Utapeli kwenye uchawi na hatua za kuchukua

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
359,869
Reaction score
828,403
Utapeli unaohusisha uchawi na uganga nchini Tanzania umekuwa ukichukua sura mpya, ambapo matapeli hutumia hofu, imani za kishirikina, na teknolojia kuwaibia wananchi. Kufikia Machi 2026, Jeshi la Polisi na mamlaka mbalimbali zimeongeza jitihada za kudhibiti vitendo hivi ambavyo mara nyingi huleta chuki na uvunjifu wa amani katika jamii.

Mbinu za Kawaida za Utapeli wa Kishirikina
Ramli Chonganishi na "Kamchape": Hii ni mbinu ambapo waganga feki hudai kutambua wachawi au vifaa vya uchawi kwenye makazi ya watu. Mara nyingi hulazimisha watu kutoa mifugo (kama ng'ombe) au fedha ili "kusafisha" nyumba, jambo ambalo limepigwa marufuku kisheria.

Utapeli wa Mitandao ya Simu:

Matapeli hujifanya waganga maarufu na kutuma ujumbe mfupi (SMS) au kupiga simu wakidai kumuona mhusika ana matatizo ya nyota, mikosi, au amelogwa. Huwataka wahanga kutuma fedha za "dawa" au "kafara" kupitia mitandao ya simu.
Chuma Ulete na Utajiri wa Haraka:

Matapeli huwahadaa wafanyabiashara kuwa fedha zao zinachukuliwa kishirikina (Chuma Ulete) na kuahidi kuwapa dawa za kuongeza mauzo au utajiri wa miujiza, hali inayopelekea watu kupoteza akiba zao kubwa

Kutumia Hofu ya Vifo au Maradhi:
Baadhi ya matapeli huwashawishi watu kuwa vifo au magonjwa kwenye familia yamesababishwa na ndugu wa karibu (kama wajane au vikongwe) ili wapate nafasi ya kutoza ada kubwa za "kinga".

Hatua za Kuchukua na Sheria

Ripoti Utapeli: Ikiwa umepokea ujumbe au simu ya kitapeli, unaweza kuripoti kupitia Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kuandika neno UTAPELI na kutuma kwenda namba 15040.

Sheria ya Uchawi (Witchcraft Act):

Sheria nchini inakataza vitendo vya kishirikina vinavyosababisha hofu, madhara, au vifo. Jeshi la Polisi (kwa mfano mkoani Mwanza na Rukwa) limekuwa likiwakamata wanaojihusisha na "Kamchape" au mauaji yanayohusiana na imani hizi.

Waganga Waliosajiliwa:
Serikali inatambua waganga wa tiba asili waliosajiliwa tu. Ni muhimu kuepuka waganga wanaopiga ramli chonganishi ambazo ni kinyume na taratibu za Baraza la Tiba Asili.
 
Hebu nifanyie hizo tricks na mimi mkuu..
Screenshot_20260323-182410~2.jpg
 
Utapeli unaohusisha uchawi na uganga nchini Tanzania
Waganga nuksi. Miaka ya nyuma sana, kabla utandawazi haujangia, nikiwa bado mdogo nilikwenda kumsalimia mjomba wangu. Alikuwa na mgonjwa na akaamua kumpeleka kwa mganga wa kienyeji. Mganga alianza kwa kupiga ramli, ili kujua kinachomsibu mgonjwa. Mbele yake kulikuwa na kibuyu kidogo, kina shanga nyingi, hirizi na manyoya na juu amepachika kijiti ambacho kimeingia ndani ya kibuyu. Mjomba akaambiwa akae mbele. Kibuyu kikaanza kuzungumza kwa sauti ndogo kama mtoto ''logwa, logwa, ndugu, ndugu, Tini, Tini''. Mganga akatoa tafsiri kuwa kimesema amelogwa na ndugu yake anaitwa Martin. Kibuyu kuweza kuzungumza ilikuwa ni ajabu kweli kweli. Fast foward baada ya kukua na kupata akili nikahisi mganga aliweka spika ndogo ndani ya kibuyu halafu aka-connect kwa waya chini kwa chini na kulikuwa na mtu mwengine chumba kingine alikuwa anazungumza,
 
Uwii🤣🤣🤣
Cc: min -me
 
Kuna siku nlikuwa Tanga, natembea mtaani nakuta watu wanakimbizana barabarani, kuna Jamaa kavaa kitambaa chekundu kichwani anakimbia vibaya mno yaani anaruka Tu mitaro mara anaruka katikati kwenye vijiwe vya watu yaani anakimbia Tu hovyo hovyo ikabidi sasa niulize, nikaambiwa Jamaa ameona jini au mnyama (kitu kama hicho kama sijasahau), ndo anakikimbiza hicho kitu na watu kibao wanamfuata nyuma Yake...Nikashangaa Sana.
 
Waganga nuksi. Miaka ya nyuma sana, kabla utandawazi haujangia, nikiwa bado mdogo nilikwenda kumsalimia mjomba wangu. Alikuwa na mgonjwa na akaamua kumpeleka kwa mganga wa kienyeji. Mganga alianza kwa kupiga ramli, ili kujua kinachomsibu mgonjwa. Mbele yake kulikuwa na kibuyu kidogo, kina shanga nyingi, hirizi na manyoya na juu amepachika kijiti ambacho kimeingia ndani ya kibuyu. Mjomba akaambiwa akae mbele. Kibuyu kikaanza kuzungumza kwa sauti ndogo kama mtoto ''logwa, logwa, ndugu, ndugu, Tini, Tini''. Mganga akatoa tafsiri kuwa kimesema amelogwa na ndugu yake anaitwa Martin. Kibuyu kuweza kuzungumza ilikuwa ni ajabu kweli kweli. Fast foward baada ya kukua na kupata akili nikahisi mganga aliweka spika ndogo ndani ya kibuyu halafu aka-connect kwa waya chini kwa chini na kulikuwa na mtu mwengine chumba kingine alikuwa anazungumza,
Nimewahi mtafuta mganga wa mambo ya kazini nikamkuta work mate ndiye mpigq tunguli nikaishia kucheka nikaondoka zangu .

Akaanza kunionea aibu job maana hakuna aliyejua uwa anaijonogeza pia kwenye uganga
 
Hahahaha😂 kuna story nitaisimulia hapa kwa ruhusa ya mhusika! Nimemuona yupo hapa😎
 
Back
Top Bottom