round kick
JF-Expert Member
- Feb 3, 2025
- 933
- 3,045
NI kijana mdogo mwenye ndoto kubwa ya kufanikiwa kimuziki. Anajiona anaweza, wanaomsikiliza pia wanamwambia anaweza japo hawakosekani wa kumsema kwamba analazimisha fani.
Kuambiwa huwezi ni kitu cha kawaida, maana hata Lionel Messi kuna wenye uthubutu wao husema hawezi. Binadamu utawaweza? Hata Mohamed Dewji ‘Mo’ husemwa kuwa hana kitu, eti ni mali za baba yake. Ndiyo dunia!
Basi kijana mwenye kipaji anasikia maneno ya kumkatisha tamaa, yeye anayafanyia kazi kwa kuandika mashairi yenye kumpa nguvu, wanaita mistari na zile ghani husema ni kuchana, kwa ‘kukopi na kupesti’ lugha ya wenzetu huita ‘kufloo’.
Mwenyewe anachana sasa: “Jifanye unaweka Berlin mimi kibishi nitatoboa, walionitegea ukuta wa Gaza discipline nilishawagea, hivyo vijimaneno shombo vinaongeza kasi napaa, nini wewe, wewe nani kwangu hata Kanye anangojea…” Mistari inampa nguvu, harudi nyuma, kipaji kinazidi kukua.
Mwenye kipaji cha muziki hayupo peke yake, anakutana na wengine safarini. Wanapeana simulizi za Marekani. Kijana mwenye kipaji anaona ili maisha yake ya kimuziki yaende na wakati inabidi ‘akopi’ Umarekani, kuanzia mavazi, vilevi, miondoko na kadhalika.
Kijana mwenye kipaji anapongezwa, anaambiwa ana miondoko ya Kimarekani, wao wanaita Swagger (swaga). Kijana mwenye kipaji hata kabla hajafanikiwa kusikika redioni au kuonekana kwenye runinga, mabadiliko yake yanaonekana waziwazi. Mtu akimuona anajua tu ni msanii.
Inaaminika kuwa msanii ni lazima awe na muonekano tofauti na watu wengine. Msanii kufanana na raia wengine wa kawaida ni kosa kubwa la kiufundi. Lazima ajitofautishe kwa mtindo wa nywele, kuvaa, akizungumza lazima swaga zihusike, ‘yo yo’ ziwepo anapozungumza kwa mseto wa Kiswahili na Kimarekani.
Mwanaume anaweka hereni sikioni, avae suruali na shati au fulana kubwa kumzidi (wakaita oversize), siku hizi mpango mzima ni kutinga vivazi vidogo vya kuwatosha wadogo zao wa shule za msingi, wao na ndevu zao wanavaa halafu wanaita modo. Hiyo ndiyo tabia ya wasanii kujitofautisha!
Kijana mwenye kipaji anazungumza na wenzake kwamba ili uwe msanii mzuri lazima uwe na muonekano wa kisanii kwa kunyanyua vyuma, kutanua vifua na kutengeneza michoro ya mbavu (abs) imara. Wanaita six-pack.
Halafu zile six-pack zikishatokeza ili kuzitendea haki, kijana mwenye kipaji anashauriwa akiwa jukwaani awe anafanya maonesho yake kifua wazi, eti ndiyo mashabiki watamuona mjanja zaidi, kidume hasa mwenye swaga za Kimarekani, vilevile watoto wa kike watampenda maana hudatishwa na vifua vipana pamoja na six-pack.
Kijana anaendelea kufanyia kazi maono ya Kimarekani na ujana kama anavyopokea kutoka kwa wasanii wenzake. Wengine anaokutana nao wanavuta bangi, wakiwa pamoja wanavuta yeye analewa moshi. Anawasikia wanaovuta wakizungumza: “Mwanangu hiki kitu cha Tarime nikikikung’uta napata stimu za ki-Jay Z kabisa.”
Mwingine naye anajibu: “Cha Arusha mwanangu huwa kinanipa hisia za ki-BIG.” Kila mwamba ngoma huvutia kwake, yupo mwenye kusema: “Zote hizo cha mtoto, mzigo wa Makete unanifanya nabembea kama mtu mzima Snoop Dog.” Mpenda cha Tabora naye anatoa sifa: “Ukitaka uchane kama Tupac gonga cha Tabora.”
Kijana mwenye kipaji anasikia mapambio hayo, anaona wenzake wanafaidi. Anaamua kufanya majaribio ya kimoja kwenda kingine. Ndani ya siku moja anapuliza cha Makete, Tarime, Tabora, Arusha na Mbeya. Matokeo yake anakuwa mvuta bangi kuliko waliomfundisha.
Akiwa anavuta bangi zake, anaingia studio anatengeneza wimbo mzuri unafanya vizuri redioni na kwenye televisheni. Kijana mwenye kipaji anakuwa maarufu, redioni anatajwa yeye, runingani yeye. Mashabiki wanapiga simu kuomba wimbo wakae uchezwe. Anapata shoo nyingi zinampa pesa nyingi harakaharaka. Anavimba kichwa, anaamini bangi ilikuwa na nafasi kubwa ya kumfikisha alipo.
Kijana mwenye kipaji haishi dunia ya peke yake, yupo kwenye ulimwengu wa kawaida, anakutana na watu ambao wameathirika na dawa za kulevya, anawaona na anawasikitikia. Yeye anaamini hataweza kufika kwenye hatua hiyo. Anaendelea kupuliza puli zake za bangi kwa kasi kubwa.
Ndani ya studio, kijana mwenye kipaji anakutana na wasanii wengine ambao ni wakomavu wa bangi. Wakati wakifanya yao, anagongea bangi ya msanii mwenzake ile kupiga funda moja la moshi, anaona kitu kipo tofauti mno halafu kinamsafirisha kupita kawaida. Mchanayato wa Jamaica na Mexico.
Anauliza: “Hiki kikali, cha wapi?” Anajibiwa: “Ni cha Arusha kimechanganywa na cha Pakistan.” Anajiona amelewa muda wote. Wikiendi akiwa klabu anakutana na msanii mwenzake, anagongea sigara anapewa, akipiga funda moja tu anajiona yupo ‘high’ kupita maelezo, anauliza sigara ina nini, anaambiwa: “Fegi imemiksiwa na mzigo kutoka Colombia.”
Mara kijana mwenye kipaji anajiona kuvuta bangi bila kuchanganya na kitu cha Peru haimpi stimu. Anakuwa mtumia dawa za kulevya. Wakati mwingine anashtuka, anawaambia wenzake: “Jamani haya madude mwisho tutakuwa mateja kama wale wa Kinondoni Manyanya.” Wanamjibu: “Wale wanalanduka halafu hawali, haya mambo uzuri wake unatumia halafu unakula vizuri, huwezi kuwa teja.”
Akiwa na akili hiyohiyo, kijana mwenye kipaji chake ambaye tayari ni supastaa mkubwa, anakuwa anatumia unga kwa kiasi kikubwa akiwa na jeuri ya kauli mbiu kwamba “unanusa unga kisha unakula vizuri.”
Kutahamaki sumu ya unga inajaa kwenye mwili wa supastaa, anakuwa hawezi tena kuishi bila kutumia. Akipitisha muda bila kunusa (ku-sniff) anapatwa na uzoba wa kukosa unga ambao wenyewe wanaita alosto. Supastaa anakuwa alosto.
Anapofikia hatua hiyo, supastaa anapoteza uwezo wake wa kufanya kazi nzuri. Masupastaa wenzake wanamteta kwa kutumiana SMS, kupigiana simu au hata wakikutana wanazungumza kwamba “jamaa kawa teja.”
Kwa vile amepoteza uwezo wa kufanya kazi nzuri kutokana na uteja wake, supastaa taratibu anapotea redioni, anakuwa hasikiki tena. Runingani haonekani na kwa maana hiyo hata mialiko ya ziara za muziki hapati. Supastaa anaishi bila shoo, anakosa pesa.
Supastaa kwa uteja wake anakimbiwa na masupastaa wenzake. Akiwapigia simu hawapokei au wakipokea wanampa majibu ya kumrusha, hawataki kukutana naye, wanamuona amefulia, yupo tofauti na wao.
Maisha bila shoo, supastaa anashuka thamani kwa kasi. Ikitokea bahati akipigiwa simu ya shoo, akipewa pesa siku ya tukio haonekani. Wanasema kaingia mitini, kumbe pesa aliyopata yote alitumia kuvuta unga na kulipa madeni ya muuza unga wa rejareja (pusher). Kuanzia hapo mapromota wanaambiana, wanamkwepa, hawampi tena shoo.
Supastaa alikuwa anatengeneza malimioni kwenye kazi zake lakini inafika mahali anakaukiwa kabisa. Alikuwa anamiliki gari na yumba, vyote anauza ili apate pesa za kuvuta unga. Vingine anaweka ‘bondi’lakini vinapotea, maana hana uwezo wa kukomboa.
Anageuka ombaomba, anawapigia simu masupastaa wenzake anawapiga vibomu vya shilingi 20,000 au 10,000 na akipata tu, anakimbilia kwenye unga. Anakuwa mtumwa wa dawa za kulevya. Kula inakuwa siyo kipaumbele chake. Kutahamaki, supastaa anakongoroka mwili. Anakuwa skeleton, mifupa mitupu!
Kwa hatua hiyo, anatamani kutoka alipo anashindwa maana sumu ilishauteka mwili wote. Ni hapo ndipo supastaa huanza kuona anaishi maisha ambayo hayataki. Anateswa na msongo wa mawazo (stress). Unaweza kumkuta peke yake analia, akikutana na anayemjua anamlilia.
Ile hali ya kutengwa na masupastaa wenzake, akiona hata wale ambao alikuwa akiwafunika kwa kazi wanaishi vizuri yeye akiwa amesahaulika, hapati msaada wa kuacha unga, mwisho huamua kujikomesha kwa kujidunga sindano kujiingizia ‘madawa’ kwenye mishipa ya damu. Hali ya uteja inafika hatua mbaya zaidi.
Inafika wakati supastaa anakuwa hajijali, ngozi inapata ukungu na ukurutu kwa uchafu. Haogi na nguo hazifuliwi, supastaa anakuwa mchafu, mwendawazimu. Anakuwa mtu wa maonesho, watu wanasimuliana “jamaa lakini mkali, sijui alishikwa na nini?” Ndiyo hivyo tena, supastaa ameshapotea mazima.
Akihurumiwa na kukaribishwa aketi na masupastaa wenzake anawaibia. Mara anashirikiana na mateja wenzake kuvamia magari ya masupastaa wenzake na kupora power windows, taa na vioo, supastaa anakuwa mwizi. Mabadiliko makubwa, kutoka usupastaa wa muziki mpaka usupastaa wa ukibaka.