Katikomile
JF-Expert Member
- Jul 12, 2007
- 471
- 74
Jamani Kuna utapeli mpya umezagaa katika jiji la Dar Es Salaam. Ambapo unaweza kupokea simu kutoka kwa mtu ambaye hukueleza data zote zinazoonyesha anakufahamu kweli kweli (including habari za ndugu zako, mahusiano yako na watu kadhaa, shule ulizosomea kama ni nje au seminar workshops etc). Kisha hujieleza kuwa anafanya Mashirika ya Kimataifa na kwamba ana deal. Kwa hiyo hukupa business proposal eti Shirika analofanyia (mfano UNHCR) wana vyakula vvinavyohitaji madawa kuvihifadhi ili visiharibike.
Aidha, husema maboss wake ni wazungu wapo Uganda, Kenya ama Sudan. Pia husema kuwa aliyekuwa anawa-supply madawa ameenda Marekani, Uingereza. Kwa hukuomba umpigie ili akupe details. Ukipiga simu hiyo itakuwa inaingia kwenye voice mail etc. Ukiwa-contact watakwambia subiri watafute mtu mwingine aliyekuwa anafanya shughuli hizo na yule wa Mwanzo. Baadaye watakutumia namba ya huyo mtu na kukutaka uje Dar kufuatilia deal hilo.
Wakati wote huo watasema fedha za kununua dawa hizo zipo. Hivyo watakwambia uwasiliane na contact person Dar ES Salaam ili akupatie sample uzipeleke airport (JKNIA). Sample ya chupa mbili za dawa inaweza kuwa $ 10,000 mpaka 12,000. Kama umeshaingizwa mjini (mfano 100 pcs @ $6,000 = $ 600,000 hukifikiria wewe hutanunua kwa $500,000) unaweza kuhaha kulipia $ 10,000 kwa ajili ya samples ukijua uta-win maisha baada ya kukamilisha deal.
Cha kushangaza watu hawa matapeli ukishalipa dola hizo say 10,000 unachukua sample ambazo ni kanyaboya (Uhuni mtupu hamna kitu). Ukitaka proof nenda Oysterbay Police utakuta machupa kibao ya aina hiyo ambayo watazania kibao wameshalizwa michuzi yao. Kwani ukiachana na huyo anayekupa sample ukifika airport humkuti mtu na simu zote zinakuwa hazipatikani.
Jamani kama kuna watanzania mnafikiri kuwa unaweza kuvuna bila kupanda acheni hizo. Ushahidi jamaa yangu ilibaki kidogo aliwe mchuzi wake machale yakamcheza akachukua askari kanzu pale O-bay polisi. Wakamkamata huyo kijana mmoja hapo MLIMANI CITY. Aliwekwa ndani kwa masaa na baadae nafikiri polisi nao walimtoka michuzi wakamuachia na kumwambia jamaa yangu hana kesi kwani alikuwa hajaibiwa. Naamini kuna watanzania kibao wameshalizwa.
Please if possible share this information.