Janjajanja ya wakatisha tickets za kuingia Magufuli Bus Terminal

Apr 29, 2022
5
3
Mara kadhaa nimekuwa nikiingia kituo kikuu cha mabasi ya mikoani D'Salaam (Magufuli Bus Terminal).

Kinachofanyika kwa baadhi ya wanaochukua ushuru wa kuingia mule ndani kimeniacha na maswali.

Unapofika getini na kulipa pesa ili kuingia ndani, baadhi ya wakusanya ushuru wakishirikiana na walinzi wa getini wamekuwa na tabia ya kutoa risiti lakini risiti hiyo wanapoitoa hawakupi wewe mlipaji ila badala yake hupewa mlinzi ili aichane.

Utapohitaji kupewa hiyo risiti unaambiwa hairuhisiwi wewe kupewa. Wakati mwingine wanakwambia tunaichana sisi (wao) ili kuzuia uchafuzi wa mazingira pale kituoni.

Binafsi naiita hii ni JANJAJANJA maana kwa risiti ambazo hutolewa kwa pamoja zisizoonyesha muda halisi wa mtu alipoingia, hii inatia ualakini.
 
Alafu wale mgambo wa geni kuna siku nilikuwa naingia pale stendi nikawaonyesha tiket ya basi nalosafir wakaniuliza tiket umekatia wap nilishindwa kuwaelewa wamekaa kimchongo chongo sana pale getini.
 
Alafu wale mgambo wa geni Kuna siku nilikuwa naingia pale stendi nikawaonyesha tiket ya basi nalosafir wakaniuliza tiket umekatia wap nilishindwa kuwaelewa wamekaa kimchongo chongo Sana pale getin
Hata mi nishaulizwa hili swali, ubungo haya mambo ya kuulizana hayakuwepo
 
Back
Top Bottom