Utata: Embe lisilo na kokwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Utata: Embe lisilo na kokwa!

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by Mzee Mwanakijiji, Oct 6, 2009.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Oct 6, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  Swali nawaulieni,
  Magwiji mnijibuni,
  Nimetingwa akilini,
  Jibu sijalibaini,
  Embe lisilo na kokwa, ni embe au kimbembe!?
   
 2. Shaycas

  Shaycas JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2009
  Joined: Feb 13, 2009
  Messages: 899
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 45
  Heshima mbele mkuu.Naomba ufafanue shairi hili.
   
 3. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mwanakijiji salaam,natumai u mzima
  Nashika nami kalam,Kujibu uliyosema
  Nitajaribu maadam,ntasema yalo mema
  Embe liso na kokwa,Si embe hata kwa chembe.

  Kuna embe nafahamu,Kokwale lilo laini
  Lipo tangia Adamu,Yaani enzi za zamani
  Lamung'unywa kwa nidhamu,Kung'atwa katu jamani
  Embe liso na kokwa,Si embe hata kwa chembe
   
 4. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2009
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,987
  Likes Received: 691
  Trophy Points: 280
  we ni mubaya bana, unatisha, haya mm - mjibu huyu.
   
 5. SYLLOGIST!

  SYLLOGIST! JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2009
  Joined: Dec 28, 2007
  Messages: 306
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  Embe hili halipatikani mchangani?
   
 6. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #6
  Oct 11, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,364
  Likes Received: 6,396
  Trophy Points: 280
  Naam!
   
 7. M

  Mchili JF-Expert Member

  #7
  Oct 13, 2009
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  He!! si haba, malenga wetu tunao humu, big up
   
 8. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #8
  Oct 13, 2009
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Tulipendalo kulinyonya kabla hatujalichokoa
   
 9. JoJiPoJi

  JoJiPoJi JF-Expert Member

  #9
  Oct 13, 2009
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 2,477
  Likes Received: 1,448
  Trophy Points: 280
  heshima kwako mkuu,
  mkuu usipo kokotoa hii shahiri mimi utakuwa umeniacha mbali sana
   
 10. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #10
  Oct 13, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  Babu yangu Mwanakijiji,katu usitingwe akilini
  Watakuja wengi wajibuji,na majibu yaso kifani
  Haihitaji kumpa mtu mji,ili upate jibu akilini
  Embe lisilo na kokwa,si embe bali kimbembe

  Embe lisilo na kokwa,kamwe haliwezi tokea
  Hata ukienda Rukwa,lenye kokwa watakuelea
  Embe lilo na kokwa,vizuri mtini labembea
  Embe lisilo na kokwa,si embe bali kimbembe

  Amani kweli umenena,kuhusu kokwa lilo laini
  Kwa hakika umenikuna,kwa wako ubeti makini
  Kokwa laini lililotuna,embe lake ni tamu jamani
  Embe lisilo na kokwa,si embe bali kimbembe

  Embe lililo na kokwa,kwa nafasi linanyonywa
  Laliwa pasi kumenywa,na maganda lameng'enywa
  Hilo embe lisilo na kokwa,hata bure huwezi pewa
  Embe lisilo na kokwa,si embe bali kimbembe
   
 11. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #11
  Oct 13, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Mkuu kumbe nawe uko!, safi sana
   
 12. Balantanda

  Balantanda JF-Expert Member

  #12
  Oct 13, 2009
  Joined: Jul 13, 2008
  Messages: 12,322
  Likes Received: 1,039
  Trophy Points: 280
  kidogo kidogo mkuu
   
 13. Mndundu

  Mndundu JF-Expert Member

  #13
  Oct 13, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kuna embe nalo tamu, kwa ndani lajaa miiba
  Lipo taangia adamu, muumba alipotuumba
  Embe hili ni adimu, ukilipata watamba
  Ng`ong`o nalo ni embe, naomba msisahau

  Embe lisilo na kokwa, si tija wala wala kimbembe
  Kwani vingapi vya kokwa, vyafaa kuitwa embe?
  Halifai kwa kunyonywa, bali utapata shibe
  Ng`ong`o nalo ni embe, naomba msisahau

  Ni maarufu mtaani, Wajuvi wataliomba
  Likizubaa mkononi, Wenzio wanalilamba
  Likipakwa chumvini, Vidole utajilamba
  Ng`ong`o nalo ni embe, Naomba msisahau

  Wandugu muwe makini, na dodo chini ya mbuyu
  lazima tilie walakini, usije okota kibuyu
  zoazoa jalalani, muachie mbayu wayu
  Ng`ong`o nalo ni embe, naomba msisahau
   
 14. A

  AmaniGK JF-Expert Member

  #14
  Oct 14, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,101
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 145
  Malenga mmenishika,kusema japo kidogo
  Kuna embe nakumbuka,nilitafuna kigogo
  Kwa kweli nilistuka,japo sikua mdogo
  Hili embe liso kokwa,sijui ni embe gani

  Kwa hamu nilivutika, kulitia mdomoni
  Mkeka akatandika,mwenyeji wangu chumbani
  Mkono akanishika,akanivuta kwa shani
  Hili embe liso kokwa,sijui ni embe gani

  Hili embe lajificha,kulila siwe papara
  Nlikula usiku kucha,tena sio la duara
  Mwenzenu sipati picha,embe si masihara
  Hili embe liso kokwa,sijui ni embe gani?

  Nlibaki nalitafuta,kokwale siku kucha
  Ulimi nikauvuta,nikatumia na kucha
  Mwenyeji akajivuta,akanipa lote bucha
  Hili embe liso kokwa,sijui ni embe gani
   
 15. L

  Lizy JF-Expert Member

  #15
  Oct 14, 2009
  Joined: Feb 11, 2008
  Messages: 413
  Likes Received: 285
  Trophy Points: 80

  Mimi siyo mshairi
  Kumshinda mshiiri
  Vile yeye kasafiri
  Kwa niaba nitakiri
  Embe hilo siyo siri
  Ukila uwe msiri
  Embe lisilo na kokwa, si kimbembe ni embe.

  Ninajua utabisha
  Kwa niya ya kunitisha
  Kuniita napotosha
  Na akili kunichosha
  Sihitaji kujikosha
  Ukweli utakutosha
  Embe lisilo na kokwa, si kimbembe ni embe.

  Linapatikana Pwani
  Kibandani si dukani
  Halijawekwa juani
  Limefichwa barazani
  Lapewa ugredi wani
  Usiniulize kwa nini
  Embe lisilo na kokwa, si kimbembe ni embe.

  Muuzaji mwenye nyumba
  Apenda kugomba gomba
  Ila usije yumba
  Kwa hiyo yake kasumba
  Usije sema waomba
  Kwani ataanza gomba
  Embe lisilo na kokwa, si kimbembe ni embe.

  Nitampigia simu
  Endapo italazimu
  Vile ninamfahamu
  Hawezi kuwa mgumu
  Kumbuka yana msimu
  Kuweka order muhimu
  Embe lisilo na kokwa, si kimbembe ni embe.

  Hutakiwi kuongeza
  Moja litatosheleza
  Vinginevyo kujikweza
  Utajuta endekeza
  Kiasi inapendeza
  Hasa wakati wa kiza
  Embe lisilo na kokwa, si kimbembe ni embe.

  Sasa lini utakuja
  Liandaliwe hilo moja
  Onyo! Usijelifuja
  Likageuka kioja
  Embe moja kwa mmoja
  Usije fanya ‘Umoja'
  Embe lisilo kokwa, si kimbembe ni embe.
   
 16. Mndundu

  Mndundu JF-Expert Member

  #16
  Oct 14, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 225
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Kuuliza si ujinga, Ulilia Mkuranga?
  Maana pwani kwa vibwanga, wanajua kuvipanga
  Mzinga utauchonga, lapwani likishanoga
  Si Dodo wala sindano, mwenzetu ulilokula

  Chumbani si sebuleni, mgeni ulitengewa
  Ukawekwa mtegoni, bila hiyana wanaswa
  Taratibu safarini, katika kusaka kokwa
  Si Dodo wala sindano, mwenzetu ulilokula

  Mwenyeji kwa ujasili, mkekani makusudi
  Embe lake kama mwali, pekeyo kakukabidhi
  Kwa kucha pia ulimi, binamu ulifaidi
  Si Dodo wala sindano, mwenzetu ulilokula
   
Loading...