Utapeli mpya kupitia kampuni ya Azam

Powder

JF-Expert Member
Jan 6, 2016
4,958
6,555
Jamaa yangu amepanda Daladala, akisubiri abiria wajae ili Bus liondoke, baada ya muda anaingia jamaa akiwa amevaa T'shirt ya Azam, Kofia ya Azam, in short yuko uniform kwa Sale na akionekana anafanya kazi Azam, smart vya kutosha.

Jamaa anaingia na kukaa siti ya mbele yake, baada ya muda ananyanyuka na kuja kukaa siti moja na jamaa yangu, baada ya salam na story mbili 3 jamaa akajitambulisha anafanya kazi Azam, jamaa yangu Ana kampuni yake inayojishughurisha na kazi flani, akatumia nafasi hiyo kuuliza mambo flani kuhusu Azam kuona kama anaweza anaweza kupata connection yoyote, baada ya story za hapa na pale mdau wa Azam akafungua begi akatoa Juice ambayo ilikua kwenye Kopo kama la Heineken vilevile, mdau akalifungua akaanza kunywa, akamwambia Jamaa yangu, Azam wana bidhaa mpya, na wao wanapita mitaani kupata Mawazo ya wadau kuhusu bidhaa mpya kabla hawajaingiza sokoni.

Akafungua begi akatoa kopo jingine akampa yangu, jamaa akaanza kusoma Maelezo yote yaliokua kwenye ile label, Ina nembo ya Azam kama kawaida, Jamaa yangu baadaye akaiweka kwenye begi lake akisema ataionja akifika home vile hapendi kulakula njiani, but baadaye akaona atakua hajamtendea haki jamaa, coz mdau angehitaji feedback, basi akaamua kunywa, akamwambia Ni nzuri sema Ina uchachu flani ambao haoni kama Ni mzuri....zilipita dakika kama 10 akazima, kuja kuzinduka baada ya siku 3 wamebeba vitu vya thamani kubwa na pesa, simu n.k jumla 5 millions na ushee!

Police wakamwambia kesi ya aina yako Ni ya 4, Muhimbili walimwambia wewe Ni mtu wa 6 kwa tatizo kama lako!

Tuwe take care Wadau!
 
Aisee!

Watu kweli wanajishughulisha.

Mimi nashukuru tabia ya kula kula njiani sina.

Nikiona sikuelewi elewi halafu unakuja anga zangu nakutolea mbavuni.

Kwanza sina muda wa kukupa uanze kunitangazia bidhaa yoyote (hata isiokuwa ya kinywaji, kilaji).

Ahsante kwa kutupa tahadhari.
 
Duuh... Weee kweli unapewa m juice kweye gari ati onja, na wewe mzobe mzobe unakunywa...

Kwani wee mkemia wa kiwanda?o_O.. Si apeleke TFDA wakampimie kama inafaa:rolleyes:

Tuacheni kula hovyo hovyo...na kuamini watu tu on the spot haswa vitu vya kula. Unawezapoteza uhai hiv hvi.
 
Mkuu Shukrani Kwa Kutupa Tahadhali Mapema
Ningeomba Mrejesho Wa Jamaa Baada Ya Kutoka Mubimbili Hali Yake Vp?
Police Nao Hatua Gani Wamechukua Kwa Kesi Ya Nne
Sasa hajambo, alipelekwa Dispensary wakam transfer Mwananyamala then Muhimbili, kama moja ya Simu yake ikitumika Bongo atavipata vitu vyake...

Police wanahangaika kukamata Daladala, ila inaonekana Ni mchongo toka alipoenda, coz safari yake town ilijulikana na mdau mmoja ambaye hufanyanae biashara, it means mdau alijua jamaa ataenda na atakua na vitu vya thamani, vitu kama Laptop Mac mpya zaidi ya 2 millions...so binafsi naamini mchongo ulianzia kule
 
Ni story nzur yakufundisha kwan ungesema wamemuibia simu na pesa kwenye wallet ungeshindwa kueleweka mkuu?
 
hii imemtokea jirani yangu, alikua anatoka Posta mida ya jioni kwenye gari akakutana na jamaa wakapiga stori mbili tatu uyo jamaa akatoa juice mbili akampa jamaa 1 na yeye akabaki na 1 baada ya hapo jamaa alikuja kuzinduka katupwa barabarani kule Mbezi mwisho.Tulikaa siku 3 ndio tukajua hospital aliolazwa jamaa.
Huu utapeli unakua kwa kasi hapa jijini
 
Back
Top Bottom