Utapeli mpya kupitia kampuni ya Azam

Utapeli mpya kupitia kampuni ya Azam

hii imemtokea jirani yangu, alikua anatoka Posta mida ya jioni kwenye gari akakutana na jamaa wakapiga stori mbili tatu uyo jamaa akatoa juice mbili akampa jamaa 1 na yeye akabaki na 1 baada ya hapo jamaa alikuja kuzinduka katupwa barabarani kule Mbezi mwisho.Tulikaa siku 3 ndio tukajua hospital aliolazwa jamaa.
Huu utapeli unakua kwa kasi hapa jijini
We acha Tu......
 
Pole shemeji ungeniambia niwaulimbokishe wakome..
Shemeji nimekumis na umsalimie laaziz wangu.
Hahaha sasa si unalala naye mi ni msalimieeeeee. Tena?! Vipi yule WA badoo anayepupu umemuacha?!
 
Lawama hazipaswi jutupiwa kwa azam bali zitupiwe kwa huyo tapeli na jamaa yako mpenda kula kula ovyo vitu vya dezo.

Mbona hayo ni madawa ya kulevya wamemchanganyia kwenye juice, wangeweza pia kumuwekea kwenye ndizi, biscuit, chungwa, soda za kopo nk

Jambo la muhim ni kuepuka kula kula ovyo tena vyakula vya kupewa na watu usiowajua kwenye usafiri wa umma.

Poleni sana,
 
Jamaa yangu amepanda Daladala, akisubiri abiria wajae ili Bus liondoke, baada ya muda anaingia jamaa akiwa amevaa T'shirt ya Azam, Kofia ya Azam, in short yuko uniform kwa Sale na akionekana anafanya kazi Azam, smart vya kutosha.

Jamaa anaingia na kukaa siti ya mbele yake, baada ya muda ananyanyuka na kuja kukaa siti moja na jamaa yangu, baada ya salam na story mbili 3 jamaa akajitambulisha anafanya kazi Azam, jamaa yangu Ana kampuni yake inayojishughurisha na kazi flani, akatumia nafasi hiyo kuuliza mambo flani kuhusu Azam kuona kama anaweza anaweza kupata connection yoyote, baada ya story za hapa na pale mdau wa Azam akafungua begi akatoa Juice ambayo ilikua kwenye Kopo kama la Heineken vilevile, mdau akalifungua akaanza kunywa, akamwambia Jamaa yangu, Azam wana bidhaa mpya, na wao wanapita mitaani kupata Mawazo ya wadau kuhusu bidhaa mpya kabla hawajaingiza sokoni.

Akafungua begi akatoa kopo jingine akampa yangu, jamaa akaanza kusoma Maelezo yote yaliokua kwenye ile label, Ina nembo ya Azam kama kawaida, Jamaa yangu baadaye akaiweka kwenye begi lake akisema ataionja akifika home vile hapendi kulakula njiani, but baadaye akaona atakua hajamtendea haki jamaa, coz mdau angehitaji feedback, basi akaamua kunywa, akamwambia Ni nzuri sema Ina uchachu flani ambao haoni kama Ni mzuri....zilipita dakika kama 10 akazima, kuja kuzinduka baada ya siku 3 wamebeba vitu vya thamani kubwa na pesa, simu n.k jumla 5 millions na ushee!

Police wakamwambia kesi ya aina yako Ni ya 4, Muhimbili walimwambia wewe Ni mtu wa 6 kwa tatizo kama lako!

Tuwe take care Wadau!

Huyo mtu alizima kwenye gari? Kama alizima kwenye gari iliwezekana vipi jamaa am search na kuchukua kila kitu hadi hizo laptop bila abiria kujua?..alitokaje kwenye gari mpaka hospitali?..hebu tusaidie kidogo habari muhimu sana hii iweke sawa tuchukue tahadhali
 
Laptop zilikua kwenye begi moja, simu mfukoni Na pochi mfuko WA nyuma, si unajua gari Ni ya route ndefu, yeye wakati huo alikua kazima tayari, cha ajabu alipanda gari ya K'koo - Tegeta Nyuki, but dereva WA Bodaboda ambaye alimpeleka kwake akisema anamjua, anasema alishushwa Na gari ya Bunju-Makumbusho! Ilikua jioni, kumbuka safari ilianzia K'koo, mwana anasema kumbukumbu zake zilikata Magomeni?
 
Huyo mtu alizima kwenye gari? Kama alizima kwenye gari iliwezekana vipi jamaa am search na kuchukua kila kitu hadi hizo laptop bila abiria kujua?..alitokaje kwenye gari mpaka hospitali?..hebu tusaidie kidogo habari muhimu sana hii iweke sawa tuchukue tahadhali
Huyo mtu alizima kwenye gari? Kama alizima kwenye gari iliwezekana vipi jamaa am search na kuchukua kila kitu hadi hizo laptop bila abiria kujua?..alitokaje kwenye gari mpaka hospitali?..hebu tusaidie kidogo habari muhimu sana hii iweke sawa tuchukue tahadhali

anasema ni jamaa yake tena walipanda gari MOJA it means aliona jamaa mchezo unavyokwenda kwa nini hakumsaidia?
 
Mimi hata kabla ya huu utapeli siwezi na sitaweza kupewa chochote cha kula na mtu nisiyemjua hata kama akinunua naona huwa siwezi kula kwnye gari
 
inayojishughurisha na kazi flani, akatumia nafasi hiyo kuuliza mambo flani kuhusu Azam kuona kama anaweza anaweza kupata connection yoyote, baada ya story za hapa na pale mdau wa Azam akafungua begi akatoa Juice ambayo ilikua kwenye Kopo kama la Heineken vilevile, mdau akalifungua akaanza kunywa, akamwambia Jamaa yangu, Azam wana bidhaa mpya, na wao wanapita mitaani kupata Mawazo ya wadau kuhusu bidhaa mpya kabla hawajaingiza sokoni.

Akafungua begi akatoa kopo jingine akampa yangu, jamaa akaanza kusoma Maelezo yote yaliokua kwenye ile label, Ina nembo ya Azam kama kawaida, Jamaa yangu baadaye akaiweka kwenye begi lake akisema ataionja akifika home vile hapendi kulakula njiani, but baadaye akaona atakua hajamtendea haki jamaa, coz mdau angehitaji feedback, basi akaamua kunywa, akamwambia Ni nzuri sema Ina uchachu flani ambao haoni kama Ni mzuri....zilipita dakika kama 10 akazima, kuja kuzinduka baada ya siku 3 wamebeba vitu vya thamani kubwa na pesa, simu n.k jumla 5 millions na ushee!

Police wakamwambia kesi ya aina yako Ni ya 4, Muhimbili walimwambia wewe Ni mtu wa 6 kwa tatizo kama lako!

Tuwe take care Wadau!

= Inayojishughulisha
 
Back
Top Bottom