Utata usioisha na aliyekuwa rafiki yangu!!!

livewise1

JF-Expert Member
May 25, 2019
837
952
Wakuu habari za saizi!!
Poleni kwa majukumu kwa wenye nayo kama mimi, wengine hongereni kwa bata.

■ Kuna jambo limeishi miaka mingi sana {niseme mpaka sasa hivi}
● Nikiwa O'level mkoa mmoja hivi nilikuwa na rafiki yangu ambaye tulishirikiana kwa masomo na pia tulikuwa tunaenda mishe mishe pamoja (ikiwemo kusakata kabumbu)
● Tulipofika kidato cha tatu rafiki yangu alipata rafiki wa kike (baadae wakawa wapenzi) na huyo binti alikuwa yupo shule jirani kabisa ya binafsi (private school)
● Kwenye hiyo shule ya binafsi kaka yangu alikuwa anafundisha na alikuwa ananichukua kwenda kufanya mitihani na majaribio ya kila wiki waliyokuwa wanafanya wanafunzi wao.
● Mimi nilikuwa na pen pal pale kama wawili hivi lakini wao walikuwa wapo kidato cha nne, kwa hiyo nikimaliza paper tunakutana japo dakika tano kwenye ofisi ya kaka yangu.
● Kuna siku rafiki yangu akaniambia ana mpenzi kwenye ile shule namimi nikamwambia pale nina marafiki wawili kwa hiyo akajiunga nae tukawa tunaenda kupiga paper pamoja kwa idhini ya bro.
● Siku ya kwanza akanitambulisha kwa shemeji tukasalimiana na nikawa nawahi kuonana na mabest zangu tupige stori kidogo.
● Juma tatu tukiwa shuleni rafiki yangu akaniambia ebana shemeji yako anataka namba yako ha simu....mi nikamwambia usimpe, jamaa akanambia itakuwa sio fresh na haileti picha nzuri nisipompa namba yako bana maana anajua sisi ni marafiki.
● Tukazozana pale lakini jamaa akamtumia demu wake namba hangu ya celtel, sijui kwa nini sikutaka ampe namba ila tu nilikuwa naona sio ishu.
※ Usiku nikiwa najisomea sms zikaingia mbili, namba ngeni...za salamu na kunilaumu kwamba kwa nini sikupenda nitoe namba kwake (nikajua tu huyu ni shemeji)
※ Nikamtumia sms kuwa mi huwa sikai sana na simu na nawasiliana mara chache sana na watu muhimu kwa sababu simu zinapoteza mda sana wa kusoma.
※ Nikajibiwa acha ushamba shem...mi napenda tuwasiliane (kichwani nikasema mmmh huyu badala awasiliane na mtu wake....) tunataka kupotezeana mda.
♢ Kuanzia siku hiyo nikawa nakuta sms na missed call kibao nika notice hata maneno anayotumia yamebadilika amekuwa kama amenizoea sana. Mfano alianza kuniita (mume pacha) badala ya shem...akini keep bize mda mwingi kuchati na kuongea usiku.
♢ Siku moja rafiki yangu akanilalamikia kwa kusema [ Asee shem wako siku hizi yupo bize sana hata mawasiliano hafifu ] nikastuka nikamwambia sio kweli, hayupo bize yulee.
♢ Jamaa akakazia kana kwamba ana uhakika...mi nikamwambia ngoja tuchunguze kama kweli yupo bize..akasema powa.
♢ Usiku akanitafta swali la kwanza nikamuuliza "UNAWASILIANA NA JAMAA YAKO?" akajibu ndio nimetoka kuwasiliana nae mda si mrefu kama dakika 5 tu.
● Nikaona hapaaa kuna namna nikamwambia subiri kidogo nitakupigia akakata simu. Nikampigia rafiki yangu nikamuuliza akasema hajaongea nae ana siku 5 ....nikamwambia ukweli kuwa binti anaongopa awe makinj nae.
● Jamaa akanipa wazo tumpigie halafu tuweke conference call amskie....nikampigie na yule binti akapokea mi chap nikaunganisha tukawa wote online bila ya binti kujua.
● Sasa bahati mbaya akaniita jina lileee..."nambie mume pachaa" nikamwambia kwa nini unaniita hivo na sio shem...akacheka kisha akasema ni sawa tu yote majina.
● Nikamuuliza kwa nini unadanganya umewasiliana na jamaa kumbe hujawasiana nae??? Mi nimempigia ameniambia siku 5 hujawasiliana nae kwa nini?!?!
■ " asalaaaaale...alichojibu...eti achana na yule mshamba unajua shem mi nakufagilia wewe yaani una mapigo mazuri upo cool yaani kiufupi natamani nipate nafasi ya kuwa wako"
■ Jamaa uvumilivu ukamshinda akaita jina la binti weee lily...yaani unanizungukaa ( yule binti akakata simu)
■ Nikamwambia jamaa umejionea huyu dem sio atatugombanisha bure...JAMAA KWA SAUTI YA UNYOOONGEÈE AKANIAMBIA , MAN WE MCHUKUE TU.
♡ Baada ya pale niliuwa mawasiliano na yule binti na kumwambia aachane na sisi tena hata zile sms jamaa aliziona kwenye simu yangu kesho yake asubuhi.
■ Jamaa nikamwambia yule binti ni kigeugeu akija mtu anabeba ...jamaa hakujibu chochote. ..kuanzia hapo mawasiliano baina yangu na Rafiki yangu yakaanza kupungua na akawa akinikuta sehemu anaweza akapita bila kunisemesha.
■ Ile kitu iliniuma sana ila kuna baadhi ya washikaji pale class waliusoma mchezo wakaniuliza mi sikuwajibu pale pale...nikasubiri tuwe wote na jamaa ndio tuongee pamoja.
■ Mda wa kuondoka shule jamaa tukamuona nikamwita hakuitika....kuna jamaa akamuendea na kumlazimisha aje...mi nikasimulia kila kitu naye yupo pale ...washikaji wakamkanya asivunje urafiki kisa manzi asiejielewa.
■ Jamaa akaondoka bila kusema kitu, ila mpaka tunamaliza shule jamaa hakutaka hata kushea group la discussion mi nikasema poa tu maana sina nilichokosea.
■ JAMAA ALIKAZA MPAKA LEO HII HATA KWENYE GROUP LA WASAP LA WALIOMALIZA SHULE MWAKA WETU HUWA HAZIIVI.
□ WATU WAMEMCHANA SANA ILA HAJABADILIKA.
□ JE, HUU NI UUNGWANA?! (MAANA KUNA LEO NA KESHO UKITAZAMA KWA UMBALI ZAIDI)
 
Si ulishaambiwa jamaa yako mshamba? Chukulia poa tu. Cha muhimu kaa kwenye msimamo wako, hataki achana nae. Angekuwa mwelewa angeomba ushauri namna ya kudumisha mahusiano na hilo zezeta lake au kutafuta mwingine.
Pole mkuu.
 
Kabisa mkuu

Unadhani nisingemwambia mwisho wake ingekuwaje?!
Kwa mtu yeyote anaejua asingevumilia kuona rafiki yake anapata zahma hiyo. After all sikuwa natafta credit ila nilimuonesha anapopotelea.
Jifunze kubalance shobo, sasa ilikuaje umwambie mambo mnayoongea na demu wake?
 
Sio sifa ni ujinga.
Huo ndo ushujaaa...!! Lakini kama ungekuwa na Hekima ungeacha kuwasiliana na huyo demu tu...usingejibu txt wala call zake hukuwa na haja ya kumuonesha jamaa kuwa demu anakutaka..!! Upuuzi uliofanya aliwahi fanya rafiki yangu nae waliishia kutokuongea na jamaa mpaka keshoo...
 
Write your reply... Hata .ingekua mimi ningekukazia maana wewe ni mshamba, hata huyo dem amekuona boya sana maana wewe ndio mgombanishi.
Naunga mkono hoja...
Hawa jamaa wote washamba ndio maana wamemshindwa huyo demu wote wamemkosa na wameishia kugombana wenyew kwa wenyew...
Mtoa post sasa hapo umeepusha nn? We ungejipigia zako kimya kmya uzwazwa wako umekuponza
 
Back
Top Bottom