Utata, upotoshaji na ukweli unaouma kuhusu 'The Da Vinci code'

Labda mkuu uweke wazi katika injili mbili ipi imetofautiana na nyingine? Je zote zilishushwa nyakati moja (kwa kila dini). Na kama sivyo una maoni gani
INJILLI halisi ni ile ambayo haikuonesha maisha ya NABII ISSA(YESU) injili ili simama katika kuelezea mambo yaliokuwepo kabla ya NABII ISSA na si baada yake na hii INJILI ndiyo inayofanana kwa kiasi kikubwa na AGANO LA KALE na siyo jipya....kwahiyo BIBLIA sio INJILI halisi kutokana iliandikwa na mwanadamu moja kwa moja na sio kutokana na mtiririko ambao utaonesha kuwa maneno yale ama maandiko yale ni ya mwenyezi mungu na hii inashahidiliwa kutokana na AGANO JIPYA kuwa na INJILI NYINGI badala ya kuwa na ile injili moja ambayo ndiyo iliyoshushwa na mwenyezi mungu na hii inaoneshwa moja kwa moja kwa kuwepo kwa injili kama INJILI YA MARKO,PAULO,na nyinginezo na kuonesha kuwa AGANO JIPYA liliandikwa na mwanadamu na sio maneno ya mungu..matendo ya NABII ISSA yakaja kuelezewa katika kitabu kilichofuata ambacho ndicho cha ummat wa mwisho ambacho ni QURAN na kikashushwa katika ummat wa NABII MUHAMMAD na hii ni moja wapo mwa sababu zinazo onesha kuwa QURAN imekusanya vitabu vyote mfano MAISHA YA NABII ISSA,MAISHA YA NABII MUSSA,IBRAHIMU,NUHU,DAUDI,YAQQUUB, na kadhalika ambayo yote kwa ujumla yalioneshwa katika vitabu vilivyopita
 
yote hayo niCRAP
vitabu vya Biblia (Agano la Kale Agano Jipya zaidi ya vitabu 66 mpaka 73) viliandikwa na binadamu wa kawaida kama Musa wa Misri huko nyikani na hata vitabu vya Dr Luka na wengine walikuja fia Ethiopia
Hivi vitabu ni tofauti na Quran iliyoshushwa tena ni baada ya Biblia kuandikwa na kuhifadhiwa na zaidi ilikuwa Copy & Paste katika simulizi
 
Qurani imeshushwa?? Imeshushwa kutoka wapi?

Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Muu na mimi nimekaririshwa tu vivyo hivyo kuwa ilishushwa hakuna Mwandishi, na nina hakika vitabu wa kwanza vya Biblia viliandikwa na Mose (Musa) akiwa huko Nyikani
matendo ya NABII ISSA yakaja kuelezewa katika kitabu kilichofuata ambacho ndicho cha ummat wa mwisho ambacho ni QURAN na kikashushwa katika ummat wa NABII MUHAMMAD
 
Huu upuuzi niliusoma zamani sana, kwenye makala moja kwenye gazeti la RAI la wakati huo ikiandikwa na Padri Privatus Karugendo ambaye kanisa katoliki lilimtimua kwa sababu ya aina ya mafundisho yake.

Kwa kifupi, Don Brown alikuwa na nia na lengo la kuchafua kanisa katoliki na mafundisho yake. Askofu Methodeus Kilaini aliwahi kutolea ufafanuzi kuhusu hii kadhia katika kipindi kilichokuwa kikirushwa na Radio Tumaini kipindi kiitwacho Historia ya kanisa.

Da vinci michoro yake mingi ipo katika mafumbo. (Code) Don Brawn Amejaribu kuelezea zile nadharia ambazo wengi wamekuwa wakizisema. Ukweli ni kwamba kanisa katoliki ni moja kati ya Kanisa (taasisi?) Yenye historia kubwa na ambayo haiwenzi kuaribiawa na watu wa aina ya dan brawn na wafuasi wao kina Karugendo.

Eti Yesu alikuwa na Mahusiano na Maria Magdalena! Wanaenda mbali kwa kusema kwamba eti YESU alizaa watoto na Maria Magdalena.

Ajabu!
embu bisha kwa hoja.....
 
Nikiwa Nawaza na Kuwazua kuhusu Mambo kadha wa Kadha wazo linanijia Kichwani, wazo lenyewe ni Kuhusu Kitabu hiki tata, kinaitwa The Davinc'i Code!
Mawazo yanayonipelekea kukaa nyuma ya Keyboard ya Computer yangu kutaka kuelezea na Kujadili Kisa cha Kitabu hiki na nyinyi!!

Kitabu hiki ni riwaya, ni hadithi ya kubuni, lakini inaongelea vitu vya uhakika na ukweli. Mfano vikundi viwili vya siri katika Kanisa katoliki vinavyoongelewa katika riwaya hii vipo na wala si vya kubuni: The Priory of Sion, ni kikundi cha siri kilichoanzishwa mwaka wa 1099.

Kuna ushahidi wa kutosha kwamba watu maarufu kama Sir Isaac Newton, Botticelli, Victor Hugo na Leonardo da Vinci walikuwa wanachama wa kikundi hiki. Dan Brown, anaelezea vizuri muundo wa The Priory of Sion, kiasi kwamba mtu aliyejifunza historia ya kanisa, atakubaliana nami kwamba mtu huyu amefanya utafiti wa kina na wala si kazi ya kubuni tu.

Opus Dei,(Kazi ya Mungu), ni taasisi iliyoanzishwa mwaka 1928 na Padri wa Kihispanishi, Jose-Maria Escriva de Balaguer. Kuna ushahidi wa kutosha kwamba watu mashuhuri na wenye utata ni wanachama wa Opus Dei, kwa mfano iligunduliwa kwamba mawaziri na wakuu wengine waandamizi katika serikali ya Jenerali Franco,(anayejua huyu alikuwa ni kiongozi wa namna gani ni laima aweke alama ya kuuliza kwa kikundi hiki cha Opus Dei) aliyekuwa kiongozi wa Hispania, walikuwa wanachama waaminifu wa kikundi cha Opus Dei.

Miaka mitatu iliyopita, iligunduliwa kuwa Robert Hanssen, kachero wa Shirika la Upelelezi wa Jinai la Marekani (FBI) aliyeuzia siri za marekani kwa Urusi, alikuwa anahusiana na Opus Dei. Dan Brown, anaielezea vizuri Opus Dei, kiasi cha kutilia shaka kwamba labda na yeye alikuwa au ni mwanachama!.

Hivyo ingawa The Da Vinci Code, ni riwaya inaelekea imefanyiwa utafiti wa kina na imebeba ukweli mwingi wa kihistoria. Ukweli huu ni lazima utagusa imani ya wale waliokuwa katika giza kwa muda mrefu. Wale waliokuwa wanaamini kinyume cha Thomas, kugusa, kutafiti, kuhoji na kujadiliana. Na kwa upande wa Afrika, au niseme kabisa kwa upande wa Tanzania, kitabu hiki ni changamoto kubwa, na kimekuja wakati mbaya kabisa. Zamani ingetosha kukusanya vitabu kama hivi na kuvichoma moto au kuvipiga marufuku.
Leo hii haiwezekani, maana hata ukikichoma moto kitabu bado watu watakikuta kwenye mtandao na kukisoma. Watahoji na kutaka wapatiwe majibu ya kitaalamu yenye kufanyiwa utafiti.

Riwaya kama ya Dan Brown ya The Da Vinci Code, inawachochea watu kuanza kuchokonoa na kuhoji mambo mengi yenye utata. Maaskofu wetu na wanateolojia wamejiandaa vipi kukabiliana na changamoto kama hii ya The Da Vinci Code? Huu si wakati wa kuzuia kitu bila maelezo. Huu ni wakati wa kufanya utafiti, kujadiliana na kuelimishana. Ni wakati wa kujenga imani yenye mizizi katika jamii, imani inayotokana na watu wenyewe, kwa kuzingatia historia yao, mila zao na jinsi Mungu Mwenyewe anavyojifunua kwa watu wake aliowaumba na kuwapatia uwezo wenye mapungufu!

Mfano katika riwaya hii Dan Brown, anaelezea ukweli wa historia kwamba Injili nne tulizonazo kwenye Agano jipya zilipitishwa kwa kura kwenye mkutano wa Nicaea wa 325 AD ulioitishwa na kusimamiwa na Mfalme Constantine, ambaye alikuwa mpagani na aliendelea kuwa mpagani hadi mwisho wa maisha yake alipobatizwa akiwa mgonjwa kiasi cha kutokuwa na uwezo wa kukataa ubatizo. Yeye aliona faida ya kuutumia Ukristu kuupanua utawala wake. Aliutumia Ukristu kama chombo cha kumzidishia madaraka na nguvu ya kuzitawala himaya zake, hakuutumia Ukristu kuijenga imani yake na kuishi utu wema.

Injili zilikuwa nane, zilitupwa nne na kukubaliwa nne tu ambazo hazikuonyesha wazi uhusiano wa karibu sana kati ya Yesu na Maria Magdalena. Kati ya Injili zilizotupwa ni Injili ya Philip na ile aliyoiandika Maria Magdalena mwenyewe. Waliopata bahati ya kuzisoma injili hizi( Dan Brown, ni mmoja wao) zilizotupwa na hasa ile ya Philipo na Maria Magdalena, wanakili wasiwasi, mashaka na chuki iliyokuwepo kati ya mitume wengine wanaume na Maria Magdalena, walilalamika wazi kwamba Yesu, alimpenda Maria Magdalena zaidi kuliko alivyowapenda mitume wengine, Mtakatifu Petro, ndiye alilalamika sana juu ya upendo wa Yesu, kwa Maria Magdalena.

Hata na zile Injili zilizobaki kama ile ya John, jambo hili linajitokeza ingawa kufuatana na mabadiliko yaliyofanywa na Mkutano wa Nicaea, tunayasoma kwa mtazamo mwingine, lakini ukweli unabaki kwamba aliyekuwa akilalamikiwa ni Maria Magdalena, maana hakuna popote katika Injili tulizonazo inapoonyeshwa wazi kwamba Yesu, alikuwa na uhusiano wa karibu na mtume wa kiume zaidi ya mitume wengine. Soma mistari hii kwa macho ya Dan Brown, uone ukweli uliofichwa na Mkutano Nicaea:
“ Hapo Petro akageuka, akamwona yule mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda, anafuata.(Huyu ndiye ambaye wakati wa chakula cha jioni, alikaa karibu sana na Yesu na kumwuliza: Bwana, ni nani atakayekusaliti?) Yesu akamjibu Petro, ‘Kama nataka abaki mpaka nitakapokuja, yakuhusu nini? Wewe nifuate mimi’. ( Yohana 21:20-22).

Kufuatana na Injili ya Philipo na Maria Magdalena, ni kwamba Petro, hakuamini na kukubali kwamba Yesu, angeliliacha kanisa lake mikononi mwa mwanamke na kuwaacha wanaume. Hivyo Constantine, kwa kuita mkutano wa Nicaea na kuusimika mfumo dume katika kanisa, iliendana na mapenzi ya Mtakatifu Petro.

Mbali na kuingiza mfumo dume katika kanisa, Constantine, aliingiza mambo mengine mengine mengi ya kiupagani. Mfano siku ya Jumapili, ilikuwa ni siku ya kipagani ya kuliabudu Jua. Leo hii ndiyo siku inayoheshimika sana katika dini ya Kikristu! Yako mengine mengi anayoyataja Dan Brown, ambayo hayana kitu wala uhusiano na Yesu wa Nazareti, bali ni upagani aliouingiza Constantine.

Katika riwaya yake Dan Brown, anaelezea ukweli mwingine wa kihistoria usiokuwa na upinzani kwamba ni mkutano huo huo wa Nicaea, ulioamua juu ya Umungu wa Kristu. Kwamba Kristu, ni mwana wa Mugu, ni kitu kilichopigiwa kura na Maaskofu katika Mkutano Nicaea wakiongozwa na Constantine!

Kikundi cha The Priory of Sion, kinatunza siri ya Maria Magdalena. Kikundi hiki kinaamini kwamba Yesu Kristu, aliliacha kanisa mikononi mwa mwanamke na wala si kwa Petro. Kuna ushahidi wa kutosha kwamba kikundi hiki bado kinatunza masalia ya mwili wa Maria Magdalena na uzao wake. Kuna imani kwamba kuna watu wenye uhusiano wa damu na Yesu kwa kupitia kwa Maria Magdalena! Kikundi hiki kinailinda siri hii kwa gharama yote yote ile. Kanisa katoliki limekuwa likiitafuta siri hii kwa udi na uvumba ili kuhakikisha limeifuta kabisa na kuwa salama.

Riwaya ya Dan Brown, inaelezea mapambano kati ya Kanisa Katoliki na kikundi kinachoitunza siri ya Maria Magdalena. Haya ni mapambano ya watu walio tayari kufanya mauaji kwa kulilinda kanisa, wanamwaga damu, wanafanya mambo mabaya na baadaye wanapiga magoti na kusali. Wanajitesa kwa kujipiga mijeledi, kufunga chakula na kujifunga minyororo. Watu hawa wanaamini kwamba wanafanya Kazi ya Mungu yaani “Opus Dei”!

Young-Leonardo-Last-Supper-Canvas-Painting.jpg

Mchoro huu wa Mlo wa Mwisho (Last Supper) ndio Mchoro unaoleta utata Mkubwa!!

Je wewe unaamini nini na una Maoni gani??
andiko hili niriwaya, ni hadithi ya kubuni...!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Umeshasema kitabu hicho ni hadithi ya kutunga lkn inasehem yenye ukweli .yanini kujadili kitabu cha hadithi

Kitabu cha Mwanzo ni mambo ya kutunga yenye lengo la kueleza kwamba kila kitu kionekacho au kisichoonekana kimeumbwa na Mungu. Sasa inashangaza sana kwa maelezo ya jamaa, jambo la kutunga libadilike kutoka kuwa hadithi na kuwa ukweli na Uhalisia.
 
Kwenye The Da Vinc'i Code anachosema ni kua, kuna uwezekano wa Bwana Yesu alizaa na Maria Magdalena!!! na kwamba kizazi hicho kipo mpaka leo kikitunzwa kwa siri kubwa za kumwaga damu

1. Kwa hiyo ni damu ya nani ilimwagika ndio Dan Brown akapa hiyo Siri?

2. Na kama kuna damu ilimwagika na watu wakapata siri sasa inashindikanaje kumwagika nyingine ili hicho kizazi kijulikane.

4. Hicho kizazi kina watu wangapi kiasi kimefichwa na hakijulikani na kimefichwa wapi?

5. Hicho kizazi kinazaliana wao kwa wao tu,yaani ndugu kwa ndugu?

6.Hivi kwa maendeleo ya Sayansi na Tekinolojia tuliyo nayo,hata Satellites zimeshindwa kunasa na kuonyesha walipo hao watu?
 
Eti Yesu alikuwa na Mahusiano na Maria Magdalena! Wanaenda mbali kwa kusema kwamba eti YESU alizaa watoto na Maria Magdalena.

Pd. Titus Amigu amepata kukichambua Kitabu hicho. Anachosema ni kwamba jamaa alijaribu ni watu wangapi wana husuda, chuki na hasira na Kanisa Katoliki na ni mambo gani wangalipenda kuyasikia zaidi. Kwa kulifahamu hilo jamaa akaona atapiga pesa akitoka kihivyo.
 
maana mtu wa kwanza kumtabiria mtume MUHAMMAD utume wakati akiwa mdogo kabisa alikua ni PADRI BAHIRA

1. Huyo Padri Bahira alikuwa Wa Nchi gani,Shirika gani,Jimbo gani na alisemaje juu ya huo utabiri?

2. Ninyi ni wababaishaji na hamujui mkisemacho. Tabia zenu na mafundisho yenu juu ya utume wa Muhammad ni jambo ambalo hamna uhakika nalo na mumebakia kutapatapa tu. Mara museme Muhammad alitabiriwa na Nabii Musa katika Kitabu cha Kumbukumbu la Torati,Sura ya 18:18-20 kama inavyosomeka:

"18 Mimi nitawaondokeshea nabii miongoni mwa ndugu zao mfano wako wewe, nami nitatia maneno yangu kinywani mwake, naye atawaambia yote nitakayomwamuru.
19 Hata itakuwa, mtu asiyesikiliza maneno yangu atakayosema yule kwa jina langu, nitalitaka kwake.
20 Lakini nabii atakayenena neno kwa kujikinai kwa jina langu, ambalo sikumwagiza kulinena, au atakayenena katika jina la miungu mingine, nabii yule atakufa."

3. Na baada ya kutumia kifungu hicho cha Kumbukumbu la Torati na kubanwa kwa Ushahudi mkubwa Wa Kiteolojia, mkakimbilia kuongeza jambo jingine kwamba Yesu ndiye aliyemtabiria Muhammad juu ya ujio wake, pale alipowaambia Mitume wake kwamba baada ya yeye kuondoka angaliwaletea Msaidizi. Na kwamba huyo msaidizi badala ya kuwa ni Roho Mtakatifu basi ni Muhammad.

Sasa kwa ushahidi huu inaonekana wazi munatapa tapa tu kiasi kwamba "mkipigwa" hapa mnakimbilia kule mithili ya Nyani kutoka mti mmoja hadi mwingine.
 
shida inakuja hapa kwamba ni ngumu kuibadilisha mitazamo ya wakristo na wafia dini hiyo kutokana nakuwa hawapendi kuukubali ukweli biblia inamashaka mengi na inatia wasi wasi hata kwa wale waiaminiyo........iwaje kitabu kitakatifu kiwe na nakala mbili ya kale na ya zamani...kwahiyo inamaanisha mungu kwenye agano la kale aliikosea mpaka akaamua atoe NEW EDITION....kuna kitu huwa najaribu kulinganisha kati ya vitabu hivi viwili vikuu ambavyo vina watumiaji wengi yani QURAN na BIBLIA ambapo Quran imeweza beba mafundisho yake yote ndani ya kitabu kimoja ambapo mafundisho yake yanatafsiriwa kwa SUNNA[matendo ya mtume MUHAMMAD] na HADITHI za mtume ikiwa hadithi na sunna hizo zote hakuna zinazoongeza chumvi wala kupunguza bali kutafasiri kwa upana mafunzo yaliomo ndani ya QURAN ambapo BIBLIA kwa hapa imefeli kabisa kutokana na kuwa na BIBLIA nyingi mara hii ya WASABATO ile ya KKKT nk........jambo jingine ni lugha zinazotumika ndani ya vitabu hivyi viwili katika suala la ibada na hapa ndipo BIBLIA IMEFELI 100%.......pale muhubiri wa dini wa kikristo mfano anatokea china akija kuongoza ibada TANZANIA yeye atatumia KICHINA ambapo atahitaji mkalimani ili aweze kuyatafasiri maneno yake ili waumini waweze kuelewa ni nini cha kufanya WAKATI wafia dini ya UISLAMU wanatoka nchi mbalimbali duniani zikiwemo TANZANIZ,CHINA,JAPAN,USA nk wakielekea kwenye ibada MAKKA.....pale imamu atakayekuwa anaiongoza ibada hatahitaji mkalimani akisema 'ALLAH AKBAR' kila mtu ndani ya msikiti ule ataelewa ni nini cha kufanya ama nikipi kimeamrishwa bila kuhitaji mkalimani...na hii inaprove ya kwamba dini yauislamu ni ya ulimwengu mzima na sio mtu na mtu ama nchi na nchi na pia inaonesha UISLAMU kuwa ndiyo dini ya haki iliyotoka kwa mwenyezi Mungu jala jalali na sio ya kutungwa na mtu ndo maana haioneshi makosa katika utendaji wake.........UKRISTO UNAONESHA MAPUNGUFU MENGI!!!!!!
Hapa mbona hujajadili riwaya ya Da Vinci Code? Au hujaelewa?
 
Nikiwa Nawaza na Kuwazua kuhusu Mambo kadha wa Kadha wazo linanijia Kichwani, wazo lenyewe ni Kuhusu Kitabu hiki tata, kinaitwa The Davinc'i Code!
Mawazo yanayonipelekea kukaa nyuma ya Keyboard ya Computer yangu kutaka kuelezea na Kujadili Kisa cha Kitabu hiki na nyinyi!!

Kitabu hiki ni riwaya, ni hadithi ya kubuni, lakini inaongelea vitu vya uhakika na ukweli. Mfano vikundi viwili vya siri katika Kanisa katoliki vinavyoongelewa katika riwaya hii vipo na wala si vya kubuni: The Priory of Sion, ni kikundi cha siri kilichoanzishwa mwaka wa 1099.

Kuna ushahidi wa kutosha kwamba watu maarufu kama Sir Isaac Newton, Botticelli, Victor Hugo na Leonardo da Vinci walikuwa wanachama wa kikundi hiki. Dan Brown, anaelezea vizuri muundo wa The Priory of Sion, kiasi kwamba mtu aliyejifunza historia ya kanisa, atakubaliana nami kwamba mtu huyu amefanya utafiti wa kina na wala si kazi ya kubuni tu.

Opus Dei,(Kazi ya Mungu), ni taasisi iliyoanzishwa mwaka 1928 na Padri wa Kihispanishi, Jose-Maria Escriva de Balaguer. Kuna ushahidi wa kutosha kwamba watu mashuhuri na wenye utata ni wanachama wa Opus Dei, kwa mfano iligunduliwa kwamba mawaziri na wakuu wengine waandamizi katika serikali ya Jenerali Franco,(anayejua huyu alikuwa ni kiongozi wa namna gani ni laima aweke alama ya kuuliza kwa kikundi hiki cha Opus Dei) aliyekuwa kiongozi wa Hispania, walikuwa wanachama waaminifu wa kikundi cha Opus Dei.

Miaka mitatu iliyopita, iligunduliwa kuwa Robert Hanssen, kachero wa Shirika la Upelelezi wa Jinai la Marekani (FBI) aliyeuzia siri za marekani kwa Urusi, alikuwa anahusiana na Opus Dei. Dan Brown, anaielezea vizuri Opus Dei, kiasi cha kutilia shaka kwamba labda na yeye alikuwa au ni mwanachama!.

Hivyo ingawa The Da Vinci Code, ni riwaya inaelekea imefanyiwa utafiti wa kina na imebeba ukweli mwingi wa kihistoria. Ukweli huu ni lazima utagusa imani ya wale waliokuwa katika giza kwa muda mrefu. Wale waliokuwa wanaamini kinyume cha Thomas, kugusa, kutafiti, kuhoji na kujadiliana. Na kwa upande wa Afrika, au niseme kabisa kwa upande wa Tanzania, kitabu hiki ni changamoto kubwa, na kimekuja wakati mbaya kabisa. Zamani ingetosha kukusanya vitabu kama hivi na kuvichoma moto au kuvipiga marufuku.
Leo hii haiwezekani, maana hata ukikichoma moto kitabu bado watu watakikuta kwenye mtandao na kukisoma. Watahoji na kutaka wapatiwe majibu ya kitaalamu yenye kufanyiwa utafiti.

Riwaya kama ya Dan Brown ya The Da Vinci Code, inawachochea watu kuanza kuchokonoa na kuhoji mambo mengi yenye utata. Maaskofu wetu na wanateolojia wamejiandaa vipi kukabiliana na changamoto kama hii ya The Da Vinci Code? Huu si wakati wa kuzuia kitu bila maelezo. Huu ni wakati wa kufanya utafiti, kujadiliana na kuelimishana. Ni wakati wa kujenga imani yenye mizizi katika jamii, imani inayotokana na watu wenyewe, kwa kuzingatia historia yao, mila zao na jinsi Mungu Mwenyewe anavyojifunua kwa watu wake aliowaumba na kuwapatia uwezo wenye mapungufu!

Mfano katika riwaya hii Dan Brown, anaelezea ukweli wa historia kwamba Injili nne tulizonazo kwenye Agano jipya zilipitishwa kwa kura kwenye mkutano wa Nicaea wa 325 AD ulioitishwa na kusimamiwa na Mfalme Constantine, ambaye alikuwa mpagani na aliendelea kuwa mpagani hadi mwisho wa maisha yake alipobatizwa akiwa mgonjwa kiasi cha kutokuwa na uwezo wa kukataa ubatizo. Yeye aliona faida ya kuutumia Ukristu kuupanua utawala wake. Aliutumia Ukristu kama chombo cha kumzidishia madaraka na nguvu ya kuzitawala himaya zake, hakuutumia Ukristu kuijenga imani yake na kuishi utu wema.

Injili zilikuwa nane, zilitupwa nne na kukubaliwa nne tu ambazo hazikuonyesha wazi uhusiano wa karibu sana kati ya Yesu na Maria Magdalena. Kati ya Injili zilizotupwa ni Injili ya Philip na ile aliyoiandika Maria Magdalena mwenyewe. Waliopata bahati ya kuzisoma injili hizi( Dan Brown, ni mmoja wao) zilizotupwa na hasa ile ya Philipo na Maria Magdalena, wanakili wasiwasi, mashaka na chuki iliyokuwepo kati ya mitume wengine wanaume na Maria Magdalena, walilalamika wazi kwamba Yesu, alimpenda Maria Magdalena zaidi kuliko alivyowapenda mitume wengine, Mtakatifu Petro, ndiye alilalamika sana juu ya upendo wa Yesu, kwa Maria Magdalena.

Hata na zile Injili zilizobaki kama ile ya John, jambo hili linajitokeza ingawa kufuatana na mabadiliko yaliyofanywa na Mkutano wa Nicaea, tunayasoma kwa mtazamo mwingine, lakini ukweli unabaki kwamba aliyekuwa akilalamikiwa ni Maria Magdalena, maana hakuna popote katika Injili tulizonazo inapoonyeshwa wazi kwamba Yesu, alikuwa na uhusiano wa karibu na mtume wa kiume zaidi ya mitume wengine. Soma mistari hii kwa macho ya Dan Brown, uone ukweli uliofichwa na Mkutano Nicaea:
“ Hapo Petro akageuka, akamwona yule mwanafunzi ambaye Yesu alimpenda, anafuata.(Huyu ndiye ambaye wakati wa chakula cha jioni, alikaa karibu sana na Yesu na kumwuliza: Bwana, ni nani atakayekusaliti?) Yesu akamjibu Petro, ‘Kama nataka abaki mpaka nitakapokuja, yakuhusu nini? Wewe nifuate mimi’. ( Yohana 21:20-22).

Kufuatana na Injili ya Philipo na Maria Magdalena, ni kwamba Petro, hakuamini na kukubali kwamba Yesu, angeliliacha kanisa lake mikononi mwa mwanamke na kuwaacha wanaume. Hivyo Constantine, kwa kuita mkutano wa Nicaea na kuusimika mfumo dume katika kanisa, iliendana na mapenzi ya Mtakatifu Petro.

Mbali na kuingiza mfumo dume katika kanisa, Constantine, aliingiza mambo mengine mengine mengi ya kiupagani. Mfano siku ya Jumapili, ilikuwa ni siku ya kipagani ya kuliabudu Jua. Leo hii ndiyo siku inayoheshimika sana katika dini ya Kikristu! Yako mengine mengi anayoyataja Dan Brown, ambayo hayana kitu wala uhusiano na Yesu wa Nazareti, bali ni upagani aliouingiza Constantine.

Katika riwaya yake Dan Brown, anaelezea ukweli mwingine wa kihistoria usiokuwa na upinzani kwamba ni mkutano huo huo wa Nicaea, ulioamua juu ya Umungu wa Kristu. Kwamba Kristu, ni mwana wa Mugu, ni kitu kilichopigiwa kura na Maaskofu katika Mkutano Nicaea wakiongozwa na Constantine!

Kikundi cha The Priory of Sion, kinatunza siri ya Maria Magdalena. Kikundi hiki kinaamini kwamba Yesu Kristu, aliliacha kanisa mikononi mwa mwanamke na wala si kwa Petro. Kuna ushahidi wa kutosha kwamba kikundi hiki bado kinatunza masalia ya mwili wa Maria Magdalena na uzao wake. Kuna imani kwamba kuna watu wenye uhusiano wa damu na Yesu kwa kupitia kwa Maria Magdalena! Kikundi hiki kinailinda siri hii kwa gharama yote yote ile. Kanisa katoliki limekuwa likiitafuta siri hii kwa udi na uvumba ili kuhakikisha limeifuta kabisa na kuwa salama.

Riwaya ya Dan Brown, inaelezea mapambano kati ya Kanisa Katoliki na kikundi kinachoitunza siri ya Maria Magdalena. Haya ni mapambano ya watu walio tayari kufanya mauaji kwa kulilinda kanisa, wanamwaga damu, wanafanya mambo mabaya na baadaye wanapiga magoti na kusali. Wanajitesa kwa kujipiga mijeledi, kufunga chakula na kujifunga minyororo. Watu hawa wanaamini kwamba wanafanya Kazi ya Mungu yaani “Opus Dei”!

Young-Leonardo-Last-Supper-Canvas-Painting.jpg

Mchoro huu wa Mlo wa Mwisho (Last Supper) ndio Mchoro unaoleta utata Mkubwa!!

Je wewe unaamini nini na una Maoni gani??
Mtoa mada hicho Kitabu unachokizungumzia ni riwaya ya kubuni. Bila shaka kama wewe ni msomaji mzuri wa kazi za fasihi, hii siyo kazi ya kwanza yenye kugusa hisia za msomaji hadi kumfanya ahisi na kuamini kuwa anachokisoma ni ukweli mtupu usiopingika. Hii ndio sifa kuu ya kazi yoyote bora ya fasihi. Kama kazi ya fasihi haiwezi kuihamisha hadhira yake na kuiingiza katika maisha ya kufikirika ya kazi hiyo, basi ujue kazi hiyo imeshindwa na kamwe haiwezi kuwa na solo. Sasa sijui wewe unatakaje tukae hapa kuijadili kazi ya kubuni iliyoteka hisia zako na kukufanya uamini kuwa kila unachokisoma ni kweli tupu (facts) ambayo haipingiki kwa namna yoyote? Hapo mimi nitachangia jambo Mona tu. Mwandishi amefanikiwa kwa kiwango kikubwa kuiteka hadhira yake na kuifanya iishi katika riwaya hiyo. Yaani ukiisoma unajiona kuwa uko katika jamii hiyo ya riwaya lakini ukimaliza kusoma tu unajikuta ' haa kumbe niko hapa hapa nyumbani Buguruni kwa malapa?"Mwandishi akitunga riwaya iayoelezea jinsi wapelelezi wa usalama wa taifa wanavyopambana na majasusi wa kigeni jijini Dar , kama ilivyokuwa katika 'Kikosi cha Kisasi' na 'Njama' vya Elvis Musiba , haimsanishi kuwa ndivyo hali halisi ilivyo jijini Dar.
 
Kuna Habari kwamba huyu Dan Brown anashikishwa ukuta,,au kwa lugha ya mtaani anapakuliwa...Hii inatosha kudisqualify kila alichoandika hata kama kwa bahati mbaya kulikuwa na kuukaribia ukweli katika riwaya alizoandika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mapungufu ya ukristo hayawezi kuainishwa na watu wajinga ama wapumbaf..Na najiuliza huyu dan brown anasubiri nini asiukimbilie uislam unaopigiwa chapuo kuwa eti! dini ya kweli na ya haki..Sijui anasubiri nini!#

Back
Top Bottom