Utata kigogo UVCCM - akutwa amekufa hotelini Arusha

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,670
"Ni baada ya kukutana na mwanamke mmoja kwenye chumba cha hotel jijini Arusha jana asubuhi"

MJUMBE wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) taifa, kupitia Mkoa wa Arusha, Benson Mollel (26) amekutwa amefariki dunia ndani ya Hoteli ya Lush Garden Business, iliyopo Mtaa wa Jacaranda katikati ya Jiji la Arusha.


Mashuhuda wa tukio hilo walisema Mollel alikutwa akiwa amekufa jana mchana na kwamba tukio hilo limezua hofu kwa wakazi wa Jiji la Arusha, huku wakijiuliza chanzo cha kifo chake.

Kifo cha mwanasiasa huyo mchanga ambaye pia alikuwa ni mfanyabiashara wa madini mkoani hapa, kimezusha maswali mengi wakati wengine wakihusisha tukio hilo na masuala ya kisiasa na upande mwingine wakidai ni masuala la kibiashara.

Hisia hizo zinatokana na ukweli kwamba Arusha ni jiji lenye hekaheka za kisiasa hasa ndani ya CCM ambapo Mollel alikuwa mmoja wa vinara wake.

Polisi waliwasili hotelini hapo saa 8.00 mchana na kuupakia mwili wa marehemu kwenye gari na kisha kuupeleka Hospitali ya Mount Meru kwa ajili ya kuhifadhiwa.

Mkuu wa Polisi wa Wilaya wa Arusha (OCD), Gilles Muruta akizungumza katika eneo la tukio alisema: "Tunachunguza tukio hili ambalo ni la ghafla."

Akizungumzia kifo hicho, Katibu Mkuu wa UVCCM, Martin Shigela alisema: "Tumepokea kwa masikitiko kifo cha Mollel japokuwa sifahamu nini hasa kimejiri huko."

"Kuna rafiki yake alinipigia simu kuniarifu kuhusu kifo hicho na nikawaambia kama UVCCM Taifa tupate maelezo kamili na tujue nini cha kufanya. Iwapo familia itakuwa na mipango yoyote watutaarifu," alisema Shigela.


Baadhi ya wanasiasa na wafanyabiashara wa madini mkoani Arusha walionekana nje ya hoteli hiyo baada ya taarifa za kifo hicho kusambaa na wengine walishindwa kujizuia kisha kuangua vilio.

Miongoni mwao ni kada wa Chadema, James ole Millya na diwani wa CCM Kata ya Mlangarini, Mathias Manga. Katibu Mwenezi wa CCM wa Mkoa wa Arusha, Isaack Kadogoo ambaye pia alifika eneo hilo alisema kwamba wamepokea taarifa za tukio hilo kwa mshtuko mkubwa.

Uongozi wa hoteli hiyo haukuwa tayari kulizungumzia kwa madai kwamba limefikishwa katika vyombo vya usalama.

Hata hivy, kwa mujibu wa vyanzo vya habari ndani ya hoteli hiyo vilidai marehemu aliwasili usiku, juzi Jumamosi hotelini hapo akiongozana na mwanamke aliyetambulika kwa jina la Nancy na kuchukua chumba namba 208.
Mmoja wa walinzi hotelini hapo aliyetembulika kwa jina la Obeid Mollel kutoka Kampuni ya Ulinzi ya Victoria Support Services, alisimulia kuwa marehemu aliingia na mwanamke huyo na kisha kuondoka ghafla kabla ya kurejea tena wakiwa wote usiku.

Alisema kuwa wakati wakiwa hotelini hapo marehemu aliomba kuegesha gari lake jipya aina ya Mark II Grande ambalo halijasajiliwa na kwamba alipokubaliwa alifanya hivyo kisha akaenda chumbani. Ilibainika kuwa mwanamke huyo aliondoka jana asubuhi.

Taarifa zaidi
Mmoja wa wahudumu hotelini hapo (jina lake limehifadhiwa), alisema kuwa mwanamke aliyejitambulisha kwa jina la Mariam aliwasili hotelini hapo saa 5.00 asubuhi na kuomba kupelekwa moja kwa moja chumba alichokuwapo marehemu.

Mhudumu huyo alisema wakati mwanamke huyo akiomba kupelekwa chumbani, marehemu naye alipiga simu mapokezi akiomba mwanamke huyo apelekwe chumbani kwake, agizo ambalo walilitekeleza.

Kwa mujibu wa mhudumu, baadaye kama saa 6.00 mchana walimwona mwanamke huyo akitoka nje ya hoteli hiyo na kuondoka.
Alisema kwamba baadaye waliamua kupiga simu ya chumba alichofia marehemu ili kujua endapo ataendelea kupanga kwani muda wa kawaida ulikuwa umemalizika lakini simu hiyo ilikuwa ikiita bila majibu.

Mmoja wa wahudumu ambaye alikuwa akifahamiana na marehemu, aliamua kumpigia kupitia simu yake ya mkononi lakini nayo haikupokewa.

Mhudumu huyo aliamua kupanda ngazi kwenda chumbani kwa marehemu na katika hali isiyo ya kawaida alikuta mlango ukiwa wazi na marehemu akiwa amelala.

"Nilijaribu kumwamsha, lakini hakuamka na ndipo alipotoa taarifa kwa uongozi wa hoteli na baadaye waliviarifu vyombo vya usalama.

Chanzo cha kifo hiki kinakanganya maana kama kweli ni mauaji basi yamefanyika kwa ustadi mkubwa," alisema mhudumu huyo na kuongeza:

"Unajua vyumba vyote vya huko juu ghorofani ukifunga mlango tu huku chini sisi mapokezi tunasikia, sasa cha ajabu mlango tumeukuta wazi. Hapa kuna maswali mengi," alieleza mhudumu huyo.


Source: Mwananchi

================DEVELOPING STORY=============

Moses Mashalla, Arusha
UCHUNGUZI wa awali wa kifo cha aliyekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM), kupitia Mkoa wa Arusha, Benson Mollel (26) umeonyesha kuwa chumbani alimofariki kulikutwa mipira miwili ya kiume, mmoja ukiwa umetumika.

Marehemu Mollel alikutwa amekufa juzi ndani ya Hoteli ya Lush Garden Business, Mtaa wa Jacaranda, Arusha katika mazingira ya kutatanisha huku mwili wake ukiwa mtupu. Anatarajiwa kuzikwa kesho Arusha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema pia kuwa ndani ya chumba alichofia, ilikutwa silaha aina ya bastola, kiasi kidogo cha madini ya Tanzanite, simu mbili, kadi za benki na fedha ambazo kiasi chake hakikutajwa.

"Kwa sasa bado tunachunguza tukio hilo kwa kuwa linatawaliwa na utata kwani marehemu hakukutwa na aina yoyote ya jeraha mwilini... uchunguzi wa kina utafanyika kubaini nini kilisababisha kifo cha Mollel kwa kushirikiana na familia yake."

Kamanda Sabas alisema pia kuwa licha ya marehemu kujishughulisha na siasa pia alikuwa akifanya kazi katika Kampuni ya Madini ya Manga Germs iliyopo Arusha
Baadhi ya mashuhuda walisema, kabla ya marehemu kukutwa na mauti hayo, alitembelewa na wanawake wawili Jumamosi na Jumapili iliyopita, ndani ya chumba chake.

Mmoja wa mashuhuda hao, ambaye ni mhudumu wa hoteli alisema alimpokea mwanamke mmoja akimtaka Mollel, Jumapili iliyopita.

Mhudumu huyo (jina tunalo) alisema mwanamke huyo alionekana hotelini hapo kwa mara ya kwanza siku hiyo na mkononi alikuwa ameshikilia kipochi kidogo cha mkononi (wallet) na aliingia chumbani kwa marehemu na kutoka baada ya dakika 15.

"Alipofika hapa hotelini dada huyo aliomba tumpeleke chumba hicho namba 214 baada ya kuwasiliana na marehemu... tukamwelekeza akaenda lakini sura hii tulikuwa hatujawahi kuiona," alisema.

Naye mlinzi wa hoteli hiyo aliyejitambulisha kwa jina la Obeid Mollel kutoka Kampuni ya Ulinzi ya Victoria Support Services inayolinda hoteli hiyo, alisema alimwona dada huyo aliyekuwa na marehemu akitoka nje ya uzio wa hoteli akiwa hana kitu chochote mkononi na aliondoka kwa miguu bila usafiri wowote.

Mtumishi wa chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Mount Meru, Francis Costa 'Rasta', alithibitisha kuona mipira hiyo ya kiume iliyokuwa imehifadhiwa katika shuka lililokuwa limehifadhi mwili wa marehemu ulipofikishwa hapo saa 8.30 usiku.

Alisema muda mfupi baada ya kuukabidhi mwili huo na kuondoka, maofisa wa polisi waliopeleka walirejea na kuchukua mipira hiyo.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Mount Meru, Dk Frida Mokiti alisema utaratibu wa kuufanyia uchunguzi utategemea maagizo ya polisi.

CCM Mkoa wa Arusha kimeunda Kamati ya Mazishi itakayokuwa chini ya Diwani wa Kata ya Mlangarini, Mathias Manga ambaye alisema misa ya kumwombea marehemu itaanza kufanyika kesho Kata ya Daraja Mbili.

Alisema kuwa kwa sasa wanamsubiri baba mzazi wa marehemu ambaye yuko Mwanza.

source: mwananchi
 
Martin Shigella katibu mkuu UVCCM...!?? Hii habari ya lini?
 
MJUMBE wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) taifa, kupitia Mkoa wa Arusha, Benson Mollel (26) amekutwa amefariki dunia ndani ya Hoteli ya Lush Garden Business, iliyopo Mtaa wa Jacaranda katikati ya Jiji la Arusha.

Mashuhuda wa tukio hilo walisema Mollel alikutwa akiwa amekufa jana mchana na kwamba tukio hilo limezua hofu kwa wakazi wa Jiji la Arusha, huku wakijiuliza chanzo cha kifo chake.

Kifo cha mwanasiasa huyo mchanga ambaye pia alikuwa ni mfanyabiashara wa madini mkoani hapa, kimezusha maswali mengi wakati wengine wakihusisha tukio hilo na masuala ya kisiasa na upande mwingine wakidai ni masuala la kibiashara.

Hisia hizo zinatokana na ukweli kwamba Arusha ni jiji lenye hekaheka za kisiasa hasa ndani ya CCM ambapo Mollel alikuwa mmoja wa vinara wake.

Polisi waliwasili hotelini hapo saa 8.00 mchana na kuupakia mwili wa marehemu kwenye gari na kisha kuupeleka Hospitali ya Mount Meru kwa ajili ya kuhifadhiwa

Source: MWANANCHI
 
Namkumbuka Benson tulisoma nae Umbwe sec. Mungu ailaze mahali pema peponi roho yake!
 
Mungu ametoa Mungu ametwaa, Jina la Bwana Mungu lihidiwe, marehemu aende kwa amani ya Mungu
 
Rip kada wa CCM ! Ben Mollel!.
Whatever the cause of his death, the reasons and the motive behind, kitendo cha roho kuuacha mwili kwa sababu yoyote ile , ni kiashiria kuwa siku yake ilikuwa imefika! na chochote kilichomtokea kilikuwa kitokee ili tuu kwa sababu ni premeditated event.
Bwana Alileta, Bwana Ametwaa, Jina Lake Lihimidiwe!.
Pasco.
 
Back
Top Bottom