Utapeli mkubwa DSM: Beware

Kuna rafiki yangu mmoja (binti) wamempiga milioni moja na laki tisa.. alisubiri hapo Airport mpaka amekoma hakuna cha mzungu kutokea wala nini... na hela yenyewe alikua amekopa.
...Nini uvivu wa kufanya kazi au???
 
Hivi, mtu akikuambia anakufahamu anakutajia na majina ya watu wako wa karibu sijui ndugu zako, birthday yako, ya baba yako, jina la mbwa na paka wenu, na nyumba yenu, on top of that ni "mzungu", halafu wewe HUMJUI na wala maishani mwako hujawahi kumsikia, hii yenyewe tayari inatosha kabisa kuwa na wasi wasi.
 
Dah mm kuna kakaangu kaingizwa mjini juzi juzi hapa yaani walimtoa Mbeya wakaja kumtapeli Bagamoyo $25,000 hivi hivi ili fika kipindi jamaa wanamkamua anaishiwa anarudi tena Mbeya kukopa mke wake anamzuia lakini wapi anasema kuna bonge la dili mm mara ya mwisho nilimwona Sinza nikataka kumwokoa kwa kumpigia cmu akiwa na hayo matapeli jamaa alikana kama yupo Sinza dah nilichoka sana wakati namwona kabisa ana katisha barabara baada ya masaa 4 kupita ananipigia cmu ndio nilikuwa mm.

Hii kali, au jamaa wanatumia na nguvu za giza?
 
Just be careful. Usipende maisha mteremko. There is no such a thing called..Free Lunch.. sasa wewe ukisikia unatoa kiduchu halafu ukakuwa billionea unakimbilia. Hizo ni jinsi ya kuwapata watu wenye tamaa mbaya. You can't be a the top of Kilimanjaro without starting the journey at the bottom available entry point and climb slowly through the hillys and gullies route to the top. Tuacha kuota maisha bora overnight. It will never be there. It is a process and has steps. Asante sana Mjasiriamali kwa ku-share.

Ni kweli kabisa, mara nyingi kama si zote "shortcuts are wrong". Tutumie vyema elimu zetu, akili zetu na nguvu zetu kufanyakazi kwa bidii kujiletea maisha bora.
 
Hii kali, au jamaa wanatumia na nguvu za giza?
Ndivyo inavyosemekana. Ila kufanikisha hii sanaa kupitia simu napata shaka.
Inawezekana mhanga ni mtu aliyewahi kupelekwa kwa waganga? (Kuchanjwa hivi na mambo kama hayo?)
 
Ndivyo inavyosemekana. Ila kufanikisha hii sanaa kupitia simu napata shaka.
Inawezekana mhanga ni mtu aliyewahi kupelekwa kwa waganga? (Kuchanjwa hivi na mambo kama hayo?)

Mkuu mbwa mvivu... hakuna cha waganga wala nini! yaani wanakutafuta tu kama una tamaa ya pesa lazima uingie kingi! Mi mtu nnayemfahamu wakati anaingizwa kingi ungemuona anavyojitapa kuwa kaukwaa utajiri wa ghafla ungesikia wivu
 
Waungwana huu ni mtandao mkubwa sana,wako smart kimavazi,wanatumia magari mazuri mfano GX 110,mie walitaka kunipiga kwa kuniuzia MERCURY.kabla ya kununua nikaona bora nipate soko kwanza,nikakutanishwa na mnunuzi maeneo ya Lugaro jeshini ambaye alikuwa mzungu Mr Steve toka Ujerumani ambaye pia ni mwezao.Aiyeniokoa ni Mr wangu kwani nilikuwa ninaomba aniongezee cash.Mtandao huu una lugha zao,mfano anayetaka kupigwa wanamwita ZOBA,zoba mjanja mjanja anaitwa Man'gaa,Ukigundua kuwa anataka kupigwa wanasema Zoba limepata MASEKE!!,Wameibiwa wengi sana hata viongozi ambao hawawezi kusema kwa kuona aibu!!!
 
Hivi sijaelewa kitu kimoja wakuu, mtu akikwambia taarifa zako zooote hadi siku uliyopata tohara ndio unatakiwa ukubali kumuamini au ni vipi? kwani kufanya biashara na mtu ni lazima awe anakujua sanaaaaaaa? Uvivu wa kufikiri tu na woga wa kuuliza maswali.
 
Hivi sijaelewa kitu kimoja wakuu, mtu akikwambia taarifa zako zooote hadi siku uliyopata tohara ndio unatakiwa ukubali kumuamini au ni vipi? kwani kufanya biashara na mtu ni lazima awe anakujua sanaaaaaaa? Uvivu wa kufikiri tu na woga wa kuuliza maswali.


Yale yale ya ile deal ya kutoa dola 300 upatiwe kazi, ni kutumia akili tu kama mtu anakwambia atakulipia tiketi kwenda huko kazi iliko na atalipia gharama za visa lakini utangulize dola 300, you dont need to have a PhD kuelewa kwamba hapa unaingizwa mkenge. It is clear that once they get the money they are gone!
 
Waungwana huu ni mtandao mkubwa sana,wako smart kimavazi,wanatumia magari mazuri mfano GX 110,mie walitaka kunipiga kwa kuniuzia MERCURY.kabla ya kununua nikaona bora nipate soko kwanza,nikakutanishwa na mnunuzi maeneo ya Lugaro jeshini ambaye alikuwa mzungu Mr Steve toka Ujerumani ambaye pia ni mwezao.Aiyeniokoa ni Mr wangu kwani nilikuwa ninaomba aniongezee cash.Mtandao huu una lugha zao,mfano anayetaka kupigwa wanamwita ZOBA,zoba mjanja mjanja anaitwa Man'gaa,Ukigundua kuwa anataka kupigwa wanasema Zoba limepata MASEKE!!,Wameibiwa wengi sana hata viongozi ambao hawawezi kusema kwa kuona aibu!!!


Hii ya viongozi na wakuu wa mashirika ya umma imetokea sana, sema wanaona aibu kusema! Hawa matapeli mara nyingi wanawapigia wakuu wa mashirika ya umma ama wafanyabiashara kwa kujifanya mawaziri (wanaiga sauti) na kuwatoa upepo. Sometimes wanadai wameishiwa vocha na wako remote areas kama vile njiani kutoka Dodoma ama jimboni!.watumiwe kama laki mmoja, na kwa sababu unajua ni Mheshimiwa anapiga huhitaji kuhoji sana, ni kuzama mfukoni tu!

Walishawahi kutaka kumliza Tido Mhando wa TBC kwa kudai mpigaji ni waziri yulko Dodoma wakati Tido alirudi jioni hiyo na waziri toka Dodoma, hapo ndo akajua kanyaboya!!!!
 
Story hii ni kweli kabisa. Katika ofisi niliyomo tuna biashara mbali mbali ikiwemo ya fumigation. Mnamo February 09 meneja wa kitengo cha fumigation alipigiwa simu akaambiwa kwamba kuna dawa zinatakiwa kwenda Sudan ya Kusini kwa ajili ya kuifadhi chakula cha UNHCR. Kwamba mtu anayezichukua dawa hizo atatokea UNHCR Ngara mara tu itakapodhibitika kwamba dawa zipo atapanda charter toka Ngara hadi Dar Es Salaam nawakutane airport.

Mimi binafis nilihusika kuzungumza kiingereza na mzungu (mwenzangu hajui kimombo vizuiri) aliyejifanya yuko Ngara na aliniambia tukipeleka madawa hayo airport atatulipa cash hapo hapo na faida ilkuwa kubwa. Dawa zenyewe tuliambiwa zinapatika kwa supplier pale Mwenge na kila chupa $6,000 na zinatakiwa chupa 2. Kwa nini wasinunue direct toka Mwenge? Tukaambiwa supplier wa Mwenge hatoi commission.

Kwa bahati nzuri meneja wa kitengo cha fumigation anafahamiana na watu wa UNHCR hapa Dar ES salaam, kwa hiyo kitu cha kwanza aliwapigia simu kuhakikisha kwamba dawa kama zile ni za kuhifadhi chakula wakamwambia sio. Tena wakamwambia pia kituo cha UNCHR kule Ngara kilishafungwa hivyo tukajua huyo "Mzungu" hayuko Ngara kama alivyodai.

Hata hivyo tukaamua kufuatilia tuone mwisho wake.Tukachukua blank cheque kuelekea Mwenge. Tulipofika Petrol Station ya Bamaga tukaambiwa tusimame pale mtu atakuja na dawa tumpe $12,000 atukabithi dawa. Alipokuja tukaingia kwenye gari yake akatuonyesha "dawa". Tukamwambia tunalipa kwa cheque akarusha. To cut the long story short baada ya hapo simu zilizopigwa na yule "mzungu" akilalamika kwamba yuko tayari airport na nasubiri dawa zilikuwa nyingi mno.

Ni kweli ni mtandao wa hali ya juu wa kitapeli na wazungu wamo!! BEWARE.

Mkuu ulimpoteza mwizi tapeli hivihivi??? Yaani ungeandaa kabisa police au kwa haraka unakamata namba za gari, au unamwambia subiri ukachukue cash kumbe cash yenyewe ni askari kanzu. Siku nyingine usifanye kosa, fanya kweli.
 
Kinachoshangaza ni kuwa hawa jamaa wanapata wapi hizi taarifa maana kwa mujibu wa wadau waliolizwa ni kuwa wanakutajia mpaka namba ya nyumba unayoishi na ikiwezekana mpaka kodi unayolipa na TV uliyonayo kama ni Samsung ama Hitachi bila kusahau birthday ya mdogo wako aliye boarding.... Kwa Dar es salaam huu ni zaidi ya utapeli.

Kinachonishangaza ni kuwa kesi kama hizi zimeripotiwa nyingi tu hapo central na inawezekana baadhi ya watuhumiwa wanafahamika lakini bado huu mchezo unaendelea.Mpaka siku akilizwa waziri ama mbunge ndio watashtuka.

Umesahau kuwa alilizwa makongoro Mahanga?
 
Ni suala la kufuatilia habari tu mkuu na interest! Habari ya Tido Mhando ilirushwa TBC na kuelezea mkasa mzima.


Wanawaibia mazoba na mafala tu. Watu wajanja hawaibiwi.

Nyie woote mlioibiwa ni sawa na wale wanachama wa Deci. Hivi Deci imeishia wapi?

Mitanzania mijinga sana!!
 
Wanawaibia mazoba na mafala tu. Watu wajanja hawaibiwi.

Nyie woote mlioibiwa ni sawa na wale wanachama wa Deci. Hivi Deci imeishia wapi?

Mitanzania mijinga sana!!



Mkuu ungejua watu waliopigwa kwenye hili dili hata usingesema haya... wamepigwa watu na akili zao kisa wameongea na Mzungu kwenye simu!
 
Tunashukuru kwa information kama shule tumeipata ni sisi sasa kuwa makini na hizi deal za harakaharaka na kushilikiana na police inapowekana
 
duh! huu utapeli wa hali ya juu!
ila hapa ile post ya Yo Yo inakuwa direct applied kabisa. Wabongo tunapenda mijipesa mingi pasipo kuvuja jasho sasa ndio haya. By the way hapana sababu ya kuwaona waliotapeliwa kuwa ni mazoba la hasha, haya ni mambo yanayotokea na kupitia these experiences tuna learn ambao bado hatujakumbwa na zahama hili.
Asante mtoa hoja
 
Back
Top Bottom