UTAPELI: Kampuni ya D9 (DNINE) ni kina nani? Nani kawapa kibali cha kazi Tanzania?

tinkanyarwele

JF-Expert Member
Dec 30, 2016
2,016
1,945
Wana jamvi,

Kuna kampuni inajulikana kama D9(DNINE). Kampuni hii inajihusisha na kuuza tiketi za michezo na masuala ya kubeti.

Kampuni hii mtu anawekeza pesa kiasi fulani alafu baada ya kila juma moja wanaanza kurejesha fedha yako na shughuli zote zinafanyia ONLINE.

Sasa Naomba nisaidiwe kwa Mwenye Uelewa, hawa ni watu genuine au nao matapeli? Vyombo vya Dola vinaichukuliaje kampuni kama hii?

=====

UPDATE 1:

Hii Taasisi imepigwa marufuku na Mamlaka husika. Zaidi soma=> BoT na CMSA wautahadharisha umma kuhusu Taasisi ya Upatu ya D9 Club
 
Kiu na njaa ya mafanikio imesababisha kuibuka na mambo mengi ya kiakili kujipatia kipato.Ikiwemo kitu inaitwa D9 club,ukifatilia origin yake ni Brazil na inafanya kazi kutumia mfumo wa bitcoin ambao hutumiwa sana na drug lords na matapeli wa mtandaoni kwani kupitia bitcoin unaweza fanya miamala mtandaoni bila kujulikana na ukapokea ama kutuma kiwango kikubwa cha pesa.

Hawa jamaa wameingia Tanzania na wanamfumo wao wa kushawishi watu kujiunga kwa kuwaambia kua watakua matajiri ndani ya mda mfupi na maisha yao kubadilika.Na wabongo tunavyopenda slop wengi wamejikuta wakikopa pesa na kuingia huko.

Angalizo kwa serikali yetu ni kulinda wananchi wake kwani itakapo collapse hii system hawa raia hawatakua na pa kwenda kushtaki.
 
Mkuu mimi nikurekebishe kidogo tu. Unaposema Bitcoin ni pesa inayotumiwa na drug lords na matapeli wa mtandao unakosea sana sana.

Mimi ni trader mzuri tu na nimeitumia Bitcoin mara kadhaa hasa kwenye kuinvest na pia katika online payment. Ukiwa unatumia Bitcoin haitapita kwa mtu wa kati kama fedha ya kawaida, itakuwa transaction kati yako na na mtu mwingine. Hutohitaji central bank, Mastercard wala receiver bank, hivyo umeepuka makato yote yasiyo na ulazima.

Hakuna uhalali wa kusema wanaotumia crypto currency wanatafuta njia za kujificha. Leo eBay, amazon, Alibaba, WordPress, overstock nk wote wanapokea malipo kwa bitcoin.

Pia huwezi kusema bitcoin ni scam wakati imekuwa listed kwenye stock markets kubwa zote duniani. Pia usiseme kua ni utapeli, mimi niliexchange dollar kwa bitcoins 6, kipindi hiko bitcoin 1 ilikua ni $716.6. Juzi dunia yote imeshuhudia kwa mara ya kwanza bitcoin ikiizidi thamani Dhahabu na kuwa the most expensive stock in the market. Leo bitcoin 1 inakimbilia 2600 USD.

So niseme kuwa ni vizuri ufanye utafiti mdogo kabla haujapost, ama niseme -usiseme kitu ambacho hauna uhakika nacho.
 
Mkuu mimi nikurekebishe kidogo tu. Unaposema Bitcoin ni pesa inayotumiwa na drug lords na matapeli wa mtandao unakosea sana sana.

Mimi ni trader mzuri tu na nimeitumia Bitcoin mara kadhaa hasa kwenye kuinvest na pia katika online payment. Ukiwa unatumia Bitcoin haitapita kwa mtu wa kati kama fedha ya kawaida, itakuwa transaction kati yako na na mtu mwingine. Hutohitaji central bank, Mastercard wala receiver bank, hivyo umeepuka makato yote yasiyo na ulazima.

Hakuna uhalali wa kusema wanaotumia crypto currency wanatafuta njia za kujificha. Leo eBay, amazon, Alibaba, WordPress, overstock nk wote wanapokea malipo kwa bitcoin.

Pia huwezi kusema bitcoin ni scam wakati imekuwa listed kwenye stock markets kubwa zote duniani. Pia usiseme kua ni utapeli, mimi niliexchange dollar kwa bitcoins 6, kipindi hiko bitcoin 1 ilikua ni $716.6. Juzi dunia yote imeshuhudia kwa mara ya kwanza bitcoin ikiizidi thamani Dhahabu na kuwa the most expensive stock in the market. Leo bitcoin 1 inakimbilia 1300 USD.

mkuu naomba nikutafute kwa maelezo zaidi
 
Absolutely true
 
Kiu na njaa ya mafanikio imesababisha kuibuka na mambo mengi ya kiakili kujipatia kipato.Ikiwemo kitu inaitwa D9 club,ukifatilia origin yake ni Brazil na inafanya kazi kutumia mfumo wa bitcoin ambao hutumiwa sana na drug lords na matapeli wa mtandaoni kwani kupitia bitcoin unaweza fanya miamala mtandaoni bila kujulikana na ukapokea ama kutuma kiwango kikubwa cha pesa.

Hawa jamaa wameingia Tanzania na wanamfumo wao wa kushawishi watu kujiunga kwa kuwaambia kua watakua matajiri ndani ya mda mfupi na maisha yao kubadilika.Na wabongo tunavyopenda slop wengi wamejikuta wakikopa pesa na kuingia huko.

Angalizo kwa serikali yetu ni kulinda wananchi wake kwani itakapo collapse hii system hawa raia hawatakua na pa kwenda kushtaki.
Mbona Nime google Nimeona ni mambo Ya sports betting.
 
Mkuu mimi nikurekebishe kidogo tu. Unaposema Bitcoin ni pesa inayotumiwa na drug lords na matapeli wa mtandao unakosea sana sana.

Mimi ni trader mzuri tu na nimeitumia Bitcoin mara kadhaa hasa kwenye kuinvest na pia katika online payment. Ukiwa unatumia Bitcoin haitapita kwa mtu wa kati kama fedha ya kawaida, itakuwa transaction kati yako na na mtu mwingine. Hutohitaji central bank, Mastercard wala receiver bank, hivyo umeepuka makato yote yasiyo na ulazima.

Hakuna uhalali wa kusema wanaotumia crypto currency wanatafuta njia za kujificha. Leo eBay, amazon, Alibaba, WordPress, overstock nk wote wanapokea malipo kwa bitcoin.

Pia huwezi kusema bitcoin ni scam wakati imekuwa listed kwenye stock markets kubwa zote duniani. Pia usiseme kua ni utapeli, mimi niliexchange dollar kwa bitcoins 6, kipindi hiko bitcoin 1 ilikua ni $716.6. Juzi dunia yote imeshuhudia kwa mara ya kwanza bitcoin ikiizidi thamani Dhahabu na kuwa the most expensive stock in the market. Leo bitcoin 1 inakimbilia 1300 USD.

So niseme kuwa ni vizuri ufanye utafiti mdogo kabla haujapost, ama niseme -usiseme kitu ambacho hauna uhakika nacho.
Acha kudanganya watu, soma hiyo link useme wapi Amazon wanakubali bitcoin!!????
https://www.rewardspay.com/use-bitcoins-on-amazon
 
Mkuu fungua ubongo wako ujifunze sio unakomalia kukaa gizani ndani ya box. Hii ni 1 of the most trusted source -Forbes.

https://www.forbes.com/sites/clareo...-amazon-home-depot-cvs-and-more/#3538340e2de2

Seattle-based bitcoin payment platform iPayYou this week announced a new feature called “Amazon Direct” that lets consumers transfer any dollar amount of bitcoin to use for purchases on Amazon.

“This is the only direct way to purchase on Amazon with bitcoin today,”
 
Lkn haimaanishi unaweza tumia amazon kama unavyotaka aminisha watu.
 
HAYA NDIYO MATANGAZO YAO:

D9 CLUB IN TANZANIA WEKEZA UPATE FAIDA MARA DUFU NDANI YA D9 CLUB

D9 CLUB au D9 SPORT TRADING> ni biashara ya kuuza na kununua hisa za michezo kimataifa ambapo mwanachama anapata faida kila wiki kulingana na hisa zake kwenye kampuni na kukuza pato lake na taifa pia.

Ndani ya D9 CLUB kuna njia mbili za kufanya kazi na kupata faida bila kuathiri majukumu yako ya kila siku nazo

a) kuwekeza hisa zako na kupata faida kwa kila wiki

b) unaweza kufungua akaunti yako kwa dollar 50 tu na ukaanza kufundisha wengine na kupata faida kupitia wao baada ya kujiunga na hisa hizo

ZIFUATAZO NI HISA ZIPATIKANAZO NDANI YA D9 CLUB

-Ndani ya D9 CLUB kuna makundi manne ya hisa na gharama zake kwa kila kifurushi

1.BRONZE zinapatikana kwa dollar $302.

2.SILVER zinapatikana kwa dollar $561

3.GOLD zinapatikana kwa dollar $1070

4.GOLD+ zinapatikana kwa dollar $2086

YAFUATAYO NI MAPATO YA KILA WIKI KWA KILA HISA ZA MWANACHAMA

1.BRONZE unalipwa dollar $12.75 kwa wiki

2.SILVER unalipwa dollar $27.75 kwa wiki

3.GOLD unalipwa dollar 51 kwa wiki

4.GOLD+ unalipwa dollar $170 kwa wiki

Zingatia kila mwanachama anatozwa dollar $50 kama service charge kwa mwezi kutoka kwenye akaunti yake

YAFUATAYO NI MAPATO YA KILA MWANACHAMA KWA MWEZI BAADA YA MAKATO YA MWEZI

Akaunti zote D9 club hukatwa dollar $50 bila kujali ukubwa wa kifurushi chako kwa mwezi

1.BRONZE> $12.75×4wiki= $51-50=$1 kwa mwezi

2.SILVER > $27.75×4wiki=$111-50=$61 kwa mwezi

3.GOLD >
$51×4wiki= $204-50=$154 kwa mwezi

4.GOLD+>
$170×4wiki =$680-50=$630 kwa mwezi

zingatia malipo yote haya hufanyika kwa dollar tu

NAMNA YA KUTOA PESA KWENYE AKAUNTI YA D9 CLUB KWENDA AKAUNTI YAKO YA KAWAIDA

Zipo njia kuu nne za kutolea pesa kwene akaunti ya D9 CLUB nazo ni kama ifuatavyo
a)Bit coin (XAPO)
b)Skrill
c)Neteller
d) Box base
njia ya ziada ni kutumia member to member method

Pia kwenye D9 club waweza kufungua akaunti uwezavyo kulingana na nguvu ya mtaji wako​
 
Back
Top Bottom