa kutumia nishati gani hivi vitu?

Mvua ikinyesha au jua Kali unakaa wapi kufanya biashara yako?

Rudia tena mchanganuo wa hesabu zako Mr Finest

Nitatumia nishati ya mkaa /kuni
Kwa kawaida maeneo mengi ya shule unakuta kuna mahala pametengwa kwa hzo shughuli na unalipa ushuru kidogo sana

Pamaja na Hilo haka la biashara Kama vijishiringi vingi Sana boss
 
Elimu/makuzi yetu hayajatuandaa kuwa wajasiriamali bali wafanya biashara.

Hatuwez kutoboa kwa idea za biashara hizi ambazo kila kona ya nchi zipo.

Utapata hela ya kula tu.

Wazo la kijasiriamali ndio linahitajika.
 
Tofauti ni ipi hapo kati ya mfanyabiashara na mjasiriamali?
 
Tofauti ni ipi hapo kati ya mfanyabiashara na mjasiriamali?
Swali zuri sana, zipo tofauti tena kubwa nikipata muda nitaziweka hapa mfano tu
mfanya biashara ataenda mbeya atanunua mchele kwa magunia na kuja kuuza hivyo hivyo sokoni dar na kupata faida kawaida tofauti na mjasriamali hujiongea zaidi kwa kuongeza thamani ya bidhaa, huduma n.k

Yeye mjasriamali atau park kutoka kwenye gunia kusafisha polish kuufunga kilo moja moja na kuweka lebal ya jina la biashara yake na kuuzia madukani , supermarket n.k kwa faida kubwa zaidi.

Natumaini utakuwa na mwanga sasa wa tofauti zao
 
Naam nimepata mwanga

Shukran
 
Elimu/makuzi yetu hayajatuandaa kuwa wajasiriamali bali wafanya biashara.

Hatuwez kutoboa kwa idea za biashara hizi ambazo kila kona ya nchi zipo.

Utapata hela ya kula tu.

Wazo la kijasiriamali ndio linahitajika.

ano wa wazo lako hilo la kijasiliamari

Elimu/makuzi yetu hayajatuandaa kuwa wajasiriamali bali wafanya biashara.

Hatuwez kutoboa kwa idea za biashara hizi ambazo kila kona ya nchi zipo.

Utapata hela ya kula tu.

Wazo la kijasiriamali ndio linahitajika.
Unaweza leta wazo la kijasiliamari tione
 
Hiyo 50k mafanyia biashara ya matunda naenda hapo kilombero nanunua vitu vifuatavyo;
TIKITI kubwa-6000
Maembe-1500
Ndizi mbivu-1000
Matango-500
Apple 2@1000-2000
STRAWBERRY pkt 1-2000
Mananasi 3@1000-3000
Umma pkt 1- 1500
Percels(kontena zile)@300×20=6000
Tuishi 1-1000
Nauli -1000
JUMLA = 25,500
So kwenye hiyo 50k nitabakiwa na 24,500 kama akiba yangu.

Hapo tayari nina visu, karai kubwa, vitambaa kwa ajili ya kufuta kontena, meza kubwa ..

Naosha matunda vizuri kwa maji ya moto, napaki kwenye kontena kwa bei tofauti.

Kontena kumi naweka Apple, STRAWBERRY na matunda mengine, bei yake ni tsh 2000.

Kontena kumi naweka matunda yote kasoro apple na STRAWBERRY, bei yake ni tsh 1500.

Hivyo kwenye kontena kumi za 2000 nitapata tsh 20000 kama 'mauzo'

Kwenye kontena kumi za 1500 nitapata 15000 kama 'mauzo'

JUMLA itakuwa 35000 nikitoa 25,500 ya manunuzi nabakiwa na tsh 9500 kama faida khalisi ..nikifanya hii bizi kwa siku sita tu nazalisha tsh 50000 na kichele kama faida.

Hapo bado kuna 24,500 niliweka kama akiba

NB: HII NDIO BIASHARA NINAYOFANYA SASA.

Asante.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom