Utata Juu ya Kifo Cha Rais JF Kennedy

Utata Juu ya Kifo Cha Rais JF Kennedy

SEHEMU YA TATU


Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi @Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu Debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM @Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu The Certified DON SINYORI mij adden



bwii ONTARIO Kobe The Vein Mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya Sitaki ukuda Domhome Mpatanishi MKANDAHARI mtugani wa wapi huyo wealthier cluecell Toyota escudo mgumu2 troublemaker Linamo shedede kamtu33 SteveMollel ngushi Donald stewart Mshuza2 Glycel mnonje Ochuanilove SingleFather Santi DEOD 360 ngushi anatory antony ukhuty chris van chicha auxillius Goma Son Hubeb pes KING DUBU VILLAIN mwayena donbeny Aleppo JipuKubwa shoo61 BOMBAY John mungo Nyakageni bato Dogo 1 sufra chamlungu painscott wegman Bravo Engliash MOSELBAY wa stendi FaizaFoxy bigmind cadabraa Internal Kelvin mwalukas mnonje Kelvin X Somoche Wgr30 Miiku Poise Jabman kalamuyamwalimu BOMBAY the say juxhb witnessj Gide MK Mmanyema mgogoone Mnongane Mandingo koncho77 afsa ngaboru Paradoxer Heavy Metal KIMBURU 06 Raaj kichekoh ngumba njeche kikale DullahTza Goodluck Mshana julius Darcy Denis Kasekenya mashonga kitalembwa Khaleed Shaban middle east SirChief jiwe jeusi Mkambarani mansakankanmusa gambada ynwa ney kush
MSAADA: hii ni lugha gani?
 
Afu nyie mnao quote Uzi mrefu kama huu huwa mnakera kinyama kwa cye wenye kutumia v cm
 
Utata upi wakati huyu jamaa alipigwa risasi zaid ya moja
 
Aiseeee!! J F Kennedy angekuwepo means CIA isingekuwa hai Leo hii, na huenda Dunia ingekuwa na amani kidogo na matukio ya CIA Return If Possible J F Kennedy

CIA CIA CIA CIA CIA CIA Aisee!.......

( Hey The bold kuna hizi habari kuwa eti Raisi J F Kennedy ndie alietengeneza Virusi vya Ukimwi ili kupambana na watu weusi kwamba alikuwa hawapendi.. Hii inaukweli wowote bold au pia kuna kitu nyuma ya pazia? )
 
Aiseeee!! J F Kennedy angekuwepo means CIA isingekuwa hai Leo hii, na huenda Dunia ingekuwa na amani kidogo na matukio ya CIA Return If Possible J F Kennedy

CIA CIA CIA CIA CIA CIA Aisee!.......

( Hey The bold kuna hizi habari kuwa eti Raisi J F Kennedy ndie alietengeneza Virusi vya Ukimwi ili kupambana na watu weusi kwamba alikuwa hawapendi.. Hii inaukweli wowote bold au pia kuna kitu nyuma ya pazia? )
Hata mimi natamani kujua historia ya kutengenezwa kwa birusi vya ukimwi dhamira yake na watu walio nyuma ya pazia.
 
UTATA WA KIFO CHA RAIS JFK



FINALE

Katika sehemu zilizopita za mfululizo wa makala hii nilieleza namna ambavyo mauaji ya Rais Kennedy yalivyotokea na namna ambavyo muuaji alihusishwa na utekelezaji wa tukio hilo. Pia nilieza utata juu ya dalili kwamba anayetuhumiwa kumuua Rais Kennedy kuna uwezekano mkubwa wa kuwa anasingiziwa kwa makusudi kabisa ili kuficha uhusika wa watu halisi walio nyuma ya tukio hilo.
Mwishoni nilieleza namna ambavyo uhusiano kati ya CIA na Rais Kennedy ulizorota na kupelekea kuanza kujengeka kwa chuki kubwa kati yao.

Katika sehemu hii ya mwisho nadhamiria kuonyesha dalili na vidhibiti ambavyo vinaonyesha kuwa CIA hawawezi kukwepa lawama ya uhusika nyuma ya kifo hiki cha Rais Kennedy.

Tuendelee…


DALILI ZA 'MCHORO' WA KUMUHUSISHA OSWALD NA MAUAJI

Baada ya tukio hili la mauaji ya Rais Kennedy na baadae kukamatwa na kuuwawa kwa Oswald pasipo dunia kupata nafasi ya kumsikia Oswald anasemaje kuhusu hilo, vyombo vya ulinzi na serikali viliibuka na kutoa msululu wa 'vidhibiti' kujaribu kuhalalisha kwa nini Oswald alikuwa ni muhusika wa tukio hili.

Ili kuhalalisha uhusika wa Oswald katika tukio hili ni lazima serikali iliwabidi waeleze angalau "motive" (msukumo) ambayo iliyomfanya Oswald kutekeleza kile ambacho alikifanya.

Sababu kubwa ambayo inatolewa na serikali ya Marekani ni historia ya Oswald kuunga mkono itikadi za kijamaa kwa kiwango kilichokithiri.

Hoja hii inajengwa kutoka na kitendo cha Oswald kutorokea nchini Urusi mwaka 1959 na kujaribu kubadili uraia akiwa huko. Pia hata mkewe Bi. Marina Prusakova alimpatia huko na alikuwa raia wa Urusi.
Oswald aliishi nchini Urusi toka mwaka huo 1959 mpaka katikati ya mwaka 1962 ambapo alirejea Marekani pamoja na mkewe Marina na mtoto wao mchanga.

Historia hii mpaka hapa iko sahihi kabisa… lakini baada ya Oswald kurejea nchini Marekani kuna kila dalili kwamba kuna kikundi cha watu ambao walikuwa wanajaribu kutumia mwanya wa Oswald kuishi Urusi kwa muda na imani yake ya kijamaa kutengeneza mazingira ya uhusika wa tukio la kumuua Rais Kennedy mwaka 1963.

Jambo la msingi la kuzingatia hapa ni kwamba… kama unahitaji kutengeneza 'mchoro' wa kumdondosha mtu mzito kama rais wa Marekani na unahitaji mtu ambaye atabeba lawama hiyo, basi unapaswa kuwa na mpango adhimu haswa ambao unatakiwa kuwa na 'back-up story' yenye mashiko ya hata miezi au miaka kadhaa nyuma.

Sasa basi,

Watu wengi wa karibu na wanaomfahamu Oswald wamekuwa wakisema kwamba Oswald alibadilika mno na kulegeza misimamo yake ya kijamaa tangu arejee Marekani kutoka Urusi. Kwa hiyo kutumia kigezo hicho kuhalalisha nadharia ya "motive" iliyomfanya ampige risasi Kennedy inakuwa si sahihi.

Lakini serikali ya Marekani kupitia taarifa ya Wareen Commision walikuja na taarifa yao nyingine wakidai kwamba kwa mujibu wa uchunguzi wa CIA wenyewe wanadai kuna ushahidi kwamba Oswald alijaribu tena kwenda nchini Urusi hata baada ya kurejea Marekani.

Wanasema kwamba miezi miwili kabla ya tukio la mauaji ya Rais Kennedy, Oswald alisafiri mpaka nchini Mexico kwenye ubalozi wa Cuba akiomba 'transit visa' kwamba anataka kupita nchini Cuba kabla ya kwenda Urusi.
CIA wanadai wamba ubalozi wa Cuba nchini Mexico ulimtaka Oswald kwanza wapate uthibitisho kutoka nchini Urusi kwamba Oswald amepata kibali cga kwenda huko.

Taarifa hiyo inaeleza kwamba Oswald alikaa karibia siku tano nchini Mexico akihangaika kati ya ubalozi wa Urusi na ubalozi wa Urusi ili kupata vibali husika aweze kwenda nchini Cuba na hatimaye Urusi lakini hakukuwa na mafanikio yoyote.

Taarifa hii ya CIA inatumika kuhalalisha tuhuma ya itikadi kali ya kijamaa ambayo Oswald alikuwa nayo na kupelekea kutekeleza tukio la mauaji ya rais Kennedy.


Lakini hii ni taarifa ya CIA… je uhalisia ukoje?


Kwanza kabisa ifahamike kwamba siku ya Octoba 18, 1963 ubalozi wa Cuba nchini Mexico ulitoa visa kwa mtu anayeitwa Lee Harvey Oswald. Lakini visa hii haikuchukuliwa na muhusika ambaye aliomba.

Kwa hiyo japo jambo linaweza kuonekana ni jepesi lakini inaanza kutia shaka kwa nini visa hii haikuchukuliwa. Kwa nini Oswald asafiri mpaka nchini Mexico ili kujaribu kwenda Cuba na baadae Urusi aiche Visa hii wakati ndicho alichokifuata. Lakini pia inaibua swali kwa nini Oswald, mjamaa wa itikadi kali kama ambavyo CIA wanamuelezea akache tu ghalfa safari yake hiyo ya ndoto zake.

Ndipo hapa ambapo inafungua mlango wa kuangalia kwa undani suala hili.

Huko nyuma nilieleza kwamba licha ya Rais Lyndon Johnson kuunda kamati yake (The Warren Commision) lakini kwenye miaka ya 1970 baraza la wawakilishi la Congress liliunda kamati yake kuchunguza matukio yote ya mauaji ya kupangwa kwa viongozi. Kamati hii iliitwa House of Representatives Select Committee on Assasinations. Lengo la kamati hii lilikuwa ni kufanya uchunguzi upya na kwa mlengo tofauti na chunguzi ambazo zilifanywa na kamati za serikali kuu, mfano The Warren Commision.

Kama sehemu ya utendaji kazi wa kamati hii, walimuajiri mwandishi nguli wa habari za kichunguzi aliyeitwa Gaeton Fonzi. Kazi ambayo alipewa Bw. Fonzi ilikuwa ni kuangalia uwezekano wa wahamiaji kutoka Cuba wenye kupinga utawala wa Fidel Castro kama kuna uwezekano wowote walihusika kwenye tukio la mauaji ya rais Kennedy.

Katika uchunguzi wake, Fonzi alimuhoji mtu anayefahamika kwa jina la Antonio Veciana. Huyu alikuwa kiongozi wa kikundi cha Alpha 66 ambao walikuwa ni moja ya vikundi vya wapiganaji wa Cuba wanaoishi Marekani wakiwa na dhamira ya kumuondoa madarakani Fidel Castro.
Veciana alikuwa recruitted na kuwa 'asset' wa CIA na 'handler' wake alikuwa afisa wa CIA anayejiita 'Maurice Bishop'. Hili jina lilikuwa ni 'alias' ambayo huwa inatumiwa na afisa nguli wa CIA anayeitwa David Atlee Phillips.

Kama umekuwa msomaji wa makala zangu kwa siku nyingi lazima umekutana mara kadhaa na jina hili. David Atlee Phillips alikuwa ni kiongozi wa Oparesheni za CIA ukanda wa magharibi (Chief Of Operations For the Western Hemisphere).
David Atlee anahusika kwenye skandali nyingi mno za CIA. Kuanzia kuondoa madarakani serikali ya Guatemala, Iran na hata mauaji ya viongozi wa Kiafrika kama vile Patrice Lumumba.

Sasa basi,

Veciana anasema kuwa kulikuwa na mara kadhaa ambazo alipokutana na handler wake, yaani "Bishop" nchini Mexico alikuwa ameambatana na 'asset' mwingine ambaye alimjua kwa jina la Lee Harvey Oswald kama ambavyo alitambulishwa.
Lakini Veciana alipoambiwa aeleze muonekano wa Oswald alito maelezo ambayo hayarandani kabisa na muonekano wa Oswald 'halisi'.

Lakini pia Fonzi alipata ushahidi kutoka kwa mtu anayeitwa Oscar Contreras. Huyu alikuwa ni kiongozi wa chama cha wanafunzi nchini Mexico ambao walikuwa wanaunga mkono utawala wa Fidel Castro. Contreras anaeleza kwamba kwamba akiwa nchini Mexico aliwahi kufanya maongezi na mtu anayeitwa Lee Harvey Oswald akimueleza namna ambavyo alikiwa anapata ugumu kupata visa ya Cuba.
Contreras naye alipoambiwa aelezee muonekano wa huyo 'Oswald' ambaye alikutana naye Mexico… naye pia alieleza muonekano tofauti kabisa na Oswald halisi.

Kama hii haitoshi… Fonzi alimuhoji Bw. Eusebio Azcue ambaye aliyekuwa balozi wa Cuba nchini Mexico kipindi ambacho inadaiwa Oswald alifika mara kadhaa kuomba visa. Balozi Azcue alipoonyeshwa picha ya Oswald halisi na kuulizwa kama huyo ndiye mtu aliyefika ubalozini kuomba visa alikataa katakata kwamba hafanani kabisa na mtu ambaye alifika ubalozini kuomba visa.

e97d04bfb78c51f4af21dd6753c66a9a.jpg

DAVID ATLEE PHILLIPS


Lakini si balozi pekee ambaye alihojiwa na Fonzi, bali pia Fonzi alimuhoji Bi. Sylvia Duran ambaye alikuwa kwenye dawati la mapokezi ubalozini katika kipindi ambacho inadaiwa kuwa Oswald alifika ubalozini kuomba Visa. Naye alipoonyeshwa picha ya Oswald halisi alisema kuwa huyo sio mtu aliyefika ubalozini kwao kuomba visa na kujitambulisha kama Lee Harvey Oswald.

Kutokana uchunguzi wake huu na mahojiano na wahusika hao juu… Bw. Gaeton Fonzi katika taarifa yake ambaye aliiwasilisha kwa kamati ya baraza wa wawakilishi la Congress alihitimisha kwamba kuna kila dalili kwamba afisa wa CIA Bw. David Atlee Phillips (ambaye huwa anajitambulisha kama 'Maurice Bishop') amefanya kazi kubwa na kuhusika katika kumtengeneza mtu bandia anayejiita Lee Harvey Oswald ambaye amekuwa akifanya harakati kadhaa ili kutoa image ya kwamba 'Lee Harvey Oswald' ni mtu mwenye kuunga mkono Ujamaa na mwenye kupinga vikali tamaduni na uongozi wa kimagharibi.

Kutengenezwa kwa 'image' hii ya Oswald kwamba ni mjamaa na mwenye kuchukia mataifa ya magharibi na viongozi wake, ilikuja kuleta urahisi wa kuhalalisha shutuma ambazo Oswald alituhumiwa kumuua rais Kennedy.

Kama hii haitoshi kuna ushahidi mwingine wa kutosha zaidi kudhihirisha kwamba CIA walihusika kutengeneza 'mchoro' na kumjengea 'image' mbaya Oswald ili ije kuwa rahisi kumbebesha shutuma kwa kile ambacho walipanga kukitekeleza kama mwezi mmoja baadae.

Siku ya tarehe 1 octoba 1963, CIA walituma taarifa kwenya FBI, Wizara ya Mambo ya Nje na Navy kuwaeleza juu ya raia wa Marekani mwenye jina la Lee Harvey Oswald kutembelea Mexico na harakati zake za kupata visa za Cuba na Urusi.

Ajabu ni kwamba taarifa hii ya CIA haikuwa imeambatanishwa na picha kama ilivyo desturi ya taarifa zote za CIA. Ni ajabu zaidi kwa kuwa kipindi hicho CIA walikuwa wana kamera nje ya balozi za Cuba na Urusi nchini Mexico ili kufuatilia nyendo za kila anayetoka na kuingia.
Ni dhahiri kwamba kitendo chao hiki cha kutoambatanisha picha bali maelezo tu kuhusu Lee Harvey Oswald, kulidhihirisha taarifa hii ilikuwa inapikwa na walijua kuwa 'Oswald' huyo wa kwao siye yule halisi na hii ilikuwa ni jitihada za kuendelea kutengeneza image ya kwamba Oswald halisi ni mjamaa wa itikadi kali na mwenye kuchukia umagharibi. Na hii kama nilivyosema ilikuwa inafanyika makusudi ili kuja kurahisisha mpango wa kutupa shutuma kwa Lee Harvey Oswald.

Katikati ya mwezi octoba, 1963 kwa mara nyingine tena CIA walituma ujumbe wa sauti kwenda FBI, Wizara ya mambo ya Nje na Navy kuwataarifu kwamba ujumbe huo wa sauti umedukuliwa kutoka kwenye mawasiliano ya simu kati ya Lee Harvey Oswald na maafisa wa ubalozi wa Urusi nchini Mexico.

Katika kipindi hicho suala hili liliaminiwa na FBI lakini baadae, baada ya baraza la wawakilishi la Congress kuagiza uchunguzi ufanyike upya iligundulika kwamba recording hiyo haiwezi kuwa ni Lee Harvey Oswald kwa kuwa anayeongea kwenye recording hiyo ni mtu ambaye anaonekana kuhangaika na kuongea lugha ya Kirusi tofauti na Oswald halisi ambaye anafahamika kuwa alikuwa na ufasaha wa hali ya juu kwenye lugha hiyo kutokana na kuishi nchini Urusi.

Niongeze suala lingine la mwisho…

Kama ulikuwa haufahamu lakini kuna suala ambalo limekuweponkwa miaka mingi sana… japokuwa kwa sasa wamebaki kama wapinzani wa jadi tu lakini miaka ya zamani kulikuwa na uhasama halisi kati ya idara hizi mbili, CIA na FBI. Kila upande ulikuwa unahisi wenyewe ndio wenye kutukuka na kufaa kuwa mlinzi wa Taifa la Marekani. Pia kila upande ulikuwa unahisi upande mwingine ni kikwazo kwenye kutekeleza majukumu yake. Katika makala yangu ya "Behind The Curtain" nilionyesha ni namna gani kila upande ulikuwa na taarifa fulani fulani lakini walikuwa hawashirikishi upande mwingine na matokeo yake kutengeneza mwanya adhimu kabisa wa adui kufanya shambulio la september 11.
Kwa hiyo kama ni huu 'mchoro' wa kumdungua Rais Kennedy ulichorwa na CIA basi ni dhahiri kwamba hakuna mtu yeyote ndani ya FBI ambaye alihusishwa.
32b6c7a941b7f56b0faf41e7ffccc13e.jpg

Mkurugenzi wa FBI wa kipindi hicho Bw. Hoover

0d9bf79eef88ba38adea47260fa855d6.jpg

Sehemu ya "memo" ya siri kutoka FBI juu ya mauaji ya Rais JF Kennedy

Na hii ndio inatoa sababu kwa baadhi ya wakubwa wa FBI siku za mwanzoni kabisa baada ya mauaji ya Kennedy kuanza kuwa na wasiwasi kwamba inawezekana kuna la zaidi;

Kuna 'transcript' ya maongezi kati ya Mkurugenzi wa FBI Bw. Edgar Hoover na rais Lyndon Johnson yaliyofanyika Nov 23, 1963 siku moja tu baada ya mauaji ya Kennedy. Transcript hij ilivuja mwaka 2006 kutoka kwenye files za FBI wenyewe;

Nanukuu transcript hii kama ilivyo;


Rais Johnson; "Have you established anymore about the (Oswald) visit to the Soviet Embassy in Mexico in September?

(Kuna lolote umeling'amua juu ya (Oswald) kutembelea Ubalozi wa Urusi nchini Mexico?)

Hoover; No, there is an angle that's very confusing for this reason. We have up there a man at the Soviet Embassy , using Oswald's name.……….. do not correspond to this man's voice, nor to his appearance. In other words, it appears that there was a second person who was at the Soviet Embassy."

(Hapana, kuna upande wa suala hili unachanganya mno. Nahisi kuna mtu kule ubalozi wa Urusi anatumua jina la Oswald na hawarandani kwa sauti, wala kwa muonekano. Kwa maneno mengine, inaonekana kwamba tuna mtu mwingine tofauti wa pili anayeenda ubalozi wa Urusi na kujitambulisha kama Oswald).


Ni kwa nini CIA watumie nguvu nyingi hivi kumtengeneza mtu anayetumia jina la Oswald ambae matendo yake yalisababisha kujenga image kwa Oswald halisi kwamba ni mwenye kufuata itikadi ya Ujamaa mkali na mwenye kuchukia umagharibi?

Ni kwa namna gani hasa CIA hatimaye walitekeleza tukio hili la mauaji?? Nani ailifyatua risasi?


Nitarudi tena…

Stay here.


The Bold
To Infinity and Beyond.
 
Back
Top Bottom