Utata Juu ya Kifo Cha Rais JF Kennedy

Utata Juu ya Kifo Cha Rais JF Kennedy

ahsante sana,nilikuwa sifahamu chochote juu ya tukio hilo la mauaji, ila nahisi hii sehemu niliyoinukuu hujaimalizia au ndio bado inaendelea?
Siku nyingine usiwe una-quote Uzi mrefu namna hii, unatupa tabu watumiaji wa simu.
 
Hii imenipitaje sijui nimechelewa kuifuatilia. Tupo sambamba sasa.


Kuna makala ya kuhusu kifo cha Osama niliisikia katika redio moja kama ilivyo namna ulivyoiandika humu.
 
ni vilaza wasiopenda kukishughulisha kutafuta story zao kuna story nyingi tu za uku JF naziona FB na IG zinabadilishwa heading tu
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Hii imenipitaje sijui nimechelewa kuifuatilia. Tupo sambamba sasa.


Kuna makala ya kuhusu kifo cha Osama niliisikia katika redio moja kama ilivyo namna ulivyoiandika humu.
Kama wapo wanasheria humu wamsaidie jamaa kudai haki yake sio siri inauma
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Uongozi wa JF wasipochukua hatua za kulinda machapisho humu tutapoteza makala za wadau wengi tu. Piracy imemkatisha tamaa mno The Bold!
 
UTATA WA KIFO CHA RAIS JF KENNEDY




SEHEMU YA TATU






"NANI ALIYEMFUNGA PAKA KENGERE??"



Japokuwa serikali ya Marekani wameendelea kushikilia msimamo kuwa Lee Harvey Oswald alihusika yeye kwa binafsi yake kudungua na kumuua Rais Kennedy kutokana na kudaiwa kuwa misimamo mikali ya sera za kijamaa, lakini kuna vidhibiti vingi vinavyoonyesha kuwa kuna kikundi au vikundi vya watu wenye nguvu kubwa walio nyuma ya mauaji haya.

Kabla sijaweka vidhibiti vya kuonyesha labda ni watu gani wamehusika na kifo cha Kennedy, ningependa awali ya yote tujaribu kukiangalia kisa cha Oswald kuambiwa kuwa ndiye aliyemdungua rais na ukweli na wake na maswali yayozunguka suala hili.


Dalili ya kuwepo ya wadunguaji zaiji ya mmoja


Nikumbushe kuwa, wiki moja baada ya mauaji haya ya Rais Kennedy, Rais mpya Johnson aliunda tume maalumu kuchunguza ukweli juu ya tukio hili.
Tume hii iliundwa kwa kutokana na Executive Order number 11130 na kutambuliwa na Congress kupitia Resolution number 137.

Kamisheni hii ilikuwa chini ya Uenyekiti wa Chief Justice Earl Warren na ndio sababu ya kujulikana kamaa The Warren Commission.
Kulikuwa na mabishano makali juu ya uundwaji wa kamisheni hii, hiku baadhi ya viongozi waandamizi serikali wakiamini kuwa kamisheni hii itaamsha hasira za wananchi badala ya kutatua utata uliopo.

Licha ya viongozi wengi wakuu serikalini kushauri kutoundwa kwa hii kisheni lakini kwa sababu ambazo Rais mpya Johnson yeye binafsi aliziona ni muhimu akaunda tume hii wiki moja tu baada ya tukio na ilifanya kazi kwa takribani miezi kumi na hatimaye kukabidhi ripoti yake kwa Rais tarehe 24 September, 1964 na kuwekwa hadharani kwa wananchi siku tatu baadae.

Nitaizungumzi zaidi Ripoti hii na masuala kadhaa kuihusu huko sehemu za mbeleni za hii makala. Lakini jambo kuu zaidi hii Ripoti inachojaribu kuonyesha ni kwamba Lee Oswald alifanya tukio kwa utashi wake pekee na hakushirikiana na mtu yeyote!!

Siku moja tu baada ya ripoti hii kutoka ilikutana na upinzani mkubwa kutoka kwa watu waliofuatilia tukio hili kwa makini pamoja na wachambuzi wa masuala ya intelijensia.
Ripoti hii ilionekana kama vile ilikuwa ni jaribio la serikali kujisafisha na haikuwa na nia ya kuchimbwa ukweli juu ya nini hasa kilitokea siku ya November 22, 1963.

Moja wapo ya vitu ambavyo Ripoti hii imepingwa vikali ni jaribio lake la kutaka kuaminisha umaa kuwa Oswald ndiye muhusika na alikiwa pekee kwenye tukio hili.

Japokuwa ripoti yaa Warren Commission inabakia kuwa msimamo rasmi wa serikali mpaka leo hii juu ya kifo cha Rais Kennedy lakini vipo vidhibiti kadhaa vinavyoonyesha kuwa kuna uwezekano mkubwa wa tukio hilo (kumpiga risasi rais) siku ya Nov 22, lilitekelezwa na zaidi ya mtu mmoja.



Nitaeleza…



Kuna jambo moja la msingi sana ambalo nadhani wengi labda watakuwa hawajawahi kulisikia licha ya kusoma makala nyingi kuhusu kifo cha Kennedy.

Wakati natafiti kuhusu makala hii nilijitahidi kuipitia ripoti ya Warren Commission na baada ya kuipitia kuna jambo lilijoficha sana ambalo nililiona na kufanya nichimbe zaidi kuhusu ni nini kilitokea polisi ambapo Oswald alishikiliwa.



Hiko hivi,


Bunduki iliyotumika kufyatua risasi iliyomuua Rais Kennedy inatajwa kwenye ripoti ya Warren Commission kuwa ni "Mannlicher-Carcano."
Lakini ukifuatilia kwa undani utagundua kwamba bunduki hii ni aina ya 6.5x52mm Carcano (model 91/38 - Infantry Rifle).

Bunduki hii ina uzito wa kilo 3.9 na urefu wa milimita 1285 (inch 50.6) ambapo urefu wa mdomo wa mbele pekee (barrel length) ni 780mm (inch 30.7).

Risasi inayopigwa kutoka kwenye bunduki hii ina uwezo wa kusafiri mita 700 kwa sekunde na kwenda umbali mpaka kufikia mita 1000.

Pia uzalishwaji wa bunduki hizi nyingi ulifanyika mwaka 1891 nchini Italia na kuna model chache zilitengenezwa miaka1940s huko huko Italia.


59dc5645a4e684b34ace5b2370139a59.gif

BUNDUKI AINA YA "MANNLICHER-CARCANO" INAYODAIWA KUTUMIWA NA OSWALD KUMUUA KENNEDY


f45dfb3aafb34503a80967bd81642eda.jpg

KIDHIBITI NAMBA 141 CHA WARREN COMMISSION... RISASI AMBAYO ILIKUTWA KWENYE BUNDUKI YA HAPO JUU



Tutarudi baadae kuhusu umuhimu wa hizi details nilizozoweka lakini kwa sasa nataka tuweke mkazo zaidi kwenye 'feature' moja muhimu ya bunduki hizi, telescopic sight.

Bunduki nyingi zilizopo za Mannlicher-Carcano (hata kipindi hicho cha mwaka 1963) hazina Telescopic sight (darubini ya mdunguaji… yaani ile lenzi ambayo sniper anachungulia kupata muono mzuri wa target yake).

Lakini bunduki inayodaiwa kutumiwa na Oswald ilikuwa na telescopic sight. Hii ina maana kwamba eidha aliifanyia modifications au alihangaika kupata model chache za Carcano zilizozalishwa miaka ya 1940s.


Sasa basi,

Kuna kitu ambacho naamini watumiaji wengi wa silaha watakuwa wanakifahamu, kinaitwa GSR au wengine wanaita CDR (Gunshot Residue au Cartridge Discharge Residue).

Hili ni kama unga au vumbi fulani jembamba sana linatoka ukifyatua risasi na mara nyingi huwezi kuliona.
Vumbi hili linatokana na propellant ya risasi ndani ya bunduki pale inapofyatuliwa, pia vipande vidogo vidogo sana (particles) za risasi na catridge ikifyatuka.

Kitaalamu, GSR inaruka futi 3 mpaka 5 kutoka bunduki ilipofyatuliwa, kwa maana ya kwamba mtu anayefyatua bunduki hii ni lazima atarukiwa na 'vumbi' hili la GRS na vumbi hili huwa linakaa mwilini kwa mfyatuaji risasi kwa masaa matatu mpaka sita kitegemea na aina ya silaha iliyotumika.


Sasa,

Katika uchunguzi wa matukio ya uhalifu kwa kutumia silaha kuna kipimo kinaitwa Paraffin Test.
Kipimo hiki huwa kinapima uwepo wa GRS katika nguo na mwili wa mtu ambaye anahisiwa kutumia hiyo silaha katika tukio hilo mahususi.

Kipimo kikileta majibu positive - hii maana yake ni kwamba mtu huyo alifyatua hiyo risasi, au alikuwa karibu muda ambao risasi ilipofyatuliwa au aliigusa risasi silaha muda mfupi baada ya kufyatuliwa.


Majibu ya kipimo yakija negative - hii ina maana kwamba mtu huyo hakufyatua risasi, au hakuwa karibu muda ambao risasi ilifyatuliwa au hakuigusa silaha baada ya kifyatuliwa.


Turudi kwenye ninachojaribu kueleza… kwa mujibu wa taarifa ya makao makuu ya polisi Dallas ambapo Oswald alishikiliwa, alipokuwa hapo kituoni alifanyiwa Paraffin Test.
Ajabu ni kwamba majibu yalikuja negative.!!
Maana yake ni kama nilivyoeleza hapo juu, majibu negative yanamaanisha kuwa mtu huyu hakufyatua risasi, na hakuwa karibu na silaha wakati inafyatuliwa na wala hakuigusa baada ya kufyatuliwa.

Hii ina maana gani? Warren Commission na serikali hawakuiona hii ripoti ya Polisi???


Jibu ni kwamba waliiona na wakaja na "majibu" yao;

Kwamba,

Kwenye ripoti ya Warren Commission wanaeleza kwamba walimuhoji mama anayeitwa Earlene Roberts. Huyu ni yule mama wa usafi katika jengo ambalo kulikuwa na chumba cha Oswald anapoishi.
Warren Commission wanadai kuwa mama huyu aliwaeleza kuwa alimuona Oswald akirudi kwake na kuondoka tena baada ya kama dakika tatu au nne na alipoondoka alikuwa amevaa nguo nyingine tofauti na zile za awali alizokuja nazo.

Kwa hiyo Warren Commission wakatumia ushahidi huu kuhitimisha swali la kwanini majibu ya Parrafin Test ya Oswald yalikuja negative.
Ufafanuzi wao ni kwamba nguo alizozivaa wakati anapimwa hicho kipimo hazikuwa zile ambazo alizivaa wakati anafyatua risasi na hata baada ya kupekuliwa alipokuwa anaishi na nguo za awali kupatikana tayari muda ulikuwa umepita kuwezesha kipimo kubashiri uwepo wa GSR.


Lakini huu ni ukweli nusu ambao unapotoshwa kwa makusudi au kwa bahati mbaya.

Nilieleza kwamba bunduki inayodaiwa kutumika na Oswald ina telescopic sight (darubini ya kudungulia). Maana yake kwamba mtumiaji lazima ainame juu ya bunduki ili aweze kuchungulia kutumia telescopic sight.
Maafisa wote wa FBI ambao ni walengaji (Marksmen) ambao walitumiwa kwenye uchunguzi wa miaka ya hivi karibuni kutafiti juu ya GSR kwa kutumia bunduki ile ile inayodaiwa ilitumiwa na Oswald ikiwa na telescopic sight, katika vipimo vya Parrafin wote walikutwa na kiwango kikubwa cha GSR usoni na hasa hasa mashavuni.

Kwa hiyo, maelezo ya kuwa Oswald alibadili nguo ndio maana majibu ya Parrafin Test yakaonyesha negative yanakuwa hayajitoshelezi sana.


Labda tuchukulie ndani ya dakika tatu hizo alizoingia chumbani, Oswald alioga kwa umakini wa hali ya juu na kujisugua haswa na kisha kubadili nguo (which is unlikely mtu kufanikisha yote hayo ndani ya dakika tatu)…. Bado kuna kiwango kikubwa cha sintofahamu kuhusu ufyatuaji wa risasi…. Nitarejea baada ya muda mchache kueleza kuhusu utata wa risasi zilizofyatuliwa kutoka Texas School Bokoks Depository!



Stay tuned for Part 4


The Bold - 0718 096 811
 
SEHEMU YA TATU


Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi @Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu Debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM @Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu The Certified DON SINYORI mij adden



bwii ONTARIO Kobe The Vein Mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya Sitaki ukuda Domhome Mpatanishi MKANDAHARI mtugani wa wapi huyo wealthier cluecell Toyota escudo mgumu2 troublemaker Linamo shedede kamtu33 SteveMollel ngushi Donald stewart Mshuza2 Glycel mnonje Ochuanilove SingleFather Santi DEOD 360 ngushi anatory antony ukhuty chris van chicha auxillius Goma Son Hubeb pes KING DUBU VILLAIN mwayena donbeny Aleppo JipuKubwa shoo61 BOMBAY John mungo Nyakageni bato Dogo 1 sufra chamlungu painscott wegman Bravo Engliash MOSELBAY wa stendi FaizaFoxy bigmind cadabraa Internal Kelvin mwalukas mnonje Kelvin X Somoche Wgr30 Miiku Poise Jabman kalamuyamwalimu BOMBAY the say juxhb witnessj Gide MK Mmanyema mgogoone Mnongane Mandingo koncho77 afsa ngaboru Paradoxer Heavy Metal KIMBURU 06 Raaj kichekoh ngumba njeche kikale DullahTza Goodluck Mshana julius Darcy Denis Kasekenya mashonga kitalembwa Khaleed Shaban middle east SirChief jiwe jeusi Mkambarani mansakankanmusa gambada ynwa ney kush
 
Back
Top Bottom