Utata usioisha na aliyekuwa rafiki yangu!!!

Utata usioisha na aliyekuwa rafiki yangu!!!

Ni wivu tu. Jamaa anakuonea wivu na inamuuma mpaka leo. Kiufupi jamaa amegoma kuswallow his pride.
 
HIVI ENZI ZA CELTEL WANAFUNZI WALIKUA WANAMILIKI SIMU KWELI? HONGERA INAONESHA MLIKUA MNATOKA FAMILIA BORA.
ILA ILIKUA NI UCHONGANISHI MBAYA SANA KUONGEA NA MTU UKU HAJUI KAMA KUNA MTU WAKE WA KARIBU ANAMSIKILIZA, LAZIMA TU KUNGETOKEA UHASAMA KATI YENU.
Mkuu unakwama wapi? Wengine tulikuwa tunasoma na tulikuwa tayari tunamiliki simu, 1997 mi nilikuwa tayari namiliki simu mkuu
 
Haijanipunguzia furaha hata kidogo, nina maisha yangu nao wanayo ya kwao. Walikuwa wapuuzi sana sema yule kinara wao familia zetu zilikuwa na ukaribu kwa hiyo nilikuwa naogopa nikimsemea inaweza kuathiri hata mahusiano ya wazazi....juzi hapa nilimsimulia sister waliyokuwa wananifanyia aisee alishangaa sana akauliza kwa nini ulikuwa husemi??
Oooh! Mhm ni kuachilia as if halikuwa kutokea. Unajua hata ulivyolisemea kwamba hadi leo nikiwaona......... inaonyesha bado kuna hisia zenye chuki juu yao. Nilitaka tujifunze kusamehe mambo madogo na kuyaacha ili yatokeapo makubwa tunayaachia pia. Sabuni inatakatisha chombo kichafu sana na hata chenye vumbi tuu. Jaribu bana..maisha yenye huo utamaduni ni mataaaamu sana na huwezi ona mlima mbele yako.[emoji122][emoji122][emoji122]
 
Amen
Oooh! Mhm ni kuachilia as if halikuwa kutokea. Unajua hata ulivyolisemea kwamba hadi leo nikiwaona......... inaonyesha bado kuna hisia zenye chuki juu yao. Nilitaka tujifunze kusamehe mambo madogo na kuyaacha ili yatokeapo makubwa tunayaachia pia. Sabuni inatakatisha chombo kichafu sana na hata chenye vumbi tuu. Jaribu bana..maisha yenye huo utamaduni ni mataaaamu sana na huwezi ona mlima mbele yako.[emoji122][emoji122][emoji122]
 
Huu uzi wote maboya tu!
Kuanzia kwa mwenye demu
Wewe mwenyewe
Na demu wenu pia
 
Yaan demu wa rafiki yako mnachat na kuongea usiku kwani ungemblock ingekuaje kwa mfano?

Wewe ndio mwenye makosa na kwa maneno aliyoyaongea demu jamaa akayasikia ni wazi alihisi tiari ushambandua demu wake..
 
Usilazimishe urafiki, kama mtu hataki uwe rafiki yake achana nae
Wakuu habari za saizi!!
Poleni kwa majukumu kwa wenye nayo kama mimi, wengine hongereni kwa bata.

■ Kuna jambo limeishi miaka mingi sana {niseme mpaka sasa hivi}
● Nikiwa O'level mkoa mmoja hivi nilikuwa na rafiki yangu ambaye tulishirikiana kwa masomo na pia tulikuwa tunaenda mishe mishe pamoja (ikiwemo kusakata kabumbu)
● Tulipofika kidato cha tatu rafiki yangu alipata rafiki wa kike (baadae wakawa wapenzi) na huyo binti alikuwa yupo shule jirani kabisa ya binafsi (private school)
● Kwenye hiyo shule ya binafsi kaka yangu alikuwa anafundisha na alikuwa ananichukua kwenda kufanya mitihani na majaribio ya kila wiki waliyokuwa wanafanya wanafunzi wao.
● Mimi nilikuwa na pen pal pale kama wawili hivi lakini wao walikuwa wapo kidato cha nne, kwa hiyo nikimaliza paper tunakutana japo dakika tano kwenye ofisi ya kaka yangu.
● Kuna siku rafiki yangu akaniambia ana mpenzi kwenye ile shule namimi nikamwambia pale nina marafiki wawili kwa hiyo akajiunga nae tukawa tunaenda kupiga paper pamoja kwa idhini ya bro.
● Siku ya kwanza akanitambulisha kwa shemeji tukasalimiana na nikawa nawahi kuonana na mabest zangu tupige stori kidogo.
● Juma tatu tukiwa shuleni rafiki yangu akaniambia ebana shemeji yako anataka namba yako ha simu....mi nikamwambia usimpe, jamaa akanambia itakuwa sio fresh na haileti picha nzuri nisipompa namba yako bana maana anajua sisi ni marafiki.
● Tukazozana pale lakini jamaa akamtumia demu wake namba hangu ya celtel, sijui kwa nini sikutaka ampe namba ila tu nilikuwa naona sio ishu.
※ Usiku nikiwa najisomea sms zikaingia mbili, namba ngeni...za salamu na kunilaumu kwamba kwa nini sikupenda nitoe namba kwake (nikajua tu huyu ni shemeji)
※ Nikamtumia sms kuwa mi huwa sikai sana na simu na nawasiliana mara chache sana na watu muhimu kwa sababu simu zinapoteza mda sana wa kusoma.
※ Nikajibiwa acha ushamba shem...mi napenda tuwasiliane (kichwani nikasema mmmh huyu badala awasiliane na mtu wake....) tunataka kupotezeana mda.
♢ Kuanzia siku hiyo nikawa nakuta sms na missed call kibao nika notice hata maneno anayotumia yamebadilika amekuwa kama amenizoea sana. Mfano alianza kuniita (mume pacha) badala ya shem...akini keep bize mda mwingi kuchati na kuongea usiku.
♢ Siku moja rafiki yangu akanilalamikia kwa kusema [ Asee shem wako siku hizi yupo bize sana hata mawasiliano hafifu ] nikastuka nikamwambia sio kweli, hayupo bize yulee.
♢ Jamaa akakazia kana kwamba ana uhakika...mi nikamwambia ngoja tuchunguze kama kweli yupo bize..akasema powa.
♢ Usiku akanitafta swali la kwanza nikamuuliza "UNAWASILIANA NA JAMAA YAKO?" akajibu ndio nimetoka kuwasiliana nae mda si mrefu kama dakika 5 tu.
● Nikaona hapaaa kuna namna nikamwambia subiri kidogo nitakupigia akakata simu. Nikampigia rafiki yangu nikamuuliza akasema hajaongea nae ana siku 5 ....nikamwambia ukweli kuwa binti anaongopa awe makinj nae.
● Jamaa akanipa wazo tumpigie halafu tuweke conference call amskie....nikampigie na yule binti akapokea mi chap nikaunganisha tukawa wote online bila ya binti kujua.
● Sasa bahati mbaya akaniita jina lileee..."nambie mume pachaa" nikamwambia kwa nini unaniita hivo na sio shem...akacheka kisha akasema ni sawa tu yote majina.
● Nikamuuliza kwa nini unadanganya umewasiliana na jamaa kumbe hujawasiana nae??? Mi nimempigia ameniambia siku 5 hujawasiliana nae kwa nini?!?!
■ " asalaaaaale...alichojibu...eti achana na yule mshamba unajua shem mi nakufagilia wewe yaani una mapigo mazuri upo cool yaani kiufupi natamani nipate nafasi ya kuwa wako"
■ Jamaa uvumilivu ukamshinda akaita jina la binti weee lily...yaani unanizungukaa ( yule binti akakata simu)
■ Nikamwambia jamaa umejionea huyu dem sio atatugombanisha bure...JAMAA KWA SAUTI YA UNYOOONGEÈE AKANIAMBIA , MAN WE MCHUKUE TU.
♡ Baada ya pale niliuwa mawasiliano na yule binti na kumwambia aachane na sisi tena hata zile sms jamaa aliziona kwenye simu yangu kesho yake asubuhi.
■ Jamaa nikamwambia yule binti ni kigeugeu akija mtu anabeba ...jamaa hakujibu chochote. ..kuanzia hapo mawasiliano baina yangu na Rafiki yangu yakaanza kupungua na akawa akinikuta sehemu anaweza akapita bila kunisemesha.
■ Ile kitu iliniuma sana ila kuna baadhi ya washikaji pale class waliusoma mchezo wakaniuliza mi sikuwajibu pale pale...nikasubiri tuwe wote na jamaa ndio tuongee pamoja.
■ Mda wa kuondoka shule jamaa tukamuona nikamwita hakuitika....kuna jamaa akamuendea na kumlazimisha aje...mi nikasimulia kila kitu naye yupo pale ...washikaji wakamkanya asivunje urafiki kisa manzi asiejielewa.
■ Jamaa akaondoka bila kusema kitu, ila mpaka tunamaliza shule jamaa hakutaka hata kushea group la discussion mi nikasema poa tu maana sina nilichokosea.
■ JAMAA ALIKAZA MPAKA LEO HII HATA KWENYE GROUP LA WASAP LA WALIOMALIZA SHULE MWAKA WETU HUWA HAZIIVI.
□ WATU WAMEMCHANA SANA ILA HAJABADILIKA.
□ JE, HUU NI UUNGWANA?! (MAANA KUNA LEO NA KESHO UKITAZAMA KWA UMBALI ZAIDI)
 
Kwani urafiki lazima? Mbona unateseka na vitu vya kishamba na wakati ushajua huyo siyo rafiki. Wew mwenyew ulishakosea kuvuruga mahusiano yao ukihisi utaonekana mwema, mwenzio kakuona snitch tu. Ndio ujifunze mahusiano ya watu hayaingiliwi hata uone nini, m'ume kifua bwn! .. Pambama na maisha yako
 
Kwani urafiki lazima? Mbona unateseka na vitu vya kishamba na wakati ushajua huyo siyo rafiki. Wew mwenyew ulishakosea kuvuruga mahusiano yao ukihisi utaonekana mwema, mwenzio kakuona snitch tu. Ndio ujifunze mahusiano ya watu hayaingiliwi hata uone nini, m'ume kifua bwn! .. Pambama na maisha yako

Kwa hiyo ulitaka mtoa mada amgegede huyo demu wa rafiki yake Mis powers
 
Huyo jamaa kweli ni mshamba. Sasa ukweli wote anaujua. Anakuchukia kwa sababu ya mpuuzi mmoja tu.

Mimi rafiki yangu kwangu ni kama ndugu. Huwezi vunja undugu kwa sababu ya mtu mwingine mliyekutana juu kwaju.
Exactly na hicho cha kuthamini urafiki kuliko mtu wa kupita ndicho nilichofanya.
 
Muite huyo rafiki yako na umwambie kuwa ulifanya vile kwakuwa unampenda na hukupenda kumzunguka hivyo kama amekukasirikia hafanyi fair. Then mwambie we uko peace tu! [emoji106][emoji106][emoji106]
Nimekupata mkuu
 
Kipindi hiko huduma iliyokuepo ni ku divert kublock sidhani kama ilikuepo.
Sikuona sababu ya kumpoyeza jamaa ila hakunielewa (au egoism ilimzidi)
Yaan demu wa rafiki yako mnachat na kuongea usiku kwani ungemblock ingekuaje kwa mfano?

Wewe ndio mwenye makosa na kwa maneno aliyoyaongea demu jamaa akayasikia ni wazi alihisi tiari ushambandua demu wake..
 
Jamaa mleta uzi una tabia za kike..

Take it from me..
 
Back
Top Bottom