Hance Mtanashati
JF-Expert Member
- Sep 7, 2016
- 25,834
- 35,852
Hii inawezekana je?Unaweza kukuta kazi ambayo wewe ungeenda kulipwa hata milioni 5 ,ubao unageuzwa unalipishwa mara mbili yake ,ukijifanya mjuaji zaidi unaenda kuozea jela.
Unatengenezewa kesi kulingana na mazingira ili usilipweHii inawezekana je?
ChaiUnatengenezewa kesi kulingana na mazingira ili usilipwe
Mfano unaweza ukatenenezewa kesi ya kuiba nondo, simenti nk.
ChaiHuu uzi unawahusu mafundi aina zote haswa mafundi ujenzi.
Usione watu wana miliki nyumba zaidi ya 10 ukadhani zote wamejenga kihalali kumbe nyuma ya pazia kuna uchafu umefanyika kukamilisha ujenzi huo.
Mchezo upo hivi, tajiri atakuita vizuri atakupa kazi na mtaanza vizuri tu mwanzoni , ila sasa kazi ukishakamilisha ataanza kukutafutia kesi yoyote ili kusudi pesa yako asikulipe , fidia utamlipa na jera usioangalia utaenda.
Utapewa kesi ya upotevu wa mali /wizi. Unaweza ukapewa kesi hata ya ubakaji au kesi aina yoyote ile ili mtokomee na pesa juu mlipe.
Unaweza kukuta kazi ambayo wewe ungeenda kulipwa hata milioni 5 ,ubao unageuzwa unalipishwa mara mbili yake ,ukijifanya mjuaji zaidi unaenda kuozea jela.
Hii inaweza kuwa ni isolated incidence na siyo tatizo kubwa. Matatizo mengi ya ujenzi hutokea kwa mafundi kuwa wakorofi na siyo wenye nyumba kama unavyotaka watu waamini. Na possibly huyo fundi ni kweli aliiba au kiwango cha kazi kilikuwa duni, na sheria zilichukuliwa kwa uhalali. Mafundi wa Bongo ni nani asiyejua matatizo yao? Hapa ni kama umekuja na tahadhari eti abiria wanaibia wapiga debe wa stendiUnatengenezewa kesi kulingana na mazingira ili usilipwe
Mfano unaweza ukatenenezewa kesi ya kuiba nondo, simenti nk.
Mkuu umechambua vizuri sana.Kazi za ujenzi ni ngumu sana na inabidi kuwa na uangalifu sana. Migogoro mingi inahusu malipo na ubora wa kazi. Kuna hatua kadhaa inabidi kuzichukua.
1. Kabla ya kazi kuwa na mkataba ulioandikwa.
2. Kuwe na hesabu ya kazi iliyoandikwa ikielezea kazi zinazotakiwa kufanyika na gharama zake.
3. Malipo yafanyike kupitia benki au miamala ya simu, Malipo yafuatiwe na risiti.
4. Hakikisha kuna mtu wa kati, ambaye ataangalia kazi anaweza kuwa Architect au Engineer. Huyu ana ueleewa kuhusu kazi na anasaidia kutatua migogoro baina ya mjenzi na mwenye nyumba.
5. Kama mwenye nyumba ananunu vifaa, hakikisha usalama wa vifaa na ulinzi uwe juu yake.
6. Mabadiliko yoyote yasifanyike mpaka kwanza bei yake imejulikana kwa pande zote
7. Kata bima
8. Hakikisha unatumia pesa kwa ajili ya kazi na kwa mujibu wa makubaliano
Mjini hapa .Kwahiyo hiyo majumba kumi hujengwa na hela za mafundi? Huu ni uongo
AiseeSitaki kuhalalisha ila kuna kibwana mdogo kimoja ,kilikuja kufunga camera kwenye ofisi na biashara za mnene mmoja .Kufikia wakati wa malipo mnene akaanza kuleta gozigozi .Kibwana mdogo wakakitupa ngome wakadai pia kimekwiba na kimetapeli.Ilibidi tukichangie mpaka nauli ya kurudi Dar.
Ndivyo mchezo unavyokuwa hivyo.Zipo dalili za kuonesha kuwa huyu tajiri/mteja ni tapeli, wanakuwaga na maneno mengi ili umuone ana nia njema. Anaweza kutoa malipo ya awali nusu ukadhani atamalizia nusu iliyobaki. Kazi ikikamilika mgogoro wa madai unaanza