Utapeli mpya kupitia kampuni ya Azam

Utapeli mpya kupitia kampuni ya Azam

hii imemtokea jirani yangu, alikua anatoka Posta mida ya jioni kwenye gari akakutana na jamaa wakapiga stori mbili tatu uyo jamaa akatoa juice mbili akampa jamaa 1 na yeye akabaki na 1 baada ya hapo jamaa alikuja kuzinduka katupwa barabarani kule Mbezi mwisho.Tulikaa siku 3 ndio tukajua hospital aliolazwa jamaa.
Huu utapeli unakua kwa kasi hapa jijini
Ila ni utapeli wa zamani.
Walikuwa wanampa victim wao biscuits.... haswa kwenye magari ya mkoani.

Nashangaa miaka hii mtu analizwa kwa technique zike zile za long.....labda tabia ya watanzania kuamini amini watu hovyo ndio inawaponza.
 
mmh hii ni skendo mbaya sana kwa azam duh wahuni wanaichafua kampuni ya watu
 
Jamaa yangu amepanda Daladala, akisubiri abiria wajae ili Bus liondoke, baada ya muda anaingia jamaa akiwa amevaa T'shirt ya Azam, Kofia ya Azam, in short yuko uniform kwa Sale na akionekana anafanya kazi Azam, smart vya kutosha.

Jamaa anaingia na kukaa siti ya mbele yake, baada ya muda ananyanyuka na kuja kukaa siti moja na jamaa yangu, baada ya salam na story mbili 3 jamaa akajitambulisha anafanya kazi Azam, jamaa yangu Ana kampuni yake inayojishughurisha na kazi flani, akatumia nafasi hiyo kuuliza mambo flani kuhusu Azam kuona kama anaweza anaweza kupata connection yoyote, baada ya story za hapa na pale mdau wa Azam akafungua begi akatoa Juice ambayo ilikua kwenye Kopo kama la Heineken vilevile, mdau akalifungua akaanza kunywa, akamwambia Jamaa yangu, Azam wana bidhaa mpya, na wao wanapita mitaani kupata Mawazo ya wadau kuhusu bidhaa mpya kabla hawajaingiza sokoni.

Akafungua begi akatoa kopo jingine akampa yangu, jamaa akaanza kusoma Maelezo yote yaliokua kwenye ile label, Ina nembo ya Azam kama kawaida, Jamaa yangu baadaye akaiweka kwenye begi lake akisema ataionja akifika home vile hapendi kulakula njiani, but baadaye akaona atakua hajamtendea haki jamaa, coz mdau angehitaji feedback, basi akaamua kunywa, akamwambia Ni nzuri sema Ina uchachu flani ambao haoni kama Ni mzuri....zilipita dakika kama 10 akazima, kuja kuzinduka baada ya siku 3 wamebeba vitu vya thamani kubwa na pesa, simu n.k jumla 5 millions na ushee!

Police wakamwambia kesi ya aina yako Ni ya 4, Muhimbili walimwambia wewe Ni mtu wa 6 kwa tatizo kama lako!

Tuwe take care Wadau!

Kampuni inapozindua bidhaa mpya huita wadau wake na kufanya official launch party ambayo pia wanaalikwa watu mbali mbali kama wataalamu wa sekta hiyo ili kutoa maoni. Haya mambo ya kupeana vikopokwenye mabasi ni utapeli
 
Abiria na wewe mlikuwa mnaangalia anavyokunywa , kulewa na jamaa kufanya vyake
 
Laptop zilikua kwenye begi moja, simu mfukoni Na pochi mfuko WA nyuma, si unajua gari Ni ya route ndefu, yeye wakati huo alikua kazima tayari, cha ajabu alipanda gari ya K'koo - Tegeta Nyuki, but dereva WA Bodaboda ambaye alimpeleka kwake akisema anamjua, anasema alishushwa Na gari ya Bunju-Makumbusho! Ilikua jioni, kumbuka safari ilianzia K'koo, mwana anasema kumbukumbu zake zilikata Magomeni?

Eh! Mchongo huo lakini hapa sidhani kama wametumwa na Azam kama ulivyoandika kwenye kichwa cha habari
 
Duuh... Weee kweli unapewa m juice kweye gari ati onja, na wewe mzobe mzobe unakunywa...

Kwani wee mkemia wa kiwanda?😵.. Si apeleke TFDA wakampimie kama inafaa🙄

Tuacheni kula hovyo hovyo...na kuamini watu tu on the spot haswa vitu vya kula. Unawezapoteza uhai hiv hvi.


Very true
 
Eh! Mchongo huo lakini hapa sidhani kama wametumwa na Azam kama ulivyoandika kwenye kichwa cha habari
True, ndo maana nikasema "Kupitia kampuni ya Azam" Ili hata Azam wajue kuna watu wanaiba kupitia Jina la Kampuni Yao.
 
Abiria na wewe mlikuwa mnaangalia anavyokunywa , kulewa na jamaa kufanya vyake
Labda hata alishuka naye njiani akiwa hajitambui, ama alisubiri abiria wapungue, coz hata nauli alilipiwa Na ticket aliikuta mfukoni!
 
Aiseee.... kama kipande za move kimetengenezwa vile. Lijuis linatole kwenye mkoba harafu lamoto na joto hii unapokea na kuanza kufakamia.. sjapenda hii tabia lkn kama mzima mpe pole mwambie aacha tabia ya kupokea vyakula kwa mtu asiyemjua.
 
Inakuwaje unapewa kitu kwenye daladala unakubali?
 
Mkuu hebu tueleze sie tujifunze
nimeghairi ila namshukuru mungu nilizima home siku 2 ka`zini natafutwa sipatikani maana niliibiwa pochi kwa ujumla wake wakasaka kwenye file langu wakaktuta namba ya bi mdashi ikabidi mama ampigie baba wa mtoto wangu. akawapigia majirani bahati nzuri nilizimia sebuleni bila kufunga mlango ... wakanikuta nimekuwa mweusii nadhani nililishwa sumu ya kutosha nikaenda kuflash sumu mwilini maana nilibadilika kabisa ... na nikawa kama naelea angani wiki mzima sikuwa sawa mawenge na maumivu makali sana ya kichwa
 
Ila ni utapeli wa zamani.
Walikuwa wanampa victim wao biscuits.... haswa kwenye magari ya mkoani.

Nashangaa miaka hii mtu analizwa kwa technique zike zile za long.....labda tabia ya watanzania kuamini amini watu hovyo ndio inawaponza.
Wameuboresha sasa, Ni vizuri watu wakataadharishwa....believe me Kuna watu tumezuia kuibiwa kwao kupitia hili bandiko, watu tumetofautiana, uwezo wa kuchanganua mambo, kufikiri n.k tupo tofauti, nani anaishi Dar hapa Adult ambaye hajui karata 3 Ni utapeli??? But raia wanaibiwa everyday! Wakiongozwa Na Wamama!
 
nimeghairi ila namshukuru mungu nilizima home siku 2 kzini natafutwa sipatikani maana niliibiwa pochi kwa ujumla wake wakasaka kwenye fle langu wakaktuta namba ya bi mdashi ikabidi mama ampigie baba wa mtoto wangu wakapigia majirani bahati nzuri nilizimia sebuleni bila kufunga mlango ... wakanikuta nimekuwa mweusii nadhani nililishwa sumu ya kutosha
So ulifanikiwa kufika home? Issue ilitokea home, Kwenye daladala au mtaani?
 
Back
Top Bottom