Venus Star
JF-Expert Member
- Dec 6, 2018
- 19,680
- 59,799
Embe dodo ni aina ya maembe ambayo ni matamu sana. Watu wengi hawajui namna ya kula tunda hili kwa raha na kistaarabu.
Leo katika uzi huu nitaeleza namna ya kula embe hili.
UTANGULIZI
Embe dodo linaweza kuliwa likiwa limeiva au likiwa bichi. Na wakati mwingine embe dodo likiwa bado changa linatumiwa kwa kutengeneza chachandu au mboga. Kwa upande wa matumizi ya chakula embe hili linamatumizi mengi sana.
Embe hili ukila kwa pupa unaweza uchajichafua mdomo au kuchafua nguo zako kabisa. Maana likia limeiva vizuri, embe hili huwa linatoa juisi nyingi. Kwa hiyo ukila kwa pupa unaweza kujikuta unachafuka bila sababu.
Uzuri nchi yetu ya Tanzania embe dodo linapatikana kila mkoa. Na kuna sehemu embe hili huwa linakuwa na nyuzi nyuzi nyingi. Kwa upande wa Afya nyuzi nyuzi hizi husaidia kusaga chakula tumboni.
Embe hili unaweza ukalila kwa kunyonya na baadae ukala maganda yake hakuna shida kabisa. Lakini unaweza ukalikata kata kwa kisu na kuweka kwenye sahani safi na kula.
MUDA GANI UNAFAA KULA EMBE DODO?
Inategemea unakula embe la namna gani. Maana nimesema hapo awali kwamba embe dodo linaweza kuliwa likiwa limeiva, likiwa bichi au likiwa changa.
Embe dodo likiwa changa: Embe hili likiwa changa mara nyingi linakuwa na uchachu na uteute mwingi. Kwa hiyo siyo vyema kula embe dodo likiwa changa. Embe dodo changa linatumiwa kutengeneza chachandu au mboga.
Unatakiwa uchume embehilo vizuri kisha ulioshe na maji safi. Halafu weka kwenye chombo safi. Kisha ondoa maganda yake taratibu. Kama unataka kutengeneza chachandu katakata vipande vidogo vodogo. Changanya na pili pili. Weka chumvi kwa mbali. Kisha injika kwenye jiko. Pika kwa taratibu mpaka uone embe hilo limelainika.
Nitaendelea......