Utata usioisha na aliyekuwa rafiki yangu!!!

Utata usioisha na aliyekuwa rafiki yangu!!!

Sawa mkuu
Apo jamaa ako anaona aibu ya kuambiwa mshamba afu uyo demu anataka kuwa na ww.In short lazima ajiskie vibaya,kutokukubalika nalo ni janga ndugu.Tena linaleta mawazo hasa ukijichunguza mi nikoje mpaka niambiwe mshamba?.wewe umemzidi nn hasa mpaka manzi akukubali?. Mfano huo ni sawa na rafiki yako kafeli mtihani ww umetaulu lazima urafiki uishe coz anaona mtihani umemtenda na ww umekupendelea.Jaribu kusahau ya urafiki coz nae saizi ana mitazamo mingine na maisha yake akili ikimkaa vizuri atakukumbuka naimani
 
Mmmh nyie wote niwa shamba
naijatwittersavages-20190529-0002.jpeg
 
Hii mada imenifanya nikumbuke mbali sana Haya mambo yamenitokea sana ni zaidi ya mara tatu Mleta madaa umejaribu kujisafisha ili uwonekane perfect kuna kosa ulifanya ila ngumu mtu kuona ushauri wang acha mazoea na mademu za watu shikamoo maraha inatosha full stop
 
Nami yalinikuta haya. Jamaa yangu alikuwa na demu wake,demu akitaka kumuona jamaa lazima apitie kwangu. Wakati dem anamsubiri jamaa tunaendelea kupiga nae stori za hapa pale. Hapa tunapopigia stori sio chumbani ni kazini kwangu. Hivyo sii pahali pa kificho. Baadae jamaa alinimind nataka kumpindua. Nilijaribu kumwelewesha basi dem aje straight hapo ofisini kwenu hataki,anang'ang'ana apitie hapa kwangu. Niliona isiwe nongwa,kama natuhumiwa kwa jambo ambalo sijafanya,ngoja nifanye kweli. Kama ni kuwa mbaya basi iwe mbaya mazima. Nilipita na yule dem na urafiki ukaisha permanently.

Sipendi ujinga mimi.
 
Mazoea alileta yeye bro...siku zote mi nilikuwa simpi chance.
 
Hahaha...kweli hupendagi ujinga...ila pia inaonekana haupo nae tena huyo dem na rafiki yako amekuwa adui yako.
Hataari sana.

Siko nae tena,hata jamaa hayuko nae tena. Yalikuwa mambo ya ujana tu. Ila jamaa tukionana tunasalimiana fresh ila ule ukaribu kama zamani ulikoma. Mie nilishaoa nina mke na watoto. Jamaa nae alioa lakini walishindwana na mkewe wakaachana. Na hajaoa tena.
Hahaha...kweli hupendagi ujinga...ila pia inaonekana haupo nae tena huyo dem na rafiki yako amekuwa adui yako.
Hataari sana.
 
Sasa akiamua kuja kulipa kisasi utamlaumu?!? Kwa mama watoto.
Siko nae tena,hata jamaa hayuko nae tena. Yalikuwa mambo ya ujana tu. Ila jamaa tukionana tunasalimiana fresh ila ule ukaribu kama zamani ulikoma. Mie nilishaoa nina mke na watoto. Jamaa nae alioa lakini walishindwana na mkewe wakaachana. Na hajaoa tena.
 
Ndio kuna leo na kesho. Sasa kama leo na kesho zipo kuna tatzo gani?
 
Mazoea alileta yeye bro...siku zote mi nilikuwa simpi chance.
Mleta mada ni mshamba kosa lako ni majigambo majivuno ulio kuwa ukimwelezea rafiki yako kuhusu demu wake narudia tena mleta madaa ni mshamba unashindwaje kumkwepa mtoto wa kike narudia tena acha mazoea na mademu za watu
 
Sawa mkuu.

Wakuu habari za saizi!!
Poleni kwa majukumu kwa wenye nayo kama mimi, wengine hongereni kwa bata.

■ Kuna jambo limeishi miaka mingi sana {niseme mpaka sasa hivi}
● Nikiwa O'level mkoa mmoja hivi nilikuwa na rafiki yangu ambaye tulishirikiana kwa masomo na pia tulikuwa tunaenda mishe mishe pamoja (ikiwemo kusakata kabumbu)
● Tulipofika kidato cha tatu rafiki yangu alipata rafiki wa kike (baadae wakawa wapenzi) na huyo binti alikuwa yupo shule jirani kabisa ya binafsi (private school)
● Kwenye hiyo shule ya binafsi kaka yangu alikuwa anafundisha na alikuwa ananichukua kwenda kufanya mitihani na majaribio ya kila wiki waliyokuwa wanafanya wanafunzi wao.
● Mimi nilikuwa na pen pal pale kama wawili hivi lakini wao walikuwa wapo kidato cha nne, kwa hiyo nikimaliza paper tunakutana japo dakika tano kwenye ofisi ya kaka yangu.
● Kuna siku rafiki yangu akaniambia ana mpenzi kwenye ile shule namimi nikamwambia pale nina marafiki wawili kwa hiyo akajiunga nae tukawa tunaenda kupiga paper pamoja kwa idhini ya bro.
● Siku ya kwanza akanitambulisha kwa shemeji tukasalimiana na nikawa nawahi kuonana na mabest zangu tupige stori kidogo.
● Juma tatu tukiwa shuleni rafiki yangu akaniambia ebana shemeji yako anataka namba yako ha simu....mi nikamwambia usimpe, jamaa akanambia itakuwa sio fresh na haileti picha nzuri nisipompa namba yako bana maana anajua sisi ni marafiki.
● Tukazozana pale lakini jamaa akamtumia demu wake namba hangu ya celtel, sijui kwa nini sikutaka ampe namba ila tu nilikuwa naona sio ishu.
※ Usiku nikiwa najisomea sms zikaingia mbili, namba ngeni...za salamu na kunilaumu kwamba kwa nini sikupenda nitoe namba kwake (nikajua tu huyu ni shemeji)
※ Nikamtumia sms kuwa mi huwa sikai sana na simu na nawasiliana mara chache sana na watu muhimu kwa sababu simu zinapoteza mda sana wa kusoma.
※ Nikajibiwa acha ushamba shem...mi napenda tuwasiliane (kichwani nikasema mmmh huyu badala awasiliane na mtu wake....) tunataka kupotezeana mda.
♢ Kuanzia siku hiyo nikawa nakuta sms na missed call kibao nika notice hata maneno anayotumia yamebadilika amekuwa kama amenizoea sana. Mfano alianza kuniita (mume pacha) badala ya shem...akini keep bize mda mwingi kuchati na kuongea usiku.
♢ Siku moja rafiki yangu akanilalamikia kwa kusema [ Asee shem wako siku hizi yupo bize sana hata mawasiliano hafifu ] nikastuka nikamwambia sio kweli, hayupo bize yulee.
♢ Jamaa akakazia kana kwamba ana uhakika...mi nikamwambia ngoja tuchunguze kama kweli yupo bize..akasema powa.
♢ Usiku akanitafta swali la kwanza nikamuuliza "UNAWASILIANA NA JAMAA YAKO?" akajibu ndio nimetoka kuwasiliana nae mda si mrefu kama dakika 5 tu.
● Nikaona hapaaa kuna namna nikamwambia subiri kidogo nitakupigia akakata simu. Nikampigia rafiki yangu nikamuuliza akasema hajaongea nae ana siku 5 ....nikamwambia ukweli kuwa binti anaongopa awe makinj nae.
● Jamaa akanipa wazo tumpigie halafu tuweke conference call amskie....nikampigie na yule binti akapokea mi chap nikaunganisha tukawa wote online bila ya binti kujua.
● Sasa bahati mbaya akaniita jina lileee..."nambie mume pachaa" nikamwambia kwa nini unaniita hivo na sio shem...akacheka kisha akasema ni sawa tu yote majina.
● Nikamuuliza kwa nini unadanganya umewasiliana na jamaa kumbe hujawasiana nae??? Mi nimempigia ameniambia siku 5 hujawasiliana nae kwa nini?!?!
■ " asalaaaaale...alichojibu...eti achana na yule mshamba unajua shem mi nakufagilia wewe yaani una mapigo mazuri upo cool yaani kiufupi natamani nipate nafasi ya kuwa wako"
■ Jamaa uvumilivu ukamshinda akaita jina la binti weee lily...yaani unanizungukaa ( yule binti akakata simu)
■ Nikamwambia jamaa umejionea huyu dem sio atatugombanisha bure...JAMAA KWA SAUTI YA UNYOOONGEÈE AKANIAMBIA , MAN WE MCHUKUE TU.
♡ Baada ya pale niliuwa mawasiliano na yule binti na kumwambia aachane na sisi tena hata zile sms jamaa aliziona kwenye simu yangu kesho yake asubuhi.
■ Jamaa nikamwambia yule binti ni kigeugeu akija mtu anabeba ...jamaa hakujibu chochote. ..kuanzia hapo mawasiliano baina yangu na Rafiki yangu yakaanza kupungua na akawa akinikuta sehemu anaweza akapita bila kunisemesha.
■ Ile kitu iliniuma sana ila kuna baadhi ya washikaji pale class waliusoma mchezo wakaniuliza mi sikuwajibu pale pale...nikasubiri tuwe wote na jamaa ndio tuongee pamoja.
■ Mda wa kuondoka shule jamaa tukamuona nikamwita hakuitika....kuna jamaa akamuendea na kumlazimisha aje...mi nikasimulia kila kitu naye yupo pale ...washikaji wakamkanya asivunje urafiki kisa manzi asiejielewa.
■ Jamaa akaondoka bila kusema kitu, ila mpaka tunamaliza shule jamaa hakutaka hata kushea group la discussion mi nikasema poa tu maana sina nilichokosea.
■ JAMAA ALIKAZA MPAKA LEO HII HATA KWENYE GROUP LA WASAP LA WALIOMALIZA SHULE MWAKA WETU HUWA HAZIIVI.
□ WATU WAMEMCHANA SANA ILA HAJABADILIKA.
□ JE, HUU NI UUNGWANA?! (MAANA KUNA LEO NA KESHO UKITAZAMA KWA UMBALI ZAIDI)
Kiukweli hiyo issue uliihandle kishamba sana. Unamshtakiaje mwanamke tena kishambenga kwa conference call??? Unajua kabisa hapo hamna ndoa ni mapenzi ya utoto. Ulishindwaje kumchunia huyo binti had achoke kama hukumtaka?
All the time mambo ya mapenzi huwaga ni ya kijinga sana. Ukiona shida na haitamdhuru rafiki yako chuna na kaa mbali.
Nakushauri hivi, hata ukijatakwa na shemeji mke wa ndugu yako. Kaa mbali na usimwambie yeyote. Utasababisha shida sana.
 
Of course nimependa huyo jamaa msimamo wake hata ningekuwa mimi ningekupigia ngumu kali mzee ungeshangaa maana huwo ni ufala

"MIMI HUYO"
 
Back
Top Bottom