Utata Juu ya Kifo Cha Rais JF Kennedy

Utata Juu ya Kifo Cha Rais JF Kennedy

Nifah Divine... glory to yhwh BansenBurner Alisen Papushikashi Magazine Fire miss chagga SANCTUS ANACLETUS mngony Excel Mussolin5 Jimena Inferiority Complex gwijimimi wambura marwa Hoshea shareef conscious wambeke The Boss Deejay nasmile gkileo Juma chief Mangi flani hivi Ngongo makaveli10 KENZY kadada wa pili Root aretasludovick jonnie_vincy Clkey KAFA.cOm mbewe makedonia Afande Nyati peterchoka Leonard Robert Nchi Kavu STUNTER Chrizo jully Van persie Khalidoun Tetramelyz punje haradari Mazigazi @Alybaba babu na mjukuu platozoom jimmyfoxxgongo Nicodemas Tambo Mwikozi Ls man Heaven Sent sifongo Infantry Soldier haa mym 20acres MTS MarkHilary compos Tembo2 Erick the future nancy1983 Bulah binsaad Fazzaly the wolf everhurt Melvine Mgibeon kijana wa leo samsun Coolant Jagood pacesetter apologize payton George Betram kisengeli Kiranga Jiwe Linaloishi Madame B jay john Guasa Amboni Dinazarde Analyse Diva Beyonce snowhite Mmanu Expected Value onechromosome Missy rose Innocenthezron Immortal_MH Ficus sunola Robot la Matope mamaafacebook II JEKI likikima Compact scorpio me G'taxi YNWA adna yuzo ntamaholo Otorong'ong'o naan ngik-kundie kandukamo1 AFRICA101 mwalidebe Kobe Blaki Womani kalendi savius The Great Emanuel r2ga Ntaluke.N. Transcend Msemachochote Mchumiajuone mwampepec MTOTO WA KUKU Fukara proto cute kawombe zinginary MLALUKO JR Vupu barafu BlackPanther Ntuzu Matola impongo ntamaholo Mkoroshokigoli Deadbody KING easy mahoza Msolo kkenzki deborah1 KIDUDU buffalo44 winlicious riziki Allys MUHUNZI Moses2015 nacktary Liuumi dochivele Renzo @barbers hmjamii mbere TATIANA famicho LUCKDUBE mwanadome Straton memphis ghazar Graph Theory Honey Faith Shunie Slave ddcmanesto zinginary pacesetter Nkanaga KOMUGISHA mikatabafeki johnsonmgaya lee empire wigo MJINI CHAI Asprin mtzmweusi Erasto kalinga Chrizo kichakaa man LULU bike FORTALEZA poleni shibumi ZE DONE umande Edger Sr sir joshua sammoo Roram Password Bavaria hambiliki mwanangu Asili100 Evarist Massawe nice1 Jumong S Rogie 1babake nasreen uberito baest dustless Kilemachocho Tumosa mtembea kwa miguu Debbs Joe scorpnose musacha shibumi seeker of knowledge Simuchi Veni Vidi Vici TUJITEGEMEE abuu garcia Hon Nkundwe Festo Festo marion09 mike2k The dream bro kay vandelintz kirikou1 POINT LOAD lusaka city Dirham Rodcones bato MANCNOO multiphill90 GEORGE Dalali mwanamalundi90 MwaFreeca Roram Ta-kibombo troublemaker mambo KOMUGISHA calabocatz Papaa Azonto Msemachochote Mdomo bakuli tizo1 option dikembe iL Buono fakalava ABDUL KAREEM @Gobe Justine Marack Goodluck Mchika MR UNINFORMED darcity nkasoukumu nG'aMBu thatonegAl kabanga MPARE KIBOGOYO Edward Sambai Rassa mnonje srinavas last king of uscoch proto cute Kennedy krava Rais2020 kbosho Mzee wa BsN sam2000 fuma 999 Bableee dawa yenu The Certified DON SINYORI mij adden




bwii ONTARIO Kobe The Vein Mondray jaxonjaxon successor mzee wa liver sawariya Sitaki ukuda Domhome Mpatanishi MKANDAHARI mtugani wa wapi huyo wealthier cluecell Toyota escudo mgumu2 troublemaker Linamo shedede kamtu33 SteveMollel ngushi Donald stewart Mshuza2 Glycel mnonje Ochuanilove SingleFather Santi DEOD 360 ngushi anatory antony ukhuty chris van chicha auxillius Goma Son Hubeb pes KING DUBU VILLAIN mwayena donbeny Aleppo JipuKubwa shoo61 BOMBAY John mungo Nyakageni bato Dogo 1 sufra chamlungu painscott wegman Bravo Engliash MOSELBAY wa stendi FaizaFoxy bigmind cadabraa Internal Kelvin mwalukas mnonje Kelvin X Somoche Wgr30 Miiku Poise Jabman kalamuyamwalimu BOMBAY the say juxhb witnessj Gide MK Mmanyema mgogoone Mnongane Mandingo koncho77 afsa ngaboru Paradoxer Heavy Metal KIMBURU 06 Raaj kichekoh ngumba njeche kikale DullahTza Goodluck Mshana julius Darcy Denis Kasekenya mashonga kitalembwa Khaleed Shaban middle east SirChief jiwe jeusi Mkambarani mansakankanmusa gambada ynwa ney kush[/USER
 
Hata kama unitag nazinyaka fasta kama umeme
Hahaha hapana chief... hizi tag zinanipa uvivu kuziongeza coz hazifanyi kazi. Watu hawapati notification
Jf wafanyie kazi suala hili kitambi sana nalalamika.
Subscribe kwenye uzi and nifollow... walau inasaidia kupata notification nikipost kitu
 
mkuu unamaanisha hi sio fainale utarudi tena,tunakusubiri.lakini pia kuna files zimeachiwa mwaka huu kuhusiana na kifo cha jfk,kwenye hizo files hakuna jipya lolote au bado hujapata muda wa kuzifatilia
 
The Bold upo vizur big up sana.ile usiwe unachelewa mno k uleta muendelezo.
 
Luna kitabu cha muandishi Erick Jon phelps kinaitwa Vatican Assassins kinaelza vizur Hayo n.a. Kendra mbali .sababu nyingne inayodaiwa pia ilichochea auliwe ni vita ya Vietnam maana alitaka kuikomesha
 
Inasemekana Rais JF Kennedy aliuawa kwa amri ya papa wa kanisa catholic-vatican, unalizungumziaje suala hili
 
UTATA WA KIFO CHA RAIS JF KENNEDY



HITIMISHO


Kama ambavyo nilieleza asubuhi kwamba nitahitimisha makala hii kwa maneno machache sana kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wangu ambazo zilinifanya hata kukatisha muendelezo wa makala hii siku zilizopita.

Lakini naamini tutakuwa tumefikia lengo.


Tuendelee…


Katika ripoti ya The Warren Commision, ile kamisheni iliyoundwa na Rais Lyndon B. Johnson kuna mahala inasema kwamba kuna mtu ambaye alijitambulisha kama "Clay Bertrand" alimpigia simu Dean Andrews Jr. ambaye alikuwa ni mwanasheria wa kujitegemea kwenye jimbo la New Orleans kumtaka apande ndege kwenda Dallas kumtetea Lee Harvey Oswald.

Lakini wajumbe wa Warren Commision wanadai kwamba walihangaika mno bila mafanikio na hawakujua huyu "Clay Bertrand" ni nani na wakafanya hitimisho kwamba hili halikuwa jina halisi bali ni 'alias' ambayo ilitumiwa tu na huyo mtu.

Ilipofika mwaka 1967 mwezi March… mwanasheria wa serikali wa New Orleans wa kipindi hicho aliyeitwa Jim Garrison alifanikiwa kung'amua huyu "Clay Bertrand" ni nani haswa.

Bw. Garrison aligundua kwamba kuna mfanya biashara maarufu sana ambaye alikuwa anatumia "alias" hiyo kwenye jumuiya za watu wanajihusisha na mambo ya ushoga.


Mfanyabiashara huyu maarufu sana miaka hiyo alikuwa anaitwa Clay Shaw.

Huyu alikuwa ni muanzilishi wa shirika la International Trade Mart, ambapo shirika hili lilikuwa na lengo kuu la kuchochea biashara ya kimataifa na makao makuj yao yalikuwa ni New Orleans.

Vile vile nchini Italy Clay Shaw alikuwa ni mjumbe wa bodi ya kampuni ya CMC (Centro Mondiale Commerciale) ambayo ilikuwa ni 'subsidiary' ya kampuni mama inayoitwa Permindex (Permenent Industrial Expositions).

Sasa katika ulimwengu wa Espionage na hata mambo ya uhalifu kuna kitu kinaitwa 'front organisations'. Hizi ni kampuni ambazo zinaanzishwa kwa siri na idara ya kijasusi kwa lengo la kutekeleza maslahi yake pasipo idara husika ya kijasusi kujulikana.

8e7e84f29e87bcbe7f8cc324cf681249.jpg

CLAY SHAW; mwanzilishi nankiongozi wa International Trade Mart na Mjumbe wa bodi ya Permindex na CMC ambazo zote ni 'front organisations' za CIA.

d96db9695b094b5e1195e800fb77fc9e.jpg

Hizi ndizo zilikuwa ofisi za International Trade Mart Organasation huko New Orleans


Kwenye miaka ya hivi karibuni baada ya uchunguzi wa kina na nyaraka nyingi kuvuja imethibitika kwamba kwenye miaka ya 1960s na 1970s, CMC na Permindex zilikuwa zinatumiwa kama 'front organisation' za CIA kwenye nchi ya Italy. Kampuni hizi zilikiwa zinatumika kwa lengo kuu la kupitisha fedha kutoka CIA nchini Marekani na kwenda nchini Italia kugharamia mikakati ya kumuondoa madarakani Rais wa Italia kipindi hicho Bw. Charles de Gaulle ambaye alikuwa na sera za kufungamana mno na urusi na kupinga vikali siasa za kimagharibi.

Katika bodi hiyo hiyo ya kampuni ya Permindex (na CMC) pia kulikuwa na mjumbe mwingine wa bodi aliyeitwa Loius Bloomfield.
Huyu alikuwa ni msomi wa hali ya juu na mfanyabiashara maarufu kutoka Canada ambaye kipindi cha uhai wake alionekana na wengi kama kiongozi wa jamii ya Wayahudi nchini Canada.
Lakini ikumbukwe kwamba, Louis Bloomfield wakati wa vita kuu ya pili miaka ya 1940s aliitumikia idara ya kijasusi ya kimarekani iliyoitwa Office of Strategic Services. Idara hii ndio baadae (baada ya vita kuu ya pili) ilibadilishwa jina na kuitwa Central Intelligence Agency - CIA ambayo tunayo mpaka sasa.
Kwa maneno mengine mjumbe huyu wa bodi ya Permindex alikuwa ni jasusi nguli na hata kampuni yao hiyo (Permindex na CMC) kama ambavyo nimeeleza zilikuwa ni 'front organisation' za CIA.

Kwa hiyo basi kitendo cha mfanyabiashara maarufu Clay Shaw ambaye mwanasheria wa serikali Bw. Garrison aling'amua ndiye huwa anatumia a.k.a ya "clay bertrand"… kitendo chake cha kuwa pia mjumbe wa bodi ya CMC na Permindex inadhihirisha mafungamano yake na CIA na shughuli za kijasusi.


Hivyo basi….

Bila kuogopa mafungamano ya Clay Shaw na CIA, mwanasheria mkuu wa New Orleans Bw. Jim Garrison alimkamata Clay Shaw siku ya March 1, 1967 na kumfungulia mashtaka ya kupanga njama ya kumuua Rais Kennedy. Katika hati yake ya mashataka, Bw. Garrison alieleza pia kinaga ubaga kuwa CIA wamehusika pia kwenye tukio hilo.

Wakati wa kusikilizwa kwa kesi hiyo, Bw. Garrison alieleza mahakama sio tu kwamba Clay Shaw ndiye mwenye kutumia alias ya "Clay Bertrand" ambaye alikiwa anatafutwa miaka yote… bali pia alimleta shahidi wake aliyeitwa Perry Russo ambaye alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa wa masuala ya Bima.
Shahidi huyo alieleza mahakama kuwa alihudhuria tafrija nyumbani kwa bwana mmoja anaitwa David Ferrie ambaye anajulikana kuwa moja ya wapinzani wakubwa wa utawala wa Fidel Castro.
Shahidi akaeleza kuwa akiwa kwenye tafrija hiyo kwa bahati mbaya aliwasikia Clay Shaw, David Ferrie na watu wengine wachache ambao hakuwatambua walikuwa wamekaa chemba wakipeana maelekezo fulani kuhusu mpango huo.

Kesi hii iliunguruma kwa muda wa miaka miwili mfululizo. Lakini ajabu ni kwamba siku ya tarehe 1, March 1969…. Baraza la wazee wa mahakama (Jury) walikaa kwa muda wa chini ya nusu saa na kutoa uamuzi wa pamoja wa kumuachia Clay Shaw kuwa huru dhidi ya mashtaka yote hayo.
Hii ilikuwa habari njema kwa CIA lakini umma ulijawa na hasira na hasira hizi walizielekeza moja kwa moja kwa Clay Shaw.

Mwaka 1974 siku ya tarehe 15 August… Clay Shaw alifariki kwa "Kansa ya Mapafu".
Kama ambavyo Jack Ruby (yule aliyempiga risasi Oswald) naye alifariki kwa "Kansa ya Mapafu" akiwa gerezani. Na msururu mrefu wa kila ambaye alionekana kujua uhalisia wa mauaji ya Kennedy alifariki muda mchache tu katika mazingira ambayo yanazua maswali mengi.


Huwa sipendi kutoa hitimisho la moja kwa moja katika makala zote ninazo andika… napendelea msomaji asome, aone 'facts' na kisha yeye mwenyewe binafsi afanye hitimisho lake. Lakini katika tukio hili la mauaji ya Rais JF Kennedy, CIA hawawezi kuruka ukweli kwamba mikono yao ilimwaga damu yake.

Tutajifunza mengi zaidi siku tukianza kuchambua kifo cha ndugu yake JFK aliyeitwa Robert Kennedy maarufu kama "Bobby" ambaye kipindi cha utawala wa kaka yake JFK… yeye (Robert) alikuwa mwanasheria mkuu wa Marekani na kipindi anauwawa alikuwa kwenye kampeni za Urais ambazo zilikuwa na kila dalili ya kushinda kiti hicho.

Ila kwa kisa hiki cha mauaji ya Rais Kennedy tutaishia hapa.



MWISHO


b58a7cd3323fa8604ee12794722b88f0.jpg

JIM GARRISON; Mwanasheria Mkuu wa Serikali jimbo la New Orleans ambaye alithubutu kumburuza mahakamani Clay Shaw na kuinyooshea kidole CIA kuhusika na kifo cha Rais JF Kennedy.



The Bold - 0718 096 811
To Infinity and Beyond

Nifollow, subscribe and nifuate whatsapp
 
Back
Top Bottom