Utata kigogo UVCCM - akutwa amekufa hotelini Arusha

Utata kigogo UVCCM - akutwa amekufa hotelini Arusha

Mkuu sote tunaungana na
familia ya marehemu na ccm kuomboleza hiki kifo cha kutatanisha.
Vile vile hakuna binadamu aliyekamilika, ila kusema ni mwanamke bado ni
presumption tu, inawezekana ni kibiashara ama kisiasa ndani ya ccm
kutoana kafara.
Hapo kwenye Red, Marehemu kisiasa ana miaka 26. Lakini kiuhalisia Benson
Mollel hakosi miaka 40+

Hatumjui. Wekeni picha yake
 
Buriani Benson Mollel; nakulilia kwa jinsi binafsi nilivyopata kukufahamu!!!!!!!!
 
Poleni sana Ritz, Ze marcopolo na chama. Msiba mzito sana kwenu. Mungu amlaze mahali alipo mpangia.

Kweli nimeamini ukicheza ngoma ya washenzi unageuka mshenzi; hata wewe mtoto wa kiungwana unatoa kauli hafifu kama hii? Simfahamu wala sijawahi kumsikia marehemu lakini katika mazingira ya kibinadamu nawapa pole wafiwa na Mungu amlaze mahala pema peponi Amen! Nakukumbusha tu ndugu yangu Mohamedi Mtoi binadamu tunatembea na mauti "Qullu nafsi dhaikatul maut" usishangilie hatima mwenzako yako huijui au mwenzangu unajua hatima ya mauti yako?

Chama
Gongo la mboto DSM
cc Ritz
 
Last edited by a moderator:
Wakuu members wenzangu, mimi nimebahatika kabisa kuchunguza utata wa kifo cha BEN.

Taarifa ni kuwa marehemu pamoja na kuwa na umri mdogo (miaka 26) aligundulika kuwa alitumia viagra ma aliji-overdose. Ndio kisa cha kumpigia g/friend mwingine.
 
Kweli nimeamini ukicheza ngoma ya washenzi unageuka mshenzi; hata wewe mtoto wa kiungwana unatoa kauli hafifu kama hii? Simfahamu wala sijawahi kumsikia marehemu lakini katika mazingira ya kibinadamu nawapa pole wafiwa na Mungu amlaze mahala pema peponi Amen! Nakukumbusha tu ndugu yangu Mohamedi Mtoi binadamu tunatembea na mauti "Qullu nafsi dhaikatul maut" usishangilie hatima mwenzako yako huijui au mwenzangu unajua hatima ya mauti yako?

Chama
Gongo la mboto DSM
cc Ritz

Mkuu chama!

Kosa langu hapo ni lipi kaka?! Ushabiki unao uona nimeuonyesha kwenye kifo cha kiongozi wa UV-CCM ni upi? Kukupa pole kwa msiba mzito wewe na wana ccm wenzako?! Na kwa nini unitafsiri kuwa nimeweka ushabiki kwenye kifo ambacho ni faradhi ya kila mja?!

Umenishangaza sana mkuu. Anyway! Pole kama nimekukwaza kwa kukupa pole kwa kuondokewa na kiongozi wenu.
 
Last edited by a moderator:
hakika benson au ben kama wengi tulivyozoea kumwita licha ya kuwa meneja wangu mgodin pia alikuwa ni m2 mwnye kusikiliza na kutatua matatizo ya kila mtu mgodini kwetu,hakika hili ni pigo kwa MANGA GEMSTONE LTD. Mungu ailaze roho ya marehem ben mahali pema peponi,AMINA.
 
j
Mazingira ya kifo na mademu wawili inatia sana shaka..Tusimpangie Mungu mahali pa kumweka mkuu Kimbunga...

Mkuu katika kifo huwa tunatumia tafsida. Sijawahi kusikia watu wakisema hili liingie motoni kwa matendo yake mabaya bali humtakia rehema marehemu ili Mwenyezi Mungu aweze kumnusuru mja wake na moto hivyo husema amweka mahala pema peponi.
 
Kweli nimeamini ukicheza ngoma ya washenzi unageuka mshenzi; hata wewe mtoto wa kiungwana unatoa kauli hafifu kama
Chama
Gongo la mboto DSM
cc Ritz
Mkuu chama hii kauli yako ina chembechembe za matusi. Kwa tunaojua utumiaji muafaka wa maneno MSHENZI na MUUNGWANA tunajua WASHENZI ni wapi na WAUNGWANA ni wapi hasa ukikaa upande fulani. Haya maneno huwa yanatumika sana kuwarejea watu wa Mrima na Watu wa Pwani. Mkuu tafakari
 
Kimbunga,

Usifiche ukweli unataka kutuambia waungwana na washenzi hawapo.
 
Last edited by a moderator:
Benson Mollel (26) amekutwa amefariki dunia ndani ya Hoteli .

Mashuhuda wa tukio hilo walisema Mollel alikutwa akiwa amekufa jana mchana.

Kifo cha mwanasiasa huyo mchanga kimezusha maswali mengi.

Marehemu aliwasili usiku, juzi Jumamosi hotelini hapo akiongozana na mwanamke aliyetambulika kwa jina la Nancy na kuchukua chumba namba 208. Mlinzi alisimulia kuwa marehemu aliingia na mwanamke huyo na kisha kuondoka ghafla kabla ya kurejea tena wakiwa wote usiku.
Ilibainika kuwa mwanamke huyo aliondoka jana asubuhi.

Mmoja wa wahudumu hotelini hapo (jina lake limehifadhiwa), alisema kuwa mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Mariam aliwasili hotelini hapo saa 5.00 asubuhi na kuomba kupelekwa moja kwa moja chumba alichokuwapo marehemu. Mhudumu huyo alisema wakati mwanamke huyo akiomba kupelekwa chumbani, marehemu naye alipiga simu mapokezi akiomba mwanamke huyo apelekwe chumbani kwake, agizo ambalo walilitekeleza. Kwa mujibu wa mhudumu, baadaye kama saa 6.00 mchana walimwona mwanamke huyo akitoka nje ya hoteli hiyo na kuondoka.
 
Kimbunga,

Usifiche ukweli unataka kutuambia waungwana na washenzi hawapo.

Mkuu waungwana wapo na washenzi pia wapo lakini inategemea hayo maneno unayatumia katika muktadha gani. Chunguza utabaini.
 
Back
Top Bottom