Utawala wa Marehemu Magufuli - Blessing in Disguise

Uhodari wa kuandika matusi hausaidii kitu.Bwana "Regase" alikuwa mpigaji tu(ripoti ya CAG) na hakuwa na maono wala talanta ya uongozi.

Ripoti ya CAG ni kuanzia mwezi gani hadi mwezi gani kwani? Nazani iliyotoka kipindi jpm kakata moto ile ndo ilikua ya serikali aliyokua anaongoza. Lakini kwa hii ripoti ya sasa itakua kumuonea mwendazake tu. Hii ni ripoti ya kipindi cha hangaya tusikwepeshe kama kuna shida basi wabebeswe wa sasa
 
Kaisome ni ya kipindi kipi?
 
Wengi waliumizwa vibaya na utawala wa Marehemu Magufuli. Taifa liliumizwa na utawala wa Magufuli:

1) Katiba iliwekwa kapuni

2) Sheria ziliwekwa jalalani

3) Utekaji, upotezaji na mauaji ya watu walioonekana kuukosoa utawala wake likawa jambo la kawaida (tupo kwenye vita ya uchumi. Atakayekwenda tofauti ni msakiti. Ninyi wanajeshi mnajua msaliti huwa anafanywa nini - Magufuli)

4) Demokrasia ikatupwa chooni (sasa ni wakati wa kujenga nchi. Napiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa - Magufuli)

5) Kesi za kubambika watu ikawa adhabu kwa wale ambao utawala unataka kuwatia adabu (tajiri naweza kumfanya chochote wakati wowote - Magufuli)

6) Uporaji wa pesa za matajiri kikawa chanzo cha mapato ya serikali (DPP ongea na hao tunaowashtaki kwa ujumu uchumi. Wakikubali kutulipa, uwaachie, wakigoma, tena waache wakae huko moja kwa moja - Magufuli)

7) Kuibuka kwa wasaidizi wake majambazi (Sabaya, et al) wakiwa na mamlaka yasiyoguswa na chombo chochote

8) Matumizi ya pesa ya umma yasiyozingatia taratibu (report ya CAG)

9) Ufisadi uliolindwa na dola kwa kuziba midomo ya watu na uhuru wa vyombo vya habari (Magufuli aliiondoa Tanzania kwenye nchi zinazotekeleza mwongozo wa kuendesha Serikali kwa uwazi)

10) Kudororesha mahusiano ya kimataifa kwa ujeuri (vifaranga toka nchi jirani walichomwa, ng'ombe wa wafugaji wa nchi jirani 4,000 walioingia ardhi ya Tanzania walitaifishwa, na Magufuli akasema, Tanzania siyo shamba la bibi. Wiki moja baadaye ng'ombe wa wafugaji wa Tanzania 9,000 walikamatwa ndani ya ardhi ya Kenya, Wakaenya wakawarushia wafugaji wa Tanzania ng'ombea wote, na gavana wa Kenya kutamka kuwa uongozi wa Magufuli ulikuwa ni aibu ya Afrika. Watanzania wanalia, Wakenya wanalia)

11) Kuwajaza watu ujinga kwa propaganda mbalimbali (Magufuli akadai kuwa nchi yetu imekwishakuwa tajiri kiasi cha kuwa donor country, na miradi yote inajengwa kwa pesa zetu)

12) Kuwahadaa watu waamini kuwa mambo makubwa sana na ya pekee yanafanywa na utawala wake wakati mengi ya hayo mambo yalikwishafanywa hata na awamu zilizotangulia (SGR ya TAZARA ilijengwa wakati wa Mwalimu Nyerere, barabara za lami zenye urefu wa zaidi ya kilometa 12,000 zilijengwa wakati wa Kikwete, wakati wa Magufuli zilijengwa 2,800 tu. Ndege mpya 13 zilinunuliwa wakati wa Nyerere ukilinganisha ndege 8 zilizonunuliwa wakati wake. Daraja la Umoja wakati wa Mkapa, la Kigamboni wakati wa Kikwete, Mabwawa ya umeme ya Mtera, Kigansi, Kidatu, umeme wa gas ilikuwa wakati wa watanguluzi wake; yeye bwawa la Nyerere ikawa kelele kila siku. Vyuo vikuu UDSam, Sokoine, Dodoma; wakati wake hakuna hata kimoja. Hospitali kubwa Muhimbili, Mlaganzila, Taasisi ya Moyo ya Jakaya, Hospitali ya Mkapa; wakati waje hakuna hospitali kubwa hata moja; na mengine mengi, lakini aliwajaza ujinga raia wasio na uelewa waone kuwa watangulizi wake hawakufanya kitu)

13) Utawala wenye viashiria vya upendeleo na ubaguzi na wakati fulani kutamka wazi kabisa kuwa majimbo fulani ya uchaguzi hayatapelekewa maendeleo kwa sababu walichagua wapinzani

14) Kufuta uwepo wa bunge huru la wananchi na kumwagiza spika kuwa awashughulikie wabunge kule ndani kwa kuwatoa nje, halafu nje yeye atawashughulikia.

Kitu kilicho dhahiri ni kwamba Tanzania haijawahi kuwa na katiba nzuri bali ilitegemea hekima ya Rais, akiamua kuwaburuza, hakuna wa kumzuia.

Kuwepo kwa Marais waungwana, Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete, kuliwafanya watu waamini tuna katiba na sheria nzuri. Rais marehemu Magufuli ndiye aliyewafumbua macho Watanzania waone kuwa tuna katiba mbaya sana na tuna sheria mbaya sana. Hivyo ujio wa Rais Magufuli, pamoja na hasara tuliyoipata, umetusaidia sana kutambua ubovu na ubaya wa katiba na sheria zetu. Hivyo badala ya kuona kuwa utawala wa marehemu ilikuwa ni laana tupu, tushukuru pia kuwa ndio uliowafumbua wengi macho kutambua katiba yetu ni mbovu kiasi gani. Utambuzi huo iwe ni kichocheo kikubwa cha kutaka katiba mpya, siyo kesho wala keshokutwa bali SASA.

Tusipofanya hivyo, utawala wa Samia, kwa sababu na wenyewe umejaa uungwana, utatusahaulisha tatizo la msingi la Taifa letu, ambalo ni KATIBA MBAYA.
Mkuu mambo aliyoyafanya JPM kwa miaka sita umejaribu kuonyesha kama yalikuwa ni ya kawaida tu lakini yalihitaji ujasiri sana kuyafanya.

Kwa kiongozi wa kawaida tu angechukua miaka 20 kuweza kuyafanikisha. Siku zote kilicho kigumu ni kuanzisha mradi fulani kuumaliza sio suala gumu hata kidogo.

Kuhamia Dodoma tulikuwa tunapiga siasa tu JPM imemchukua miaka sita tu ofisi zote zipo huko. Mashirika ya ndege yalikuwa yamekufa na tunatizamana tu, amekuja JPM miaka sita ameshanunua ndege nane na nyingine tano zinakuja.

Hakuna awamu hata moja iliyofikiria kujenga daraja la Tanzanite linalopita juu ya maji mpaka alipokuja JPM na ameondoka ameacha limeshajengwa.

Jiji la Dar ndani ya miaka michache ijayo litakuwa linapambwa na fly overs nyingi, huu ni uthubutu wa JPM, hakuna hata mmoja katika waliomtangulia aliyeweza kuzijenga hizi fly overs.

Treni ya umeme kwenda mpaka Kigoma ilikuwa inajengwa ndotoni na kwenye makaratasi tu, kaja JPM hivi sasa treni za majaribio zinafanya kazi.

Unaweza kumponda JPM na ni haki yako ya kikatiba, lakini huwezi ukayashusha thamani yote aliyoyafanya tena kwa uzalendo wa hali ya juu.
 
Watanzania 90% wanaamini Magufuli alikuwa Kiongozi Bora Tanzania tangu iubwe.
Sijui tufanyeje kulibadili hili , labda tutengeneze na video za kusambaza Mabaya yake?
 
Kaisome ni ya kipindi kipi?

Sawa mkuu kwa mwendo huu ata ya miaka 10 ijayo itabidi tuisome tujue ni ya lini. Lakini kwa uelewa tu huwa ni kila mwaka inatoka ripoti mpya hivyo ya sasa haiusiani na mwendazake. Kama kuna vitu alianzisha havina maana basi serikali ya sasa inao uamuzi ya kutokuiendeleza mazima.
 
Kaisome ni ya kipindi kipi?
kama mwenyezi mungu angesimama kuhesabu makosa yetu nani angesimama na kudai ni mkamilifu ila ni mungu basi kwakuwa sisi ni viumbe wake tutende kama baba yetu wa mbinguni ili tutimize mapenzi yake
magu amemaliza safari yake dunian ni mungu pekee ndio atamuhukumu tuache kumsema vibaya sisi hatukujua kusudi la mungu
 
Hujaelewa nilichoandika
Ndo sasa linganisha hao wengine na miaka mitano ya JPM.

Taifa hili lingefikia hatua gani Kwa miaka kumi Yake ??

Ni Kwa sababuya Falsafa za Xi Jinping , China Sasa ndo Taifa lapili Kwa uchumi Duniani kiasi kwamba wamemzawadia zawadi yakukaa madarakan miaka mingi.

Nchii aitaji viongozi wenye maono, uthubutu ,Maendeleo hayaletwi na wazungu mnaoenda kuwalialia misaada .

Mambo mengi sana Kwa Sasa yamesimama, mengine yamerudi Kule yalikokua.

Ndio maana nasema, ni wajinga wapumbavu, vyeti feki, watumishi hewa, wapigaji, wenye Maisha ya ujanja ujanja na WA aina hiyo ndio pekee wanaweza kudharau kazi alizofanya JPM.

Na JPM anawaumiza sana, kiasi kwamba pamoja nakutangulia kwake, bado mnaumia kuona kwamba kaacha mambo mengi yanayoelezea Dhamira yakeBora Kwa Taifa hili.
 
China limekua Taifa la pili kwa ukubwa wa uchumi duniani tangu enzi Hu Jintao akiwa Rais wake.
Ndo sasa linganisha hao wengine na miaka mitano ya JPM.

Taifa hili lingefikia hatua gani Kwa miaka kumi Yake ??

Ni Kwa sababuya Falsafa za Xi Jinping , China Sasa ndo Taifa lapili Kwa uchumi Duniani kiasi kwamba wamemzawadia zawadi yakukaa madarakan miaka mingi.

Nchii aitaji viongozi wenye maono, uthubutu ,Maendeleo hayaletwi na wazungu mnaoenda kuwalialia misaada .

Mambo mengi sana Kwa Sasa yamesimama, mengine yamerudi Kule yalikokua.

Ndio maana nasema, ni wajinga wapumbavu, vyeti feki, watumishi hewa, wapigaji, wenye Maisha ya ujanja ujanja na WA aina hiyo ndio pekee wanaweza kudharau kazi alizofanya JPM.

Na JPM anawaumiza sana, kiasi kwamba pamoja nakutangulia kwake, bado mnaumia kuona kwamba kaacha mambo mengi yanayoelezea Dhamira yakeBora Kwa Taifa hili.
 
Hakuwa mkweli
Hii itamuandama vizazi na vizazi
Useme ukweli kwenye nini wakati inaonekana
FB_IMG_1618256675020.jpg
 
Zawadi kuu ambayo Magufuli amewaachia watanzania ni uwezo wa kutambua sifa halisi za kiongozi anayefaa kuliongoza Taifa hili.
Ni zipi hizo sifa, Je kati ya Marais wote sita wanagapi hawana hizo sifa
 
Wengi waliumizwa vibaya na utawala wa Marehemu Magufuli. Taifa liliumizwa na utawala wa Magufuli:

1) Katiba iliwekwa kapuni

2) Sheria ziliwekwa jalalani

3) Utekaji, upotezaji na mauaji ya watu walioonekana kuukosoa utawala wake likawa jambo la kawaida (tupo kwenye vita ya uchumi. Atakayekwenda tofauti ni msakiti. Ninyi wanajeshi mnajua msaliti huwa anafanywa nini - Magufuli)

4) Demokrasia ikatupwa chooni (sasa ni wakati wa kujenga nchi. Napiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa - Magufuli)

5) Kesi za kubambika watu ikawa adhabu kwa wale ambao utawala unataka kuwatia adabu (tajiri naweza kumfanya chochote wakati wowote - Magufuli)

6) Uporaji wa pesa za matajiri kikawa chanzo cha mapato ya serikali (DPP ongea na hao tunaowashtaki kwa ujumu uchumi. Wakikubali kutulipa, uwaachie, wakigoma, tena waache wakae huko moja kwa moja - Magufuli)

7) Kuibuka kwa wasaidizi wake majambazi (Sabaya, et al) wakiwa na mamlaka yasiyoguswa na chombo chochote

8) Matumizi ya pesa ya umma yasiyozingatia taratibu (report ya CAG)

9) Ufisadi uliolindwa na dola kwa kuziba midomo ya watu na uhuru wa vyombo vya habari (Magufuli aliiondoa Tanzania kwenye nchi zinazotekeleza mwongozo wa kuendesha Serikali kwa uwazi)

10) Kudororesha mahusiano ya kimataifa kwa ujeuri (vifaranga toka nchi jirani walichomwa, ng'ombe wa wafugaji wa nchi jirani 4,000 walioingia ardhi ya Tanzania walitaifishwa, na Magufuli akasema, Tanzania siyo shamba la bibi. Wiki moja baadaye ng'ombe wa wafugaji wa Tanzania 9,000 walikamatwa ndani ya ardhi ya Kenya, Wakaenya wakawarushia wafugaji wa Tanzania ng'ombea wote, na gavana wa Kenya kutamka kuwa uongozi wa Magufuli ulikuwa ni aibu ya Afrika. Watanzania wanalia, Wakenya wanalia)

11) Kuwajaza watu ujinga kwa propaganda mbalimbali (Magufuli akadai kuwa nchi yetu imekwishakuwa tajiri kiasi cha kuwa donor country, na miradi yote inajengwa kwa pesa zetu)

12) Kuwahadaa watu waamini kuwa mambo makubwa sana na ya pekee yanafanywa na utawala wake wakati mengi ya hayo mambo yalikwishafanywa hata na awamu zilizotangulia (SGR ya TAZARA ilijengwa wakati wa Mwalimu Nyerere, barabara za lami zenye urefu wa zaidi ya kilometa 12,000 zilijengwa wakati wa Kikwete, wakati wa Magufuli zilijengwa 2,800 tu. Ndege mpya 13 zilinunuliwa wakati wa Nyerere ukilinganisha ndege 8 zilizonunuliwa wakati wake. Daraja la Umoja wakati wa Mkapa, la Kigamboni wakati wa Kikwete, Mabwawa ya umeme ya Mtera, Kigansi, Kidatu, umeme wa gas ilikuwa wakati wa watanguluzi wake; yeye bwawa la Nyerere ikawa kelele kila siku. Vyuo vikuu UDSam, Sokoine, Dodoma; wakati wake hakuna hata kimoja. Hospitali kubwa Muhimbili, Mlaganzila, Taasisi ya Moyo ya Jakaya, Hospitali ya Mkapa; wakati waje hakuna hospitali kubwa hata moja; na mengine mengi, lakini aliwajaza ujinga raia wasio na uelewa waone kuwa watangulizi wake hawakufanya kitu)

13) Utawala wenye viashiria vya upendeleo na ubaguzi na wakati fulani kutamka wazi kabisa kuwa majimbo fulani ya uchaguzi hayatapelekewa maendeleo kwa sababu walichagua wapinzani

14) Kufuta uwepo wa bunge huru la wananchi na kumwagiza spika kuwa awashughulikie wabunge kule ndani kwa kuwatoa nje, halafu nje yeye atawashughulikia.

Kitu kilicho dhahiri ni kwamba Tanzania haijawahi kuwa na katiba nzuri bali ilitegemea hekima ya Rais, akiamua kuwaburuza, hakuna wa kumzuia.

Kuwepo kwa Marais waungwana, Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete, kuliwafanya watu waamini tuna katiba na sheria nzuri. Rais marehemu Magufuli ndiye aliyewafumbua macho Watanzania waone kuwa tuna katiba mbaya sana na tuna sheria mbaya sana. Hivyo ujio wa Rais Magufuli, pamoja na hasara tuliyoipata, umetusaidia sana kutambua ubovu na ubaya wa katiba na sheria zetu. Hivyo badala ya kuona kuwa utawala wa marehemu ilikuwa ni laana tupu, tushukuru pia kuwa ndio uliowafumbua wengi macho kutambua katiba yetu ni mbovu kiasi gani. Utambuzi huo iwe ni kichocheo kikubwa cha kutaka katiba mpya, siyo kesho wala keshokutwa bali SASA.

Tusipofanya hivyo, utawala wa Samia, kwa sababu na wenyewe umejaa uungwana, utatusahaulisha tatizo la msingi la Taifa letu, ambalo ni KATIBA MBAYA.

Una Akili za kufungua mlango wa Maliwato tu. Asante
 
Nimesema hospitali kubwa siyo hospitali za Wilaya au vituo vya afya.

Kwa ufafanuzi zaidi, hospitali zote za Wilaya na vituo vya afya vilivyojengwa wakati wa awamu ya 5, katika thamani havifikii hospitali moja kubwa kama Mloganzila au Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, zilizojengwa awamu ya 4.

Wakati wa awamu ya 5, kulijengwa 2,800km za lami. Wakati wa awanu ya 4 zilijengwa 12,000km za lami. Compare the difference.
Bams tutakuwa tunabishana tu, lkn mambo aliyofanya magu hao wengine huenda waliyaogopa kwani yalikuwapo lkn hayakufanyika, magu ni akili kubwa nchi hii haijawahi kupata ndiyo maana Hadi Leo mwaka umeshapita lkn mapambano dhidi ya marehemu yameshamili,boss hataki kufunikwa.
 
Kuna mipumbavu imelipwa humu kumsema Jpm hebu kanyeni mkalale hizo kenge zenu mnazo zitetea ndo zinajimilikisha nchi kama ni ya ukoo wao.... nyie kenge mkiambulia buku saba jioni mnarudi kukaa kwa shemeji zenu na kulala sebureni shwain kabisa.
Acha hoja ijadiliwe na wenye akili timamu.
 
Heee kwani Magufuli ndio agenda 2022?mnaboo endeni mfanye kazi.
Au mkishinda hapa mnamnanga ndio tutapata maendeleo.
Mnakazana kutukana asieskia wala kuwajibu.
Hakuna vitu vizuri vya maendeleo mlete tujadili?
Hatumtukani marehemu, tuyataja mambo aliyoyatenda vibaya, yaliyotupa funzo, na kisha tuone namna ya kuenenda vizuri, na mfumo wa utawala, kwa kupitia katiba, uzuie kabisa mtu kutenda uovu kama alioutenda marehemu, hata kama mtu hiyo atakuwa ni Rais.
 
Hakuna kitu na hujui kitu
Unaweza kujifanya unajua na wengine hawajui, kumve ni wewe usiyejua.

Toa hoja kukubali au kupinga, na watu wengine watajua kama unajua chochote au hujui. Hujui kitu kwa kusema tu najua bali kwa kuonesha unachojua.
 
basi tusimseme sana marehemu kwa sababu waliopo madarakan wapo since 2015
Stallin alikuja kutangazwa kama dictator na mkomunisti wa kifashisti baada ya miaka 10 tangu alipofariki, na maziko yake kuhudhuriwa na watu wengi kuliko mtu mwingine yeyote Duniani, huku mamia wakifa kwa kusukumana wakati wa kuuaga mwili wake.

Huko mbeleni ni lazima itakuja kutolewa report jinsi utawala wa Magufuli ulivyokuwa na maovu mengi. Yatakapowekwa wazi, hakuna atakayesimama hadharani na kusema kuwa eti alikuwa Rais mzalendo.

Mzalendo wa Taifa lazima atathamini Taifa lake, na Taifa ni watu na kila kilichomo ndani ya mipaka ya nchi. Huwezi kusema wewe ni mzalendo, halafu unateka watu, unawapoteza, unawaua, na kuwaonea.
 
Unashanga nn?? Nitajie Kiongozi Wa Afrika kwasasa ambaye anaubora.

Hivi Rais Maguful mpaka baadhi ya mataifa,, Raia wao wakataman ndio angekua Rais wao....

Kuna Rais mwingine TZ alipendwa namna hiyo??

Nyeupe semeni ni Nyeupe!!.
Nenda mataifa jirani ukaone nchi kadhaa ambazo mitaa, barabara na baadhi ya infrastructure zina majina ya Nyerere. Halafu niambie ni nchi gani, ina jipo genge la mama nitilie lenye jina la Magufuli.
 
Back
Top Bottom