Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 12,151
- 44,118
Dah!Duuu hii inafanana na mshikaji wangu in short kama vile umemuongelea yeye. Ana mahusiano ya muda mrefu na binti wa kisabato tena muimba kwaya halafu jamaa Mkkkt. Jamaa wakati wakutaka kuvuta jumla ikawa noma akaamua kumjaza mimba ili walegeze msimamo lkn wapi. Hadi sasa wanavutana sijui ni mpaka lini.
Wala usishangae, issue ni mapokeo ya kiiimani baina ya dhehebu moja na lingine. Kama kuna 'gap' kubwa la kiimani ni ngumu sana 'ku-comprimise' baadhi ya mambo.Yani hii ishu ya wasabato na madhehebu mengine kuoana ni changamoto sana.
Swali langu pia kwanini wakitaka kuoana kati ya RC, KKKT, TAG, EAGT au Pentekoste huwa hakuna shida.
Shida ni kwa wasabato tu?
Kuna vitu vingine ni vya kushangaza na hizi imani zetu yani, sasa ukifikiria vizuri hapo ni kama kituko fulaniDah!
Hiyo kali sana.
Yaani binti yuko tayari kufanya uzinzi ndani ya mwamvuli wa dini yake, lakini hataki kufunga ndoa nje ya mwamvuli wa dini yake.
Yaani binti anatuambia kuwa, yuko tayari kwa uzinzi lakini hayuko tayari kwa ndoa.
Sasa mwanaume unataka kuoa huyo mwanamke ili iweje? Wa nini hasa? Una wazimu?
Mkuu kuifunga hiyo ndoa sio kitu kirahisi hivyo kwa wasabato.Maana yangu ni kwamba, kila mmoja akishajua kuwa wao ni wakristo, wako chini ya uongozi wa YESU kristo, wanamwomba YESU kristo kwa shida zao, wataondoa tofauti ya madhehebu yao. Na kama kweli wanapendana, basi, watafunga ndoa ya kikristo. Sidhani taratibu za ndoa kwa madhehebu mengi ya kikristo zinatofautiana, kwa sababu tunatumia kitabu kimoja kutuongoza.
Mkuu wala sio vitu vya kushangaza ila ni kwa sababu watu watuzijui vyema imani zetu tunazoziamini, hivyo tunashangaa sana ikifika wakati zikigeuka kuwa kikwazo katika uhuru wa maamuzi yetu. Na imani zote zina hizo 'obstacles' katika uhuru wa mtu binafsi. To believe is to pay to price. No price no faith.Kuna vitu vingine ni vya kushangaza na hizi imani zetu yani, sasa ukifikiria vizuri hapo ni kama kituko fulani
Ila izi imani na dini inatakiwa watu wawe na mipaka nazo kwakweli mana namna hii dhehebu linapokuwa ni kikwazo cha kukosa mwenza, hatari sanaMkuu wala sio vitu vya kushangaza ila ni kwa sababu watu watuzijui vyema imani zetu tunazoziamini, hivyo tunashangaa sana ikifika wakati zikigeuka kuwa kikwazo katika uhuru wa maamuzi yetu. Na imani zote zina hizo 'obstacles' katika uhuru wa mtu binafsi. To believe is to pay to price. No price no faith.
Aisee hiyo mpya tena, kufunga ndoa mara mbili tena?Mambo mengine kuumiza vichwa bila sababu kwani tangu mwanzo mnapoanza ukiona mambo hayaendi si unaacha unaendelea na safari? Kuna dada mmoja alipata msabato yeye ni RC na dingi ni mkali balaa ikabidi wafunge huko Roman Catholic baada ya kwenda kwao mbona walifunga upya kabisa kama ndiyo wanachumbiana ni her ya nusu shari
Asante kwa ushauriWasabato wasumbufu sana atamsumbua mpaka kwenye watoto yan akimbie mbioo ndefu tena Ashukuru Mungu saiv mapema keshaona dalili
Asante kwa ushauri mzuri nduguWasabato tuwaache waolewe na wasabato wenzao. Ndio imani yao inavyo sisitiza siku zote. Na kamwe hawawezi kurahisisha hilo kisa tu kuwaridhisha hao wachumba wa madhehebu mawili tofauti. Na katika hili tusiwahukumu wasabato kwa msimamo wao bali tuwapongeze maana wamekubali kusimamia kile kile wanachokiamini.
Na katika maisha ya ndoa, kufunga ndoa(harusi) ni jambo moja dogo sana, issue ni kuweza kuishi na msabato kama wewe sio muumini wa kisabato. Ama wewe ni msabato uende kuishi na mtu ambaye sio msabato. Embu waza haya..
-Siku ya kuabudu.
-Vyakula.
-Vinywaji.
-Mavazi. Nk
Ila habari anakuonjeshaHuko kanisani kwao sijui wanalishwaga nini maana ukimtongoza atataka uache dhehebu lako, ufuate usabato wake.
MADE IN TARIME, RORYA , MAJITA and UPARENIKwa kukushauri tu, mwambie atafute mtu wa KKKT au dhehebu lolote la Kikristo, Ndoa na Msabato ni pasua kichwa, Msabato hachangamani na Mkristo yoyote, nimeshuhudia mateso makubwa ya ndoa a Msabato na Mkristo (Catholic, KKKT, Mlokole) Kuoa ni mara moja tu na ukikosea ni kila kitu
Na wasumbufu kweli ni afadhali akaacha mapema kuliko akaingia hivyo atajutiaWasabato wasumbufu sana atamsumbua mpaka kwenye watoto yan akimbie mbioo ndefu tena Ashukuru Mungu saiv mapema keshaona dalili
Ndiyo ilikuwa hivyo watu tulibaki na mshangaoAisee hiyo mpya tena, kufunga ndoa mara mbili tena?
Mkuu ngoja nikupe ufafanuzi mzuri hapa, halafu utaelewa vizuri Concept kati ya Ndoa na Imani.Ila izi imani na dini inatakiwa watu wawe na mipaka nazo kwakweli mana namna hii dhehebu linapokuwa ni kikwazo cha kukosa mwenza, hatari sana
Macomplicator sana kitu kidogo wanakikuzaUnajua ishu ni kwamba nahitaji kujua usumbufu wa wasabato ili nipate picha kamili?