kwanza kabisa if you are smart and informed, mi naona ni ngumu kutapeliwa na hawa mabwana! Eti dawa inahitajiwa na unhcr kwa ajili ya kuhifadhi chakula! Shirika linalohusika na chakula duniani si unhcr, ni un-wfp, hata kambini wanaotunza chakula ni wao wala si unhcr. Unhcr wanahusika kugawa non-food commodities, mahema/turubai, mashuka, nguo n.k
kitu kingine, si kwamba wana-wazungu et wanaongea kiingereza fasaha!, jamani mmemsahau steeve nyerere anayeigiza sauti ya bush, obama, marehemu sadam hussein na sarkozy! So suala la kuiga lugha na kujifanya mzungu, mkenya ama mganda, sio issue ni kuiga tu!
Kuna suala la line ya simu eti inadisplay code za uganda ama kenya. Hata wewe ukienda na voda ama zain ya tanzania ukiwa kenya ama uganda itaonesha uko tanzania. So hawa watu wanatumia line za nchi hizo tu na si kwamba wako huko, wako sinza tu hapa dar.
Beware again and again!!!!!!!!!!!!!!!!!!!