Uteuzi mpya wa Rais Samia, leo Juni 8, 2023, Prof. Abel Makubi ateuliwa kuwa Mkurugenzi wa MOI

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi wa nafasi kadhaa, amemteua Prof. Abel Makubi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa (#MOI) akichukua nafasi ya Dkt. Respicious Boniface ambaye amemaliza muda wake

Omar Issa ameteuliwa kuwa Mkuu wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST) akichukua nafasi ya Gharib Bilal (Makamu wa Rais Mstaafu) ambaye amemaliza muda wake

Amemteua Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee kuwa Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) akichukua nafasi ya Balozi Dkt. Marten Lumbanga aliyemaliza muda wake

Dkt. Edwin Mhende ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NMB Plc kwa kipindi cha pili
New.jpg

Prof. Abel Makubi.jpg

Prof. Abel Makubi
Dkt. Respicious Boniface.jpg

Dkt. Respicious Boniface
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewateua wafuatao:

1. Amemteua Bw. Omar Issa kuwa Mkuu (Chancellor) wa Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela (NM-AIST).

Bw. Issa ni Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO na anachukua nafasi ya Mhe. Dkt. Gharib Bilali, Makamu wa Rais Mstaafu ambaye amemaliza muda wake.

2. Amemteua Prof. Abel N. Makubi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Mifupa (MOI). Prof. Makubi anachukua nafasi ya Dkt. Respicious Boniface ambaye amemaliza muda wake.

3. Amemteua Dkt. Abdulhamid Yahya Mzee kuwa Mkuu wa Chuo (Chancellor) cha Taifa cha Ulinzi (NDC). Dkt. Mzee alikuwa Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na anachukua nafasi ya Balozi Dkt. Marten Y. C. Lumbanga aliyemaliza muda wake.

4. Amemteua Dkt. Edwin Mhede kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya NMB Plc kwa kipindi cha pili.

Uteuzi huu umeanza tarehe 06 Juni, 2023.

ADB3358F-73CD-4D5A-B6B0-DDB8B1BDF560.jpeg
 
Hii ndio kazi anayoiweza huyo msanii wetu, teuzi ilikuwa kila wiki, sasa ni kila siku!.

Mimi bado niko bandarini na ule mkataba wa hovyo, siondoki kule n'go!,

Wewe endelea kuteua tu hata kila dakika, hao wanaokufundisha huu utoto ili tusahau ujinga wenu mliofanya kwenye mkataba wanakudanganya.
 
Mmeacha Uteuzi wa Bandari!
Kamata haoo, shikaaa haooo, wana ona haya haoooo


Wamasai
Bandari
....na 2025 kwishney. Sijui watarudisha nini kwa Waarabu. Haki ya ngai.
 
Tunataka bandari yetu!! Watanzania tulinde rasilimali zetu!! Wasitutoe kwenye lengo!!

HUu mkataba wa Mangungo tuukatae kwa nguvu zote!!

Haiwezekani tuingizwe kwenye mkataba wa ajabu kuuza Lango kuu la uchumi wa wetu kwa miaka ya viazi vingi vya Watanganyika. Mkataba wa kinyonyaji, tuendeshe bandari yetu wenyewe!!
 
Inabidi tupate elimu ya URAIA vizuri.
  • Mambo ya Muungano na yapi?
  • Hao wa upande wa pili, wanawekwa kwenye sehemu sahihi zinazoruhusiwa kimuungano?
  • Nani ni mkaguzi na msimamizi wa hilo kwa huku Jamhuri?

Kule SMZ, ni strictly kwa wao tu!
 
Back
Top Bottom