Khantwe
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 62,099
- 127,837
Habari zenu wana-chitchat.
Utani ni kitu cha kawaida katika maisha ya kila mwanadamu na na mara nyingi huweza kuunganisha watu mkafahamiana na kufurahi pamoja. Lakini kuna wakati mwingine unaweza kupelekea usumbufu na hasara kwa yule anayefanyiwa au wote wawili. Ntaelezea mkasa ulionipata mimi last week
Ni hivi, kuna kijisehemu nafanya kazi tupo na wenzangu kama watano hivi, tumezoea kutaniana utani wa kawaida wa maneno. Siku hiyo tulikuwa tumefunga shughuli zetu za siku tukaanza kutawanyika. Mimi nikaenda hatua kama tano nikagundua sina simu. Moja kwa moja nikajua nimeacha ndani nikarudi.....nilipofika ndani sikukuta simu, nikachukua simu ya mmoja wa wenzangu nikapiga ikawa inaita tu...nikatafuta wee nikaambulia patupu....ikabidi nisaidiwe....tukatafuta kama nusu saa hola....baadae ikawa haipatikani (imezimwa)
Nikakata tamaa nikaamua kuondoka nikiamini simu nimedondosha maana ilikuwa ni giza na kulikuwa na watu wengi maeneo hayo.
Siku inayofuata nikaenda mlimani kurudisha laini....zile namba tano ulizopiga mara ya mwisho zikakataa ikaonekana sikupiga kwa hiyo nikashindwa kurudisha line....nikaondoka nikitegemea kesho nitaenda kibaruani nitachukua za wafanyakazi wenzangu maana tulipigiana siku hiyo.
Nikarudi hom nilikuwa na nokia tochi betri imekufa....nikaenda kununua betri pamoja na chaja...jumla nlitumia 15000.....nikanunua na lain ya mtandao mwingine nnaposubiri kurudisha ile ya siku zote(jumapili hiyo)
J3 nimeenda kibaruani nikaanza kukusanya namba akajitokeza mmoja kasema usiende...kwa ufupi tu ni kwamba simu aliificha yeye. Kwa muda huo sikusema chochote maana nilifurahi kupata simu yangu niliyoamini imepotea...baadae nkamuuliza kwa nini alifanya vile?
Nikamuelezea na gharama nliyotumia nikamwambia vipi kama ningefanikiwa kurudisha line si ina maana data zangu ndo ningekuwa nimepoteza? Akaniambia eti siku anachujkua alijua siku inayofuata ni ya kazi kwa hiyo alificha akijua asubuhi yake atanipa.
Je wewe mwanajamiiforums umewahi kufanya/kufanyiwa utani ambao pasipo kutegemea ukajikuta unapata hasara wewe au mwenzio?
Yawezekana ulifanya kwa nia ya kufurahi lakini matokeo yake pasipo kutegemea yakakugharimu pesa, muda au heshima yako?
Naamini lipo la kujifunza hapa...karibuni