Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,543
- 41,047
Wengi waliumizwa vibaya na utawala wa Marehemu Magufuli. Taifa liliumizwa na utawala wa Magufuli:
1) Katiba iliwekwa kapuni
2) Sheria ziliwekwa jalalani
3) Utekaji, upotezaji na mauaji ya watu walioonekana kuukosoa utawala wake likawa jambo la kawaida (tupo kwenye vita ya uchumi. Atakayekwenda tofauti ni msakiti. Ninyi wanajeshi mnajua msaliti huwa anafanywa nini - Magufuli)
4) Demokrasia ikatupwa chooni (sasa ni wakati wa kujenga nchi. Napiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa - Magufuli)
5) Kesi za kubambika watu ikawa adhabu kwa wale ambao utawala unataka kuwatia adabu (tajiri naweza kumfanya chochote wakati wowote - Magufuli)
6) Uporaji wa pesa za matajiri kikawa chanzo cha mapato ya serikali (DPP ongea na hao tunaowashtaki kwa ujumu uchumi. Wakikubali kutulipa, uwaachie, wakigoma, tena waache wakae huko moja kwa moja - Magufuli)
7) Kuibuka kwa wasaidizi wake majambazi (Sabaya, et al) wakiwa na mamlaka yasiyoguswa na chombo chochote
8) Matumizi ya pesa ya umma yasiyozingatia taratibu (report ya CAG)
9) Ufisadi uliolindwa na dola kwa kuziba midomo ya watu na uhuru wa vyombo vya habari (Magufuli aliiondoa Tanzania kwenye nchi zinazotekeleza mwongozo wa kuendesha Serikali kwa uwazi)
10) Kudororesha mahusiano ya kimataifa kwa ujeuri (vifaranga toka nchi jirani walichomwa, ng'ombe wa wafugaji wa nchi jirani 4,000 walioingia ardhi ya Tanzania walitaifishwa, na Magufuli akasema, Tanzania siyo shamba la bibi. Wiki moja baadaye ng'ombe wa wafugaji wa Tanzania 9,000 walikamatwa ndani ya ardhi ya Kenya, Wakaenya wakawarushia wafugaji wa Tanzania ng'ombea wote, na gavana wa Kenya kutamka kuwa uongozi wa Magufuli ulikuwa ni aibu ya Afrika. Watanzania wanalia, Wakenya wanalia)
11) Kuwajaza watu ujinga kwa propaganda mbalimbali (Magufuli akadai kuwa nchi yetu imekwishakuwa tajiri kiasi cha kuwa donor country, na miradi yote inajengwa kwa pesa zetu)
12) Kuwahadaa watu waamini kuwa mambo makubwa sana na ya pekee yanafanywa na utawala wake wakati mengi ya hayo mambo yalikwishafanywa hata na awamu zilizotangulia (SGR ya TAZARA ilijengwa wakati wa Mwalimu Nyerere, barabara za lami zenye urefu wa zaidi ya kilometa 12,000 zilijengwa wakati wa Kikwete, wakati wa Magufuli zilijengwa 2,800 tu. Ndege mpya 13 zilinunuliwa wakati wa Nyerere ukilinganisha ndege 8 zilizonunuliwa wakati wake. Daraja la Umoja wakati wa Mkapa, la Kigamboni wakati wa Kikwete, Mabwawa ya umeme ya Mtera, Kigansi, Kidatu, umeme wa gas ilikuwa wakati wa watanguluzi wake; yeye bwawa la Nyerere ikawa kelele kila siku. Vyuo vikuu UDSam, Sokoine, Dodoma; wakati wake hakuna hata kimoja. Hospitali kubwa Muhimbili, Mlaganzila, Taasisi ya Moyo ya Jakaya, Hospitali ya Mkapa; wakati waje hakuna hospitali kubwa hata moja; na mengine mengi, lakini aliwajaza ujinga raia wasio na uelewa waone kuwa watangulizi wake hawakufanya kitu)
13) Utawala wenye viashiria vya upendeleo na ubaguzi na wakati fulani kutamka wazi kabisa kuwa majimbo fulani ya uchaguzi hayatapelekewa maendeleo kwa sababu walichagua wapinzani
14) Kufuta uwepo wa bunge huru la wananchi na kumwagiza spika kuwa awashughulikie wabunge kule ndani kwa kuwatoa nje, halafu nje yeye atawashughulikia.
Kitu kilicho dhahiri ni kwamba Tanzania haijawahi kuwa na katiba nzuri bali ilitegemea hekima ya Rais, akiamua kuwaburuza, hakuna wa kumzuia.
Kuwepo kwa Marais waungwana, Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete, kuliwafanya watu waamini tuna katiba na sheria nzuri. Rais marehemu Magufuli ndiye aliyewafumbua macho Watanzania waone kuwa tuna katiba mbaya sana na tuna sheria mbaya sana. Hivyo ujio wa Rais Magufuli, pamoja na hasara tuliyoipata, umetusaidia sana kutambua ubovu na ubaya wa katiba na sheria zetu. Hivyo badala ya kuona kuwa utawala wa marehemu ilikuwa ni laana tupu, tushukuru pia kuwa ndio uliowafumbua wengi macho kutambua katiba yetu ni mbovu kiasi gani. Utambuzi huo iwe ni kichocheo kikubwa cha kutaka katiba mpya, siyo kesho wala keshokutwa bali SASA.
Tusipofanya hivyo, utawala wa Samia, kwa sababu na wenyewe umejaa uungwana, utatusahaulisha tatizo la msingi la Taifa letu, ambalo ni KATIBA MBAYA.