Utatu wenye utata: Umri, Pesa na Mapenzi

Habari zenu wana JF. Ni matumaini yangu kuwa mu wazima wa afya njema na mnaendelea kufuhia hii weekend njema.

Kama kichwa kinavyojieleza hapo juu hapo juu napenda kukuthibitishia kwamba pesa si kitu katika mahusiano ya kimapenzi.
kumekuwa na kasumba kuwa ukitaka mahusiano yako yawe imara na thabiti ni lazima uwe na pesa nyingi za kuweza kumpa mpenzi wako/ ili umhudumie kwa kiwango cha hali ya juu ile nae kwa upande wa mweingine aweze kukuonesha upendo wa dhati na wa kweli. kiukweli siyo jambo baya kuwa na pesa nyingi lakini kuwa na pesa nyingi usifikiri ndiyo utapewa au kuoneshwa kila kitu katika mahusiano.

Frankly speaking, hi dhana ya kwamba pesa ndiyo kila kitu katika mapenzi ni uongo na upotoshaji mkubwa sana kwa sababu leo nilienda sehemu Fulani kupata chakula cha mchana baada ya kutoka job.

Wakati napata msosi wangu wa nguvu akatokea mdada mmoja hivi mzuri sana na mwenye mikogo japo hana maringo hata kidogo na ana sifa zote za uzuri.
katika kupiga stori akasema nanukuu "nyie wanaume mnafikiri mapenzi ni pesa wapo wanawake ambao hawahitaji pesa kutoka kwako ila tu kuna kikundi cha wanawake wachache sana ambao wanatuchafua tuonekane kama tunapenda pesa sana wakati siyo kweli hasa. Tatizo lenu hamjui shughuli, mshughulikie mwanamke mpaka asubuhi anapondoka kutoka kwako kwenda kwao au kazini asahau kukuomba hela na hata ukimpa aikatae"

Nilipigwa na butwaa kusikia hayo maneno kutoka kwa mwanamke mzuri kama yule.
nilizidi kumdadisi sana ili afunguke Zaidi but muda wake ukawa umeisha wa kukaa pale hivyo akawa ameondoka na kuniacha njia panda.Ingawa kutokana na maneno yake na utafiti ambao nimekuwa nikiufanya nimegundua kuwa nyie dada zetu mnataka mapenzi na siyo pesa ila pindi ukimkuta jamaa ana pesa yake na hayuko vizuri kitandani huwa mnatafuta mbadala ili muweze kukidhi haja zenu za kimwili.

Mbali na huyo mdada aliyoyasema hayo maneno siku moja nikiwa pale MARRYBROWN nilimsikia mama mmoja analamika sana kwa mume wake anamtesa sana, nanukuu "shida siyo pesa unazonitumia, pesa ni kitu gani kwani? usije ukanilaumu mwisho wa siku kwani kutoka hapo Dodoma mpaka Dar kuna umbali gani?"

Siku nyingine nilipewa simu na mama wa makamo ili nimrekebishie WhatsApp yake. Baada ya kutengamaa ikabidi nichungulie kidogo kwenye conversations zake kwa bahati nzuri /mbaya nikakuta the same case. Kiukweli nilishangaa sana hivyo ikapelekea nigundue kuwa pesa si kitu na haina nafasi katika mahusiano bali mapenzi ya dhati tu.

UShahidi mwingine ni kwamba kumezuka na limbi kubwa sana la majimama ya mjini (sugar mumies) kupenda kutafunwa na vijana wadogo sana.( mashababi). Hao wamama huwa wanajinadi kwa kusema kuwa baba zetu wamechoka sana. wakipiga kimoja tu chali wanabaki kutoa ulimi nje.s Siyo maneno yangu bali yao.

Wanaume wenzangu naomba tuwe tunawashughulikia vizuri hawa viumbe mpaka wasahau kuomba pesa.
Let's not create any gap ambayo inapelekea tuombwe pesa hovyo na hawa viumbe. Hakika ukiwa vizuri hautaona vibomu vya hapa na pale.
Ila ukiwa mdhaifu na akajua udhaifu wako atakusumbua sana maana anajua kabisa game hujui kupiga hivyo ulinzi wako kwake ni pesa tu basi.
Ukijua kupiga kazi nzuri, ukamheshimu na kumjali hautaombwa hata mia.

Wanaume wenzangu tuache udhaifu wa kuwapa pesa hawa viumbe tukidhani ndiyo tutaoneshwa upendo uliyo wa kweli na wa dhati.
Natumai tumeelewana.

Namalizia kwa kusema kuwa pesa haina nafasi katika mahusiano ya kimapenzi.

ahsanteni na karibuni kwa michango yenu.
 
Mtoa mada sijaelewa hapo:-
-tuwajigiji kwasana nakwautaalamu mpaka tuwalizishe au tuwe namapenzi yadhati kwao natuwaheshimu kipi hapo Kipo sawa mkuu
 
Back
Top Bottom