Utatu wenye utata: Umri, Pesa na Mapenzi

Utatu wenye utata: Umri, Pesa na Mapenzi

huwa nawaza matumizi ya pesa ikitokea yamefutwa sijui tutahongana maembe!
kujiendekeza tu,sio kweli kwamba bila pesa hakuna mapenzi ya kweli,nakataa kwa 100%
Umeelewa kilichoandikwa vizuri?!
pesa haina mbafdala ndio mana shetani anaimiliki
Elezea shetani anamiliki vipi pesa
Pesa muhimu sn ktk maisha
Ina umuhimu lakini isikulevye...mlinde mwenza ama mkeo, somesha wanao shule nzuri, inshort weka familia yako vizuri lakini vyote hivyo viongozwe na upendo
 
Pesa ina nafasi yake kwenye real love

Pesa sawa na msingi wa nyumba. Bila msingi wa nyumba sidhani kama tutaweka paa.



Tutafute pesa tu hamna namna
Ni kweli comrades, but watu kuna kitu kidogo sana wanakosea,ukishakosea hicho basi hata utafutaji wako wa pesa na kua nazo hauna maana, na utakufa a lonely and stressed rich person
 
Pesa sio ishu sana kama kuna upendo toka moyoni, sasa kama mmoja wenu anategemea pesa ndio iamue juu ya penzi lake kwako lazma utashangaa siku ukiwa huna hizo hela.

Gubu, lawama na kukoseshana amani kutawala mbaya zaidi usaliti utafatia na wala hatojali hata kama ni ajali imekufanya uwe kitandani hauna uwezo wa kuleta pesa, au ugonjwa flani unaokutesa ghafla unajiuguza.

Pesa zinaisha ila upendo halisi hauishi, unaweza kuwa na mpenzi wako ukawa huna kitu ila still akakuona kama Chris brown vile. Haambiwi asikii yani anaona raha tu kuwa pamoja na wewe full time muongee na kufurahia maisha.
 
Mapenzi sio pesa, hata kama huna maisha yanaendelea

Mapenzi ni kama Mboga na pesa ni kama spices
Sasa ukikosa spices unakula Mboga isiyona spices, na maisha yanaendelea, kikubwa ni amani
 
Back
Top Bottom