A Bless in Disguise

A Bless in Disguise

GoLC

JF-Expert Member
Joined
Jul 10, 2025
Posts
219
Reaction score
376
Ndivyo ninavyoweza kusema. Kuna vitu vingine vinatokea pengine sio kwa bahati mbaya. Aidha ni roho wa Mungu katika kinywa cha mwanadamu au ni mtu mwenyewe katika kuponya hali fulani.

CHADEMA kilipoambiwa kitoe maelezo ni kwa nini kisisimamishwa usajili, ilionekana ni pigo kali kwa demokrasia iliyoanza kuonekana. Wakati wakiendelea kutafakari wafanye nini na wajibu vipi, aliibuka Mwenyekiti wa UWT - CCM, Mary Chatanda na kauli yake ngumu kuzema. Kauli hiyo imekuwa ni egemeo (leverage) zuri sana kwa Chadema kiasi cha kumfanya msajili wa vyama Nugu Nyahoza kupata kigugumizi kikali sana atoe vipi maamuzi kwa jambo lake.

CHADEMA imshukuru sana huyu mama, na wote ambao kwa namna moja au nyingine wanakuwa egemeo zuri la kimaamuzi hasa kwa kipindi hiki. Tutegemee mengi zaidi yafananayo na hayo, yaliyotangulia na yajayo.

Naviombea vyama vyote vidumu. Naviombea ushindani wa haki. Naombea maneno ya Makamu wa Rais kuhusu chaguzi mbalimbali yawe heri na kwa vitendo
 
Chadema tunamshukuru Mungu wetu aliye hai kwa namna anavyotuonyesha njia tutakayoiendea huku jicho lake Mungu likitutazama. Zaburi 32:8
 
Back
Top Bottom