UTAPELI: Kampuni ya D9 (DNINE) ni kina nani? Nani kawapa kibali cha kazi Tanzania?

Jambo hili naliona kama wanaoanzisha wanawajua Wateja wao. Huwezi kugundua kama ni upuuzi mpaka upigwe,

Nakumbuka kuna rafiki yangu alinifuata na biashara ya forever living mwaka 2011 nikakataa kwani niligundua ni biashara ya uchuuzi, huwezi kutajirika kama wanavyodhani, aliwapata marafiki zangu kama kumi, since then yeye sijui kafikia cheo cha director sijui manager vitugani but maisha yake na hao aliowaingiza kwa kupima vipato vyao kwa mwezi ukivijumlisha ndo mshahara nnaopata.

Mwaka 2013 akaja Mwingine na biashara ya Syntek, akidai unaweka kwenye tank la mafuta ya Gari afu consumption ya mafuta inakuwa ndogo, niliwaza kwa makini nikagundua ni upuuzi pia, kwani watengenezaji wa magari wanavyoshindana hii wangeitumia kama competitive edge kama ina maana, jamaa mpaka Leo yuko vilevile anaishi kwa kuota utajiri.
 
Maoni yangu kuna watu wanaweza kuwa wananufaika ila ndio maana ni kwa miezi tisa tu kama sikosei mkataba wao knachokwenda kutokea nnachokiwaza mm ni kwamba wanatengeneza trafiking ya watu kuamini hao wanaopata wanawahamasisha wenzao kwa comfidence zote ndipo makundi kwa makundi yanakwenda kukopa au kutafuta pesa kuingia huko na target yao ni kuona namba kubwa ya watu wanaojiunga kisha wapige hizo viingilio then wasepe sisi tupo tutasikia milio ya raia kwa wale mnaopata hongereni ila kuna wanaotafutwa wapatwe mazima na bora mnaopata kila wiki mtoe msiache humu mpeni huyo cordinator kama mnavyompaga hawapeni cash la mkisema mzifuge humo kwenye system jua kuwa haupo salama kwani huna pa kwenda kuanzia kuweni makini nakushauri wewe uiyejiunga washawishi washkaji sio ndugu wa karibu msije kununiana bure baadae nawakilisha
 
26ae9e47cb43057485a964eac164cebc.jpg
6b449b1532a336c6853c6fa43e8ed873.jpg
utakapo kuja kuifaham wenzako wakati tunamalizia mijengo yetu
 
Na pia usisahau kuwa risk takers wengi ndio huangamia kirahisi.

Kuwa Risk Taker hukukufanyi uwe mjinga kiasi cha kutokujua mbichi na mbivu na kufuata kila Upepo unaokuja mbele yako na kupachikwa jina la "Fursa ya kufanikiwa".

Kabla ya kuamua ku-take any risk basi kwanza jiulinze maswali haya...
1/Una taarifa za kutosha?
2/Uko tayari kupoteza?
3/Hauna namna ya kuepuka hizo risk ili kupata hiyo Fursa?
Mawazo yako ni sahihi. Ni analysis kama hizi ambazo zinatufanya wengi tuishie kwenye kazi za kuajiriwa. We are too wary and concerned of risks rhan the reality.
 
Hii lazima itakuwa janga! alafu serikali nayo ipo kama wezi, muda huu wako kimya baadae watasema biashara hii ni haramu tunaifunga wanachama watarudishiwa pesa zao ambazo ni asilimia 40 tu ndio zimesali. hiyo ndo imetoka kama deci walivyotuacha na risiti zetu hadi leo na pengine pesa zilishatumika kwenye kampeni za chama twawala.
 
duh!
 
Nadhani nimeweka pia hapo chini mambo ya msingi sana kabla ya kuamua kuwa Risk Taker. Kabla ya ku-Take Risk inabidi mtu apime gharama kwanza, sio kuja kupima gharama baada ya kushindwa na kuanza kujutia.
Napenda kuwa mkweli ili sote tupone.

Ni bora kuwa mtumwa wa milele wa kuajiriwa kuliko kuwa Muhanga wa madhira ya kujiajiri kisa tu umepitiwa na upepo wa 'Risk Taking' na kuufuata tu kama mjinga. Risk Taking sio jambo la kubahatisha bahatisha, ni uamuzi kamili huku mhusika akiamini kuna kufanikiwa kabisa huku akiwa amejitoa kupoteza.

Na ukweli mchungu ni huu 'Sio kila anayeamua ku-Take Risk basi anafanikiwa, Wengi wa Risk Taker wameangamia, na wachache wao walifanikiwa Vizuri sana'
 
N
Na Melkizedeck Karol

Maoni haya ni marefu kidogo lakini nimeona niandike kwa urefu ili nieleweke vizuri.

Nimefuatwa mara kadhaa na marafiki wakinitaka nijiunge na biashara inayoendeshwa na kampuni iitwayo D9 Clube. Pia, wapo marafiki kadhaa waliotaka kusikia maoni yangu kuhusu biashara hiyo.

Kusema ukweli, mimi mwenyewe nilivutiwa sana na biashara hiyo licha ya kuwa ukifikiria kwa makini, yapo maswali mengi ambayo nilijiuliza lakini sikupata jibu. Kwa kuwekeza kiasi cha zaidi ya dola 2,000 (zaidi ya million nne), utapata kiasi cha dola 170 kwa wiki, sawa na zaidi ya shilingi million 1 nukta nne za Tanzania kwa mwezi.

Kwa maana hiyo, kwa kuwekeza fedha hizo unaweza kurudisha fedha zako zote ndani ya miezi mitatu na utazidi kuendelea kupekea kiwango hichohicho cha fedha kwa miezi 9 zaidi achilia mbali commission na bonus nyingine nyingi ambatani.
Ikiwa nitajibiwa maswali yangu na kuondolewa hofu, mimi nitakua tayari kujiunga hata kesho. Nina hoja au masuala kadhaa ambayo yanahitaji majibu japo mengine ni madogo madogo lakini naamini ni muhimu;
1. Uzoefu wa D9 Club e
Inakuwaje kampuni iliyoanzishwa tu mwaka jana tena huko Brazili inaaminika kwa kiwango hicho? Inakuwaje rahisi kwa maelfu ya watu kuamua kuwekeza mabilioni ya fedha kwenye kampuni ambayo ndo tu imemaliza mwaka? Kwa uzoefu upi? Kwa rasilimali zipi?
2. Kuhusu usajili wa D9 Clube
Swali lingine muhimu ni kujua uhalali wa kisheria wa kampuni hiyo. Kwanza imesajiliwa hata huko Brazili? Kama ndio, nani anaimiliki? Bodi ya wakurugenzi ni akina nani? Ofisi zake ziko wapi? Au ziko mtandaoni? Anuani yao ni ipi? Kwa kifupi taarifa hizo hata ukienda tovuti (website) wa kampuni hiyo hutazipata. Ukifika kwenye hiyo tovuti unakaribishwa tu na maneno ya kujiunga. Taarifa zao nyingi si public, je, wanaficha nini?

Lakini pia, je, imesajiliwa nchini Tanzania? Je, leseni yao iko wapi? Certificate of Compliance iko wapi? Bodi ya wakurugenzi ni nani na nani? Ikiwa jibu ni kuwa kampuni iko kwenye mchakato wa kuanzishwa, swali je, nani mjinga kiasi hicho akawekeze fedha zake kwenye kampuni isiyosajiliwa? It is madness kuweka pesa nyingi kiasi hicho kwa kampuni ambayo haijasajiliwa.

3. Uhalali wa biashara/Je, D9 Clube wanafanya biashara gani
Moja ya swali muhimu la kujiuliza ni hili. Je, D9 Clube wanatoa wapi hizo fedha watakazo kurejeshea kila wiki au mwezi kama sio DECI part two? Majibu wanayotoa ni kuwa wanafanya biashara ya michezo (sports trading).

Hiyo biashara ya michezo wanaifanyia wapi? Uko wapi ushahidi kuwa wanafanya hiyo biashara ya michezo? Wanafanya na kampuni gani? Ushahidi wa hiyo partnership ukwapi? Hizo hisa wanazinunua wapi? Je, hizo faida wanapata kiasi gani? Iko wapi ripori yao ya mapato na matumizi kwa mwaka mzima wamekua wakufanya kazi? Najua hii ni public company so natarajia nione hiyo ripoti ya fedha.

Ikumbukwe kuwa, moja kazi ya taasisi zinazohusika na usajili wa makampuni ikiwemo BRELA ni kuhakikisha kuwa, biashara inayotarajiwa kufanywa na watu au kampuni husika ni halali na kwa mujibu wa sheria. Si kila biashara ni halali. Pa kuponea ni kuhakikisha kuwa tunawekeza sehemu ambayo ni salama.

4. Biashara ya mitandao
Moja kati ya biashara hatari sana duniani siku hizi ni biashara ya mitandao. Yaani biashara isiyokuwa na ofisi, ofisi ni kwenye mtandao. Ukiangalia watu waliojiunga na D9 Clube wana akaunti kwenye mfumo wa kimtandao ambao unaonesha salio lako na pia mwenendo wa pato lako kulingana na factors mbalimbali. Tukumbuke kuwa mfumo huwo unakuonesha una ela ila sio ela inayoshikika. Mara nyingi na narudia, asilimia kubwa ya watumiaji hao huuziana hizo ela kwenye huo mfumo (sytem), yaani anakutumia kwenye account yako kwenye system wewe unampa cash. Kutokana na kuwa idadi kubwa ya watu hutumia mfumo huo kuzipata fedha zao badala ya B Coin ni dhahiri kuwa asilimia kubwa ya hizo fedha zinaonekana kwenye stytem tu lakini watu hawanazo mikononi. Hii ni tofauti na bank ambapo unaangalia salio na unaweza kwenda kuzitoa bank au kwenye ATM.

Ili kukuonesha jinsi ilivyo hatari, hivi siku mfumo wa D9 Club ukifungwa utafanyeje? Utaenda wapi? Utapaa uende Brazili? Utampeleka nani mahakamani? Serikali na mamlaka zake inaitambua hiyo kampuni? Hapo ndipo utakapojua kuwa ni bora DECI maana wamiliki walikuwa wanajulikana.

5. Kodi
Je, watu hao hulipa kodi ya kipato wanachokipata kwenye hiyo biashara? Mfano ukipata USD170 kwa wiki, unalipa kodi? Umeshawahi kukatwa? Kama hukatwi sio biashara halali nay a kisheria. Play safe, be safe. Siku yakitokea ya kutokea utaeleza ulikua unaingiza shilingi ngapi? Ulikua unalipa kodi? Watu husema wabongo wanapenda vitu short cut na vya uchochoroni. Siku hiyo ikifika utalia na kusaga meno. Huwezi kuwa unapata fedha nyingi hivyo na usilipe kodi. Hata mimi ningekuwa nimejiunga ningetaka nikatwe vizuri tu.

Ushauri
- Kweli hali ya uchumi ni mbaya, lakini tusijiingize kwenye biashara za ajabu kichwa kichwa mwishowe tunaumia. Ubaya wa biashara hii unajikuta unafungua akaunti nyingi kila ili upate nyingi na mwishowe kujikuta umekwisha. Mwenyewe natamani niwekeze nizipate hizo ela tena nikiwa nimekaa zangu mguu juu. Lakini niko salama? Mwenzangu mimi naogopa kufa pressure.
- Kama majibu ya hayo maswahi huna (hata kama ni moja wapo ya hayo masuala niliyoibua), na hujajiunga, usijiunge KAMWE. Upewe hayo majibu na ushahidi. Tena ikiwezekana tafuta maoni ya mamlaka husika kuhusu hilo suala.
- Kama umejiunga tayari, na majibu ya hayo maswali huna, bora tu uzichomoe hizo ela mapema before its too late to apologize. Vunja mifupa wakati meno iko. Zichukue tu usepe.
- Nawashauri mamlaka husika ikiwemo BRELA na Kituo cha Uwekezaji nchini kutoa kauli kuhusu shughuli za kampuni hiyo na nyingine zinazofanya biashara za aina hiyo. Aidha nawashauri TRA kwa kushirikiana na TCRA kufuatila mapato yatokanayo na biashara hizo na kukusanya kodi kama Mheshimiwa Raisi Dr. John Magufuli alivyoagiza kuwa kila mtu anatakiwa kulipa kodi.
- Kama hao waanzilishi (wako gizani) wanasoma maoni haya basi watoe majibu na ushahidi kuniaminisha na kuwaaminisha watanzania kufanya hiyo biashara.
- Mwisho, ikiwa kweli hii biashara ni halali basi nayashauri mabenki yawakopeshe watu wakawekeze huko na marejesho wao yatakuwa wanayapata tu kiulaini. Na baada ya miezi mitano hivi ela yao itakua imerudi kiulaini.
- Wale mlio na mapenzi mema muwatumie wenzenu maoni haya ili wasijetahayarika

Haya ni Maoni yangu, nimeeleza fikra zangu kwa mujibu wa Ibara ya 18 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Sasa uoga wa nini,hujaona wanaume wanavyochukua Maamuzi magumu,hivi ukiwa safarini huoni semi trailer zimelala mtaloni na ni zaidi ya Milioni miamoja.
Nchi hii ukichanganya na akili za watawala itachukua miaka mingi kuendelea.
Watu wa Mexico wametengeneza manati kubwa kuweza kufanikisha kurusha mzigo wa unga kwa zaidi ya kilo moja,hebu fananisha risk taking ability ya wakenya na watanzania nani zaidi.
Ulizaliwa peke yako unapokopa unakopa peke yako jiongeze.
 
Endeleeni kujiuliza wakati wenzenu wanapiga hela. Halafu mtasema magufuli kabana hela. Huwezi kupata majibu juu ya uwekezaji mitandaoni. Utapata maoni zaidi ya 1000. Unadhani matajiri waliopo duniani waliomba mawazo JF? Kwa akili aliyokupa Mungu inatosha kupima na kujua hili ni halali au la. Huku kila mtu anatafuta mkate wa familia yake tu.
Nchi hii ina mambo mengi,kula ukishiba nawa,hiyo serikali si ndo inatimuwa watu wa makazini na ndio hiyo inatupiga porojo za viwanda wakatai gas hawaoni kuwa nacho ni kiwanda,
 
Hii lazima itakuwa janga! alafu serikali nayo ipo kama wezi, muda huu wako kimya baadae watasema biashara hii ni haramu tunaifunga wanachama watarudishiwa pesa zao ambazo ni asilimia 40 tu ndio zimesali. hiyo ndo imetoka kama deci walivyotuacha na risiti zetu hadi leo na pengine pesa zilishatumika kwenye kampeni za chama twawala.
Kufunga hawawezi labda wazime Internet maana kilakitu kipo kimtandaao
 
Alafu wanakua kama mateja kuna jamaa muda wote anaongelea huu upatu tu na kila simu anayopiga ni ya issue hizo tu had anaboa, hajui kuna upatu kama mara 2 hivi umeliza watu nchi hii
 
Never trust them get rich quick schemes,if its too good to be true then it definately aint true.
 
Na Melkizedeck Karol

Maoni haya ni marefu kidogo lakini nimeona niandike kwa urefu ili nieleweke vizuri.

Nimefuatwa mara kadhaa na marafiki wakinitaka nijiunge na biashara inayoendeshwa na kampuni iitwayo D9 Clube. Pia, wapo marafiki kadhaa waliotaka kusikia maoni yangu kuhusu biashara hiyo.

Kusema ukweli, mimi mwenyewe nilivutiwa sana na biashara hiyo licha ya kuwa ukifikiria kwa makini, yapo maswali mengi ambayo nilijiuliza lakini sikupata jibu. Kwa kuwekeza kiasi cha zaidi ya dola 2,000 (zaidi ya million nne), utapata kiasi cha dola 170 kwa wiki, sawa na zaidi ya shilingi million 1 nukta nne za Tanzania kwa mwezi.

Kwa maana hiyo, kwa kuwekeza fedha hizo unaweza kurudisha fedha zako zote ndani ya miezi mitatu na utazidi kuendelea kupekea kiwango hichohicho cha fedha kwa miezi 9 zaidi achilia mbali commission na bonus nyingine nyingi ambatani.
Ikiwa nitajibiwa maswali yangu na kuondolewa hofu, mimi nitakua tayari kujiunga hata kesho. Nina hoja au masuala kadhaa ambayo yanahitaji majibu japo mengine ni madogo madogo lakini naamini ni muhimu;
1. Uzoefu wa D9 Club e
Inakuwaje kampuni iliyoanzishwa tu mwaka jana tena huko Brazili inaaminika kwa kiwango hicho? Inakuwaje rahisi kwa maelfu ya watu kuamua kuwekeza mabilioni ya fedha kwenye kampuni ambayo ndo tu imemaliza mwaka? Kwa uzoefu upi? Kwa rasilimali zipi?
2. Kuhusu usajili wa D9 Clube
Swali lingine muhimu ni kujua uhalali wa kisheria wa kampuni hiyo. Kwanza imesajiliwa hata huko Brazili? Kama ndio, nani anaimiliki? Bodi ya wakurugenzi ni akina nani? Ofisi zake ziko wapi? Au ziko mtandaoni? Anuani yao ni ipi? Kwa kifupi taarifa hizo hata ukienda tovuti (website) wa kampuni hiyo hutazipata. Ukifika kwenye hiyo tovuti unakaribishwa tu na maneno ya kujiunga. Taarifa zao nyingi si public, je, wanaficha nini?

Lakini pia, je, imesajiliwa nchini Tanzania? Je, leseni yao iko wapi? Certificate of Compliance iko wapi? Bodi ya wakurugenzi ni nani na nani? Ikiwa jibu ni kuwa kampuni iko kwenye mchakato wa kuanzishwa, swali je, nani mjinga kiasi hicho akawekeze fedha zake kwenye kampuni isiyosajiliwa? It is madness kuweka pesa nyingi kiasi hicho kwa kampuni ambayo haijasajiliwa.

3. Uhalali wa biashara/Je, D9 Clube wanafanya biashara gani
Moja ya swali muhimu la kujiuliza ni hili. Je, D9 Clube wanatoa wapi hizo fedha watakazo kurejeshea kila wiki au mwezi kama sio DECI part two? Majibu wanayotoa ni kuwa wanafanya biashara ya michezo (sports trading).

Hiyo biashara ya michezo wanaifanyia wapi? Uko wapi ushahidi kuwa wanafanya hiyo biashara ya michezo? Wanafanya na kampuni gani? Ushahidi wa hiyo partnership ukwapi? Hizo hisa wanazinunua wapi? Je, hizo faida wanapata kiasi gani? Iko wapi ripori yao ya mapato na matumizi kwa mwaka mzima wamekua wakufanya kazi? Najua hii ni public company so natarajia nione hiyo ripoti ya fedha.

Ikumbukwe kuwa, moja kazi ya taasisi zinazohusika na usajili wa makampuni ikiwemo BRELA ni kuhakikisha kuwa, biashara inayotarajiwa kufanywa na watu au kampuni husika ni halali na kwa mujibu wa sheria. Si kila biashara ni halali. Pa kuponea ni kuhakikisha kuwa tunawekeza sehemu ambayo ni salama.

4. Biashara ya mitandao
Moja kati ya biashara hatari sana duniani siku hizi ni biashara ya mitandao. Yaani biashara isiyokuwa na ofisi, ofisi ni kwenye mtandao. Ukiangalia watu waliojiunga na D9 Clube wana akaunti kwenye mfumo wa kimtandao ambao unaonesha salio lako na pia mwenendo wa pato lako kulingana na factors mbalimbali. Tukumbuke kuwa mfumo huwo unakuonesha una ela ila sio ela inayoshikika. Mara nyingi na narudia, asilimia kubwa ya watumiaji hao huuziana hizo ela kwenye huo mfumo (sytem), yaani anakutumia kwenye account yako kwenye system wewe unampa cash. Kutokana na kuwa idadi kubwa ya watu hutumia mfumo huo kuzipata fedha zao badala ya B Coin ni dhahiri kuwa asilimia kubwa ya hizo fedha zinaonekana kwenye stytem tu lakini watu hawanazo mikononi. Hii ni tofauti na bank ambapo unaangalia salio na unaweza kwenda kuzitoa bank au kwenye ATM.

Ili kukuonesha jinsi ilivyo hatari, hivi siku mfumo wa D9 Club ukifungwa utafanyeje? Utaenda wapi? Utapaa uende Brazili? Utampeleka nani mahakamani? Serikali na mamlaka zake inaitambua hiyo kampuni? Hapo ndipo utakapojua kuwa ni bora DECI maana wamiliki walikuwa wanajulikana.

5. Kodi
Je, watu hao hulipa kodi ya kipato wanachokipata kwenye hiyo biashara? Mfano ukipata USD170 kwa wiki, unalipa kodi? Umeshawahi kukatwa? Kama hukatwi sio biashara halali nay a kisheria. Play safe, be safe. Siku yakitokea ya kutokea utaeleza ulikua unaingiza shilingi ngapi? Ulikua unalipa kodi? Watu husema wabongo wanapenda vitu short cut na vya uchochoroni. Siku hiyo ikifika utalia na kusaga meno. Huwezi kuwa unapata fedha nyingi hivyo na usilipe kodi. Hata mimi ningekuwa nimejiunga ningetaka nikatwe vizuri tu.

Ushauri
- Kweli hali ya uchumi ni mbaya, lakini tusijiingize kwenye biashara za ajabu kichwa kichwa mwishowe tunaumia. Ubaya wa biashara hii unajikuta unafungua akaunti nyingi kila ili upate nyingi na mwishowe kujikuta umekwisha. Mwenyewe natamani niwekeze nizipate hizo ela tena nikiwa nimekaa zangu mguu juu. Lakini niko salama? Mwenzangu mimi naogopa kufa pressure.
- Kama majibu ya hayo maswahi huna (hata kama ni moja wapo ya hayo masuala niliyoibua), na hujajiunga, usijiunge KAMWE. Upewe hayo majibu na ushahidi. Tena ikiwezekana tafuta maoni ya mamlaka husika kuhusu hilo suala.
- Kama umejiunga tayari, na majibu ya hayo maswali huna, bora tu uzichomoe hizo ela mapema before its too late to apologize. Vunja mifupa wakati meno iko. Zichukue tu usepe.
- Nawashauri mamlaka husika ikiwemo BRELA na Kituo cha Uwekezaji nchini kutoa kauli kuhusu shughuli za kampuni hiyo na nyingine zinazofanya biashara za aina hiyo. Aidha nawashauri TRA kwa kushirikiana na TCRA kufuatila mapato yatokanayo na biashara hizo na kukusanya kodi kama Mheshimiwa Raisi Dr. John Magufuli alivyoagiza kuwa kila mtu anatakiwa kulipa kodi.
- Kama hao waanzilishi (wako gizani) wanasoma maoni haya basi watoe majibu na ushahidi kuniaminisha na kuwaaminisha watanzania kufanya hiyo biashara.
- Mwisho, ikiwa kweli hii biashara ni halali basi nayashauri mabenki yawakopeshe watu wakawekeze huko na marejesho wao yatakuwa wanayapata tu kiulaini. Na baada ya miezi mitano hivi ela yao itakua imerudi kiulaini.
- Wale mlio na mapenzi mema muwatumie wenzenu maoni haya ili wasijetahayarika

Haya ni Maoni yangu, nimeeleza fikra zangu kwa mujibu wa Ibara ya 18 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 
Kujiunga gold member 4m mmmh naona watu wamejiunga ni mwezi sasa ilaaa mmm?

Nijuavyo hizi biashara wanaojiunga mwanzoni upata faida ila wa baadae huliwa.

Tuliliwa rifaro africa sitosahau. Kila la kheri na d9
 
Back
Top Bottom