briophyta plantae
Member
- Feb 18, 2017
- 63
- 62
Kumekuwa na utata juu ya gharama za ujenzi wa uwanja mpya wa mpira jijini arusha, wananchi wamehoji sana na kuonekana kutokukubalina na gharama na hasa wakilinganisha na gharama za Uwanja wa Benjamin Mkapa uliojengwa kipindi cha nyuma 2007 ukiwa na uwezo wa kubeba watu 60,000 kwa gharama ya 64 bilion na hatimaye huu wa sasa utakaobeba mashabiki 30,000 kwa gharama 286 bilion.
Utata huu wote kwa mtazamo unatokana na serekali kutokutoa ufafanuzi wa namna walivyopata gharama hiyo. Ni wazi kwamba serekali inaona hoja na namna ambavyo watu hawajaridhishwa na gharama hiyo kubwa hivyo wanachopaswa kufanya ni kujibu hoja hiyo kwa kutoa ufafanuzi hiyo gharama kubwa kiasi hicho imesababishwa na vitu gani hasa.
Hili jambo halitakuwa sawa endapo serekali haitatoa ufafanuzi na mwisho wa siku utakuwa ni mradi ambao mapokeo yake itakuwa sio kwa kupenda kwa watu bali mapenzi ya serekali yatimizwe..