BoT na CMSA wautahadharisha umma kuhusu Taasisi ya Upatu ya D9 Club

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,259
2,000
Mamlaka imetoa tahadhari kwa umma kwamba, taasisi ijulikanayo kama D9 Club inayotangaza au kushawishi, pamoja na mambo mengine ununuzi wa hisa, inafanya hivyo bila vibali vya mamlaka husika. Kumekuwepo na Michango tofauti kupitia JamiiForums kuhusiana na Taasisi=>D9 Club, upatu unaosambaa kwa kasi Tanzania kama moto wa kifuu.
UTAPELI: Kampuni ya D9 (DNINE) ni kina nani? Nani kawapa kibali cha kazi Tanzania?

Tuwe makini.
IMG-20170614-WA0014.jpg

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) zinapenda kuutahadharisha umma kwamba, taasisi ijulikanayo kama D9 Club inayotangaza au kushawishi, pamoja na mambo mengine ununuzi wa hisa, inafanya hivyo bila vibali vya mamlaka husika.

Ni imani ya BoT na CMSA kuwa ushawishi unaofanywa na D9 Club kwa umma kushiriki katika mpango wao utasababisha watu kupoteza fedha zao, na pia ni kinyume na Sheria ya Makosa ya Jinai Sura ya 16 ya Sheria za Tanzania ambayo katika Fungu la 171A,171B na 171C, ni kosa la jinai kuendesha, kushawishi watu kushiriki, na kushiriki au kuchangia fedha katika upatu.

Ifahamike kwamba upatu haramu hubuniwa kwa namna ambayo fedha za kila mshiriki mpya hutumika kumlipa mshiriki aliyetangulia, na hakuna maelezo ya namna yoyote ya kuwekeza au kuzalisha fedha hizo.

Kwa taarifa hii, umma unasisitizwa kutoshawishika kwa namna yoyote ile kushiriki katika upatu uliobuniwa na D9 Club na mipango mingine ya aina hiyo. Aidha, wananchi watoe taarifa kwa vyombo vinavyohusika, ikiwemo Benki Kuu ya Tanzania, Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana na vyombo vya usalama (Polisi) kuhusiana na mikutano au mafunzo yanayoendeshwa na D9 Club na mipango mingine haramu kama inayofanana na huo.

Imetolewa na:

BENKI KUU YA TANZANIA & MAMLAKA YA MASOKO YA

MITAJI NA DHAMANA

14 Juni 2017

Kwa maelezo zaidi wasiliana na: kanyoni@bot.go.tz & info@cmsa.go.tz
 
ibesa mau

JF-Expert Member
Sep 17, 2015
2,109
2,000
Hii kitu ina miaka na miaka na sijawahi kusikia kwamba mtu analalamika ameibiwa. Kwa hyo ni vema wange eleza ni watu gani waliowekeza huko walio lalamika kuibiwa . vinginevyo ni chuki tu za kutaka wachache ndio watajirike and the rest wabaki . Uzuri wake hii kitu inachezwa mtandaoni sijui kama wataweza. Miezi mitatu ela yako imerudi sasa hapo mtu anatapeliwaje. Mfano mm mwenyewe huu mwezi wa sita , nimerudisha ela yangu miezi mitatu ya mwanzo na sasa nimeshakula faida ya 2m miezi miwili na bado saba. Hapo wakisitisha huduma zao utasrmaje nimeibiwa
 
Siyabonga101

JF-Expert Member
Mar 8, 2016
2,426

Vyombo vya Dola vinahitaji ushirikiano wako katika kutokomeza huo UTAPELI.
 
mjasiliaupeo

JF-Expert Member
Apr 21, 2013
1,965
2,000
Hii kitu ina miaka na miaka na sijawahi kusikia kwamba mtu analalamika ameibiwa. Kwa hyo ni vema wange eleza ni watu gani waliowekeza huko walio lalamika kuibiwa . vinginevyo ni chuki tu za kutaka wachache ndio watajirike and the rest wabaki . Uzuri wake hii kitu inachezwa mtandaoni sijui kama wataweza. Miezi mitatu ela yako imerudi sasa hapo mtu anatapeliwaje. Mfano mm mwenyewe huu mwezi wa sita , nimerudisha ela yangu miezi mitatu ya mwanzo na sasa nimeshakula faida ya 2m miezi miwili na bado saba. Hapo wakisitisha huduma zao utasrmaje nimeibiwa
Umesoma kilichoandikwa lakini? Kama wanafanya upatu bila kusajiliwa kwako ni sawa? Au unafikili hili ni shamba la bibi?
 
MakinikiA

JF-Expert Member
Jun 7, 2017
2,822
2,000
Watupe Data za uzwaji wa madini ya dhahabu zetu mbona hawakuwa na jibu kwenye MakinikiA na Presidaa akasema Bot kuna PhD 17 this is result. . .. ...
 
Root

JF-Expert Member
Jan 23, 2012
38,946
2,000
Aiseee kuna watu wameweka hela zao huko na mie ilikuwa kidogo niweke hela huko
 
Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
17,000
2,000
Washiriki wote wanaojinasibu huku mitaani wajue wanatenda kosa la jinai!
 
Sibonike

JF-Expert Member
Dec 23, 2010
17,000
2,000
Kila baada ya muda fulani DECI inakuja kwa jina tofauti na bado kuna watu wanaingia mkenge
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
13,528
2,000
Hii kitu ina miaka na miaka na sijawahi kusikia kwamba mtu analalamika ameibiwa. Kwa hyo ni vema wange eleza ni watu gani waliowekeza huko walio lalamika kuibiwa . vinginevyo ni chuki tu za kutaka wachache ndio watajirike and the rest wabaki . Uzuri wake hii kitu inachezwa mtandaoni sijui kama wataweza. Miezi mitatu ela yako imerudi sasa hapo mtu anatapeliwaje. Mfano mm mwenyewe huu mwezi wa sita , nimerudisha ela yangu miezi mitatu ya mwanzo na sasa nimeshakula faida ya 2m miezi miwili na bado saba. Hapo wakisitisha huduma zao utasrmaje nimeibiwa
Huu ni utapeli. Kama hujalizwa subiri watakuliza tu (kama wewe si mmoja wao). Uwekeze sh milioni 4 uvune milioni 20 kwa mwaka hizo fedha zinazaaana kama panya? Vitu vingine ni vya kutumia common sense tu na wala si lazima uone mtu aliyetapeliwa!
 
Limon Escobar

Member
Feb 14, 2017
11
45
Yaani sijui nimeelewa tofauti
Mimi nimeelewa hivi D9 club inalipa watu fedha kutokana na watu wanavyo jiunga ikimaanisha kwamba walio jiunga zamani watapata fedha ila kadiri siku zinavyo kwenda wanojiunga watashidwa kulipwa kutokana na kukosekana kwa fedha kwasababu hawajajiwekeza na mitaji yao ni michango ya watu.
Cha pili nimwamba haijasajiliwa haina bima wala dhamana yoyote ile so watch out na kumbuka ukitaka fedha kirahisi unaweza zipoteza kirahisi
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom