mkulungu mkuyengo
JF-Expert Member
- Feb 5, 2015
- 786
- 566
dunia sio mbaya na haijawahi kua mbaya ila viumbe vilivyomo! tuongelee hiki kiumbe binadamu chanzo cha yote ni tamaa,kivipi? tuchukulie mfano upo bongo mbagala chumba kimoja cha hovyo tu unapiga mishe za kila siku kibishi siku nyingine bilabila siku nyingine unga unga siku zinasonga lakini unatamani one day yes umiliki nyumba yako hata room tatu atleast na ka-harrier kamoja freshi,lakini wakati wewe una mawazo na ndoto ya kumiliki vitu hivyo na fursa huzioni na hata kama unaziona huzipati sababu watu washakaba kitambo,kuna mwingine ana ndoto ya kumiliki nchi kama hii bongo na fursa anaziona,kuna mwingine ana ndoto na mawazo ya kumiliki dunia nzima hii na fursa anaziona na anaamini inawezekana,hapo ndipo kilipozaliwa kitu siasa! sasa watu dizaini hiyo wapo katika harakati za kutimiza ndoto zao kikwazo chochote kitakachojitokeza lazima kiondolewe fasta kulinda interest zao na targets zao,chunguza jinsi nchi zinavyoendeshwa ,chunguza katiba, chunguza ,mishahara chunguza aina ya elimu inayotolewa mashuleni, chunguza history ya mataifa duniani kuanzia kipindi cha ujima,utumwa,hadi sasa,chunguza masuala ya dini pia,utagundua mengi sana,i hope umenisoma bob.Kuna swali huwa najiuliza,,hivi dunia ndio mbaya au binadamu ndio wabaya?? Kwa fikra zangu nimekuja kuona hata dunia ni mbaya,,tena ndio mbaya ya kwanza na inamuambukiza binadamu.Kwa nini watu wema hawadumu?? Mawazo aliokuwa nayo JFK yangekuwa na matokeo chanya kama angedumu madarakani na kutimiza malengo yake..leo CIA ni kama bui bui ambae kamba zake zimemfunga kila mmoja.Wanaiba,,wanadanganya na kuua.Mkuu The bold Hongera tena kwa maada nzuri,,imeniweka kwenye foleni ya kusubiri.