Utata wa kutumia picha ya Mlima Kilimanjaro ikiwa inawaonyesha Tembo.

mm nadhani alitaka tu kutujuza kuwa hiyo picha ilichukuliwa upande wa kenya kwa kuwa tz hakuna view hiyo ila wanajf wajue.sijaona kitu kibaya kuchukuliwa picha upande mwingine.la msingi ni kupata wiew nzuri ya picha kwani hata ss tunapopiga picha tunatafuta view nzuri ili picha ionekane murua.sijaona swala la ukabila hapo bali nimeona swala la uzalendo la kuonyesha uzuri wa maandhali ya uchagani.pia kuna sehemu nyingi tz zina maandhali nzuri,kama mbeya (tukuyu),mbinga (Ruvuma),iringa,kagera,tanga hata baadhi ya sehemu ya mkoa wa kigoma kwa maana ya wilaya ya kasulu na buhigwe.
Una maana gani?
 
Kwa akili yako unajua huo mlima ni wa Wakenya.

Hamja muelewa MURUSI anachomaanisha ni kuwaalready kwenye soko la utalii baada ya upotoshwaji wa muda mrefu inajulikana kuwa mlima Kilimanjaro upo Kenya. Watalii wengi wanaaminishwa kuwa kuona mlima Kilimanjaro uene kenya. Matumizi ya hiyo picha ina re inforce hizo wrong belief kuwa mlima uko Kenya. Ila ukweli unabaki kuwa Mlimauko TZ.
 
Hamja muelewa MURUSI anachomaanisha ni kuwaalready kwenye soko la utalii baada ya upotoshwaji wa muda mrefu inajulikana kuwa mlima Kilimanjaro upo Kenya. Watalii wengi wanaaminishwa kuwa kuona mlima Kilimanjaro uene kenya. Matumizi ya hiyo picha ina re inforce hizo wrong belief kuwa mlima uko Kenya. Ila ukweli unabaki kuwa Mlimauko TZ.
Mlima uko Tanzania. Upo Tanzania.
 
Mke wako akipigwa picha buchani utasema sio wako kwa vile siku hiyo hukumpa hela ya nyama

Sent from my using Tapatalk
 
Nadhani mto mada hoja yake ni hiyo picha/mchoro ya mlima yenye muonekano kutokea kenya kuwepo ikulu ya Tanzania....
Badala ile inayoonyesha migomba....
Na picha hiyo pia inatumiwa na wakenya kunadi mbuga yao huku wakionyesha unaweza kuona mbuga na mlima kwa wakati huohuo hivyo kuvutia watalii wengi zaidi.....

Sasa tatizo ni kwa serikali ya Tz kuitangaza hiyo picha...
Narudisha kwako mtoa hoja.....
 
Hata Tanzania ipo view ya Kilimanjaro na Tembo, tembelea maeneo ya West Kilimanjaro na Sinya......
 
Nimeshangaa mleta mada kutekwa akili na photoshopping. Picha za matangazo nyingi huchezewa. Dhana ya uchezewaji wa picha ni ya zamani. Unasahau habari za photo studios za zamani ukutani kuna picha na mandhari ya beach, minazi, migomba na wanyama kama simba, swala, pundamilia, tembo, chui nk wako umbali wa mita 2 au tatu na hawararuani??

Hata nimeshindwa kuelewa point yako hasa ni nini. Kuonesha ujinga???
 
View ya Twiga kwenye mlima Kilimanjaro ya wapi Tz au Kenya? , maana mtoa mada anadai kwa upande wa Tz ipo ya migomba only
 
Siyo lazima unielewe na wewe, kaa kimya.
Tembo wapo kibao maeneo ya west kilimanjaro Ndarakwi maneo ya karibu na mashamba ya Nafco,maeneoa ya Sinya ect kwahiyo picha hiyo inawezekana kabisa kuwa imepigiwa upande wa Tanzania.Siyo eneo lote la mlima kilimanjaro limezungukwa na migomba au wachaga maeneo mengine ni ya wamaasai na wameru na pia kwataharifa yako kuna hifadhi ndogo za wanya huko na block za uwindaji zikiwa chini ya WMA na ulinzi wa KDU na ujue mpaka wa kenya na tz siyo mlima kilimanjaro,mlima upo ndani ya tanzania kilometer kadhaa.Na wanya waliopo huko eneo hila siyo tembo peke yake wapo hata simba chui nyumbu twiga pundamilia mbuni ect Kama hiyo ni picha sinashaka kuhusu hiyo picha kupigwa upande wa tanzania maana madhari hayo yapo eneo lote la sinya mpaka mpakani mwa wilaya ya rombo na longido
 
Back
Top Bottom